(ii)Dai kuwa Qur-an ni zao la njozi za Mtume (s.
(ii)Dai kuwa Qur-an ni zao la njozi za Mtume (s.a.w) zilizovurugika:
Katika miaka ya 1960 waandishi wawili, Anderson na Watt, walikuja na dai kuwa Qur-an ni zao la dhana (Wishful Thinking).
Walidai kuwa maneno na maelezo ya habari mbalimbali yaliyomo katika Qur-an yametokana na mawazo ya Mtume (s.a.w) aliyoyatoa kwa dhana tu. Watt, kwa kutumia njia za kisasa za kuchunguza fasihi alihitimisha kuwa angelifanya makosa makubwa sana kama angeliamini kuwa Qur-an ni ujumbe wa Allah (s.w) kwani: "Kila kinachoonekana kinatoka nje ya fikra za mwanaadamu, kwa kweli hutokana na mawazo yake ya kinjozi ambayo hutokea bila ya kufikiri." Kwa hiyo alieleza Watt kuwa Qur-an ni zao la dhana (Creative Imagination)
Udhaifu wa Dai hili:
Nadharia ya Anderson na Watt haina nguvu yoyote kwa sababu katika historia nzima ya mwanaadamu hapajatokea mawazo ya kinjozi hata yawe yamebuniwa kwa uhodari kiasi gani yakaunda kitabu mithili ya Qur-an au hata angalau sura moja iliyo mithili na sura yoyote ya Qur-an. Hata hivyo, jambo la kukumbuka ni kwamba dai hili la Anderson na Watt na makafiri wengine wa kisasa wenye mawazo kama hayo, si geni bali ni dai kongwe lililotolewa na jamii ya Mtume (s.a.w) mwenyewe kama tunavyofahamishwa katika Qur-an:
"Lakini (Makafiri) walisema: "(Hayo anayosimulia) ni ndoto zilizovurugika. Bali ameyabuni (mwenyewe). Bali huyu ni mtunga mashairi tu.Basi atuletee Muujiza kama walivyotumwa (Mitume) wa kwanza." (21:5)
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya hapa chini kuipakua sasa!
Umeionaje Makala hii.. ?
Sura mbili hizi pia hujulikana kwa jina la al muawidhatain ambazo ni surat an Nas na surat al falaq.
Soma Zaidi...Sura hii ni katika sura za kitawhidi sana. Maulamaa wanasema inatosha sura hii kuwa ni mawaidha. Imamu sharifu anasema kuwa sura hii inatosha kuwa muongozo…
Soma Zaidi...Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu srat al fatiha, faida zake na maudhui zake
Soma Zaidi...SURATUL-KAFIRUN Imeteremshwa maka na inaelezwa katika sababu za kushuka kwake ni kuwa Kundi la makafiri lilimfuata mtume (s.
Soma Zaidi...Sira na historia ya Mtume Muhammad s.a.w , sehemu ya 19. Hapa utajifunza maisha ya Mtume kabla ya utume.
Soma Zaidi...