NAMNA YA KUTUNZA AFYA KUANZIA JIKONI

NAMNA YA KUTUNZA AFYA KUANZIA JIKONI

Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote

NAMNA YA KUTUNZA AFYA KUANZIA JIKONI

AFYA NA JIKO
Itambulike kuwa utaratibu mwema wa kupangilia chakula ni katika kanuni za afya na ni katika mbinu zitakazoboresha afya yako. Ila pia ijulikane kuwa mama wa jikoni anapaswa apewe elimu ya lishe na namna gani kazi yake jikoni ni muhimu sana. Katika kipengele hiki tutaangalia namna ambavyo jiko linaweza kuwa ni tiba kwa afya zetu. Hapa tutaangalia namna ambavyo viungo vya chakula na matunda huweza kuboresha afya ya mtu.
v Nyumba nyingi zimekuwa na utaratibu wa kumuachia mpishi achague mwenyewe nini kupikwe na ni aina gani ya matunda yaliwe. Na mara nyingi maamuzi haya hutegemea kipato cha pesa ambacho familia humiliki. Baada ya kusoma daraa hili utagunduwa kuwa hata kama familia inamiliki kipato kidogo lakini afya ya familia inaweza kuboreka kwa kupangilia mapishi. Maamuzi haya pia unaweza kuyaamua kwa kuangalia:- 1.rangi za vyakula na virutubisho vilivyomo.
2.Virutubisho vilivyomo
3.Faida za vyakula hivyo mwilini

Bila ya kupoteza muda hebu tuanze na namna ya kutambua virutubisho kwenye matunda na mboga kwa kuangalia rangi zao.

RANGI ZA MATUNDA NA MAANA YAKE.
Mama wa jikoni anaweza kutambua virutubisho vilivyomo kwenye chakula au matumnda pindi anapoandaa chakula chake. Sasa hebu chukuwa elimu hii na kisha umueleze mama wa jikoni ili kusaidia maboresho ya afya ndani ya nyumba.

Unaweza kujiuliza ni kwa nini matunda yana rangi mbalimbali? Hili swali Mwenyezi mungu aliyeumba kila kitu ndiye anajuwa zaidi. Ila kwa ufupi utambuwe kuwa rangi katika matunda ni dalili ya ishara flani. Katika post hii tutaona baadhi ya rangi katika matunda. Mwisho wa post hii utaweza kutambua nini kimo katika tunda utakaloliona kwa kuangalia rang.

1.rangi nyekundu
Rangi nyekundu kwenye matunda hutokana na nyembenchembe ziitwazo lycopene. Hizi ni antoxidant ambazo husaidia katika kulinda mwili dhidi ya sumu za vyakula. Sumu hizi mara nyingi huweza kuharibu seli ndani ya miili yetu. Pia sumu hizi husababisha mtu kuzeeka haraka. Chembechembe hizi pia husaidia katika kuzuia uharibifu wa seli mwilini. Huimarisha mfumo mzima wa kinga mwilini. Na pia husaidi akatika kulinda au kupunguza adhari za magonjwa ya moyo na saratani.matunda yenye rangi hii ni pamoja na tomato, matikiti, pilipili n.k

2.rangi ya njano. Rangi ya njano kwenye matunda husababishwa na chembechembe ziitwazo beta-carotene, hizi pia ni antoxidant. Chembechembe hizi husaidia kuimarisha mfumo wa kinga mwilini. Mwili huweza kubadili beta-carotene, kuwa vitamini A. Itambulike kuwa vitamini hivi ni muhimu sana katika afya ya mtu. Kupamabana mna maradhi mablimbali nna kuimarisha afya ya macho. Kupambana na wadudu wanaosababisha vidonda vya tumbo. Huimarisha afya ya ngizi na maeneo mengune yenye utando laini.miongoni mwa matunda yenye rangi hii ni viazi, karoti, maembe n.k

3.rangi ya kijani.
Rangi ya kijani husaidia kutambuwa uwepe wa vitamini Ana C. Kama inavyotambulika mboga za majani zina rangi hii. Vitamini A na C huweza kupatikana kwa wingi kwenye rangi hii. Itambulike kuwa vitamini hivi ni muhimi katika kudhibiti mfumo mzima wa kinga mwilini. Upungufu wowote wa vitamini hivi viwili uanaweza kusababisha madhara makubwa mwilini.

4.rangi ya bluu na violet
Rangi hii hutambulisha uwepo wa anthocyanin ambayo ni antioxidat. Itambulike kuwa antioxidant ndizo ambazo kupambana na sumu mbalimbali ndani ya mwili na hatari zingine. Sumu hizi zinasababishwa ba vyakula tunavyokula kwa kiasi kikubwa. Vyakula hivi vyenye rangi hii huwa vina vitamini C kwa kiasi kikubwa. Pia vyakula hivi vina kambakamba ambazo ni muhimu sana katika afya ya mtu.

KUANGALIA VIRUTUBISHO NA UMUHIMU WA VYAKULA HIVYO
Watu wengu hawatambui namna gani viungo vinavyokutika jikoni kupikia vina umuhimu sana kwa afya ya mtu. Katika post hii tutaona viungo vya kupikia na umuhimu wake. Post hii itakuwa endelevu, hivyo ni vizuri uwe unapata upadate zetu kila baada ya siku chache.

1.kitunguu saumu. Watu wamekuwa wakitumia kiungo hiki kwa kupikia toka enzi za mababu. Halikadhalika kiungo hiki kimekuwa kikitumika kama dawa kwa karne nyingu, maeneo mengi duniani. Utafiki unaonesha kuwa katika kitunguu saumu kuna ‘allicin’ hii husaidia katika kuimarisha mfumo wa kinga katika kupambana na maradhi mbalimbali. Tumia kiungo hiki kwa kupikia. Pia unaweza kutafuna punje zake. Watu wenye maradhi mablimbali wamekuwa wakitumia kiungo hiki na kuona mafanikio.

2.Pilipili kali. Watu wengi wamekuwa wakiacha kutumia pilipili etu kwa sababu ya ukali wake. Ila itambulike kuwa ijapokuwa ni kali lakini ila faida nyingi sana kwa afya ya mtu. Pilipili pia ina vitamini c ndani yake kwa kiasi. Vitamini hivi ni muhimu sana katika mfumo mzima wa kinga ya mwili dhidi ya magonjwa na wadudu shambulizi.

3.Karoti. Watu wengi wanafahamu kuwa karoti ni mujarabu katika maatizo ya macho. Karoti huimarisha afya ya macho yako. Tafiti zinaonyesha kuwa karoti husaidia kwa mtu mwenye vidonda vya tumbo. Kariti ni kiungo safi kwa mboga ni ni dawa iliyo nzuri. Unaweza kutumia karoti kwa kutafuna, kutengeneza juisi, kachumbari iliyochanganywa na kabichi n.k

4.Tangaizi. Kiungo hiki mara mara nyingi hutumika kwenye chai. Pia hutumiwa kwenye mchuzi japo sio kawaida. Tangaizi hutibu maradhi mengi lakini ni mujarabu sana kwa tatizo la nguvu za kiume. Tutaizungumza vizuri tangaizi kwenye post zetu zijazo.

5.Tomato (nyanya). Kwa kawaida matunda yenye rangi nyekundu kama tikiti na nyanya yana virutubisho viitwavyo “lycopene.” ( antioxidant called lycopene.). Hii huweza kudhibiti mfumo wa kinga usidhurike kirahisi. Halikadhalika lycopene ni mujarabu kwa kupumguza adhari za shambulio la moyo na saratani. Lyopene husaidia kuzuia uharibifu wa seli mwilini.

Ndani ya tomato kuna aina za carotenoid kama vile: lutein na lycopene. Hizi husaidia katika kuimarisha afya ya macho. Au kupunguza athari zinazotokana na mwanga zisidhuru macho. Tomato ni katika matunda ambayo yauwezo mkubwa wa kulinda mwili dhidi ya maradhi. Pia huweza kuuwa seli za saratani.

Tomato zina vitamini C kwa wingi. Wataalamu wa afya wanaeleza kuwa vitamini hivi vina kazi kubwa ya kulinda mwili na maradhi mbalimbali. Pia vitamini hivi vinakazi ya kuzuia utengenezwaji wa seli bila ya mpangilio yaani seli za saratani.

Tomato huweza kupunguza presha kwa wale wenye tatizo la kupanda kwa presha yaani shinikizo la damu. Wataalamu wanaeleza kuwa kutumia kudhibiti kiwango cha sodium yaani madini ya sodiam hali hii husaidia katika kurekebisha shinikizi la damu.


                   



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 91


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

NAMNA AMBAZO MWILI HUPAMBANA NA MARADHI
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

darasa la afya
Soma Zaidi...

KIJUWE KISUKARI CHANZO CHAKE, DALILI ZAKE NA KUKABILIANA NACHO
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

MARADHI YASABABISHWAYO NA HALI ZA MAISHA
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

Dondoo za afya 1-20
Somo Hili linakwenda kukuletea dondoo mbalimbali za afya Soma Zaidi...

Zijuwe faida za kiafya za kula Zabibu
Kula zabibubkina faida nyingi kwa afya yako. Soma Zaidi...

Nina shida hiyo maumivu chini ya tumbo upande wa kushoto na mkojo wa kahawia sana na unatoa arufu
Kama unapatwa na maumivu ya tumbo na ilhali mkojo ni mchafu, ama una harufu sana, basi post hii ni kwa ajili yako. Soma Zaidi...

Safari ya damu kwa Kila siku
Posti hii inakwenda kukuletea mfumo wa damu mwilini na safari zake za Kila siku Soma Zaidi...

MAGONJWA 7 YALETWAYO NA MBU: MALARIA, DENGUE, HOMA YA ZIKA, HOMA YA MANJANO
Soma Zaidi...

AFYA YA UZAZI (UJAUZITO, KULEA WATOTO, AFYA YA MIMBA NA MTOTO, MAGONJWA YA KINAMAMA NA WANAUME)
Soma Zaidi...

Kauli za wataalamu wa afya
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu kauli mbalimbali za wataalamu wa afya Soma Zaidi...

MARADHI YASABABISHWAYO NA HALI ZA MAISHA
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...