Sifa za wanafiki zilizotajwa katika surat Al-Imran

Sifa za wanafiki zilizotajwa katika surat Al-Imran

Na kuwapambanua wale waliokuwa wanafiki.

Jiunge nasi WhatsApp
Upate Update zetu

Sifa za wanafiki zilizotajwa katika surat Al-Imran

Sifa za wanafiki zilizotajwa katika surat Al-Imran


Na kuwapambanua wale waliokuwa wanafiki. Nao waliambiwa: "Njooni mpigane katika njia ya Mwenyezi Mungu au mzuie (maadui pamoja na sisi)" Wakasema: "Tungejua kuwa kuna kupigana bila ya shaka tungelikufuateni." Wao siku ile walikuwa karibu na ukafiri kuliko na Uislamu (japokuwa siku zote wakidhihirisha Uislamu wa uwongo). Wanasema kwa midomo yao yasiyokuwa nyoyoni mwao. Na Mwenyezi Mungu anajua vyema (yote) wanayoyaficha. (3:167)


Wale waliosema juu ya ndugu zao - na (wao wenyewe) wamekataa kwenda (hawakwenda) vitani: "Wangalitutii wasingeuawa." Sema: "Jiondoleeni mauti (nyinyi) wenyewe msife maisha ikiwa mnasema kweli." (3:168)



"Wala usiwadhani wale waliouawa katika njia ya Mwenyezi Mungu kuwa ni wafu (maiti). Bali wahai, wanaruzukiwa kwa Mola wao." (3:169).
Kutokana na aya hizi tunapata sifa za wanafiki zifuatazo:



(i)Hawako tayari kujitoa muhanga kupigania dini ya Allah (s.w) isimame katika jamii au kuihami isiangushwe baada ya kusimama kwake.



(ii)Wanasema kwa midomo yao yasiyokuwa nyoyoni mwao. Baada ya mapambano dhidi ya maadui wa Dini ya Allah (s.w) kwisha, wanafiki hujikosha kwa kusema uwongo kuwa hawakuwa na taarifa juu ya mapambano ya Waislamu dhidi ya maadui zao, vinginevyo wangelikuwa Pamoja katika vita hivyo hali ya kuwa walijificha wasiende vitani kwa kuogopa kufa.



(iii)Huwabeza na kuwalaumu wale wanaouliwa au kupata misuko suko katika kuupigania Uislamu.
Katika aya ya 168 na 169 (3:168-1 69), Allah (s.w) anawasuta wanafiki na kuwakatisha tamaa kuwa mtu hafi kwa kuwa amepigania dini ya Allah (s.w), bali kila mtu atakufa kwa ajali yake aliyopangiwa:



“… Sema: (uwaambia wanafiki): "Jiondosheeni mauti (nyinyi wenyewe msife milele) ikiwa mnasema kweli."



Pia Allah (s.w) anawakatisha tamaa wanafiki na kuwatumainisha waumini kuwa hapana jambo lililozuri na bora kwa mtu kuliko kufa katika njia ya Allah (s.w) (kufa shahidi).




                   


Download Post hii hapa

Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Jifunze Main: Dini File: Download PDF Views 660

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani    👉2 kitabu cha Simulizi    👉3 Kitabu cha Afya    👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉5 Kitau cha Fiqh    👉6 Simulizi za Hadithi Audio   

Post zinazofanana:

(ix)Wenye kuhifadhi swala
(ix)Wenye kuhifadhi swala

Waumini wa kweli waliofuzu huhifadhi swala kwa kutekeleza kwa ukamilifu shuruti zote za swala nguzo zote za swala na huswali kama alivyoswali Mtume (s.

Soma Zaidi...
Zoezi la 3
Zoezi la 3

Kipengele hichi kina maswali mbalimbali kuhusiana na dini na mitazamo mbalimbali.

Soma Zaidi...
quran na sayansi
quran na sayansi

2; mbegu ya uhai uliyo changanyikaUmbile la mwanadamu limepitia hatua nyingi sana kama tutakavyoendelea mbele kuonalakini ukiachilia mbali na hatua zote alizopitia mwanadamu wakati wa kuumbwa lakiniumbile la mwanadamu bado limebakia kuwa dhalili kama ALLA

Soma Zaidi...
NENO LA AWALI
NENO LA AWALI

Darasa la elimu inayohusu ujauzito na namna ya kulea mimba

Soma Zaidi...
Uandishi wa hadithi wakati wa maswahaba wa mtume (s.a.w)
Uandishi wa hadithi wakati wa maswahaba wa mtume (s.a.w)

Sunnah na hadithi (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Iv shekh haifai kufunga kwa nia utimize jambo labda kuna kitu unakitaka kwhy unaamua kugunga ili kama kuzidisha maombi kwa mungu jambo lifanikiwe
Iv shekh haifai kufunga kwa nia utimize jambo labda kuna kitu unakitaka kwhy unaamua kugunga ili kama kuzidisha maombi kwa mungu jambo lifanikiwe

Ibada yavfubga ni katika ibadavanbazo hufanya nakaribia dini zote kubwa. Ibada hii imekuwaikikabiliw na naswlo mengi.

Soma Zaidi...