MAANA YA AFYA, ni nani aliye na afya?

Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote

MAANA YA AFYA, ni nani aliye na afya?

MAANA YA AFYA
Afya ni hali ya kuwa mzima kimwili na kiakili. Kuna mahusiano makubwa kati ya kuwa mzima kimwili na akili. Mtu anaweza kuwa mwili upo mzima kabisa lakini akaambiwa hana afya salama kwa maana anaweza kuwa akili yake haipo vizuri. Kuathirika kiakili pia ni ugonjwa na ndio maana kuna wagonjwa wa sikolojia.

Hivyo mtu mwenye afyqa ni yule a,baye ni mzima wa mwili na akili. Na tunaposema akili haimaanishwi mgonjwa wa akili ni yule mkichaa hapa na bali hata ambaye saikolojia yake haipo vizuri nae ni mgonjwa.

Ndani ya mwili wa binadamu kuna mifumo ambayo hiyo kazi yake ni kuhakikisha kuwa mwili haudhuriki kimwili na kiakili. Mifumo hii ipo kazini muda wowotw kupambana na mamilioni ya wadudu hatari waliopo kwenye mazingira yetu. Kwa mfano kwenye hewa kuna mabilioni ya wadudu kama bakteria ambao huambukiza maradhi.

Mwili unaweza kuthibiti maradhi kupitia njia zake nyingi kwa mfano;- katika mfumo wa damu kuna seli hai nyeupe za damu hizi zinapambana na vijidudu vya maradhi. Halikadhalika mna katika damu antibodies hizi zinafanya kazi hii pia. Kwenye mfumo wa mmeng’enyo wa chakula kuna asidi ambazo zinakazi ya kuuwa bakteria na vijidudu vingine vya maradhi. Kwenye mfumo wa upumuaji kuna uttelezi na vijinywele ambavyo hukamata vijidudu pamoja na mavumbi na kutolewa nje.

Hivyo mwili una mfumo madhubuti kabisa wa kuweza kupambana na maradhi. Na ikitokea umepambana na kushindwa hapo hutokea mtu akaumwa. Pia ijulikane kuwa kinga za mwili zinaweza kutengenezwa na mwili wenyewe au kuzipata kwa kutumia chanjo. Mwili huanza kutengeneza kinga hizi hata kabla ya kuzaliwa kwa mtoto na hivyo hivyo mwili huendelea kuzitengeneza kinga hizi wakati wa kukua na kuendelea kwa maisha baada ya kuzaliwa.

Pia wakati mwingine mapambano yanapokuwa makali ndani ya mwili huweza kutokea maumivu katika sehemu za mwili. Kwamfano mfumo wa lymph unapopambana vikali huweza kusababisha maumivu ya mtoki.


                   

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Jiunge nasi WhatsApp
Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Jifunze Main: Afya File: Download PDF Views 516

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
πŸ‘‰1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    πŸ‘‰2 Dua za Mitume na Manabii    πŸ‘‰3 Madrasa kiganjani    πŸ‘‰4 Kitabu cha Afya    πŸ‘‰5 Simulizi za Hadithi Audio    πŸ‘‰6 web hosting   

Post zinazofanana:

Nini maana ya Afya

Maana ya afya ni pana sana tofauti na vile ambavyo sisi tunajuwa. Afya inahusisha mambo mengi sana.

Soma Zaidi...
darasa la lishe

Jifunze mengi kuhusu afya na lishe, ujuwe utaratibu wa lishe

Soma Zaidi...
Jinsi ya kumsaidia Mtoto mdogo aliyekabwa na kitu kooni

Mfano wa kitu kinachoweza kumaba mtoto kooni ni kama chagula kigumu, pesa ya sarafu, kijiwe na mengineyo. Endapo hili litataokea msaada wa haraka unahitajika kwa ulazima.

Soma Zaidi...
darasa la lishe

Jifunze mengi kuhusu afya na lishe, ujuwe utaratibu wa lishe

Soma Zaidi...
madhara ya tezi dume

Endapo tezi dume haitatibiwa ama itachlewa kutibiwa basi mtu anaweza kupata madhara. katika post hii utakwenda kuyajuwa madhara ya tezi dume kwenye Mwili

Soma Zaidi...
MAZINGIRA

Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote

Soma Zaidi...
AFYA NA MAGONJWA

Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote

Soma Zaidi...