VYNZO VYA MINYOO Kama tulivyoona hapo mwanzo kuusu aina za minyoo, pia tumeona vyanzo vya minyoo hao kulingana na aina zao.
VYNZO VYA MINYOO
Kama tulivyoona hapo mwanzo kuusu aina za minyoo, pia tumeona vyanzo vya minyoo hao kulingana na aina zao. Hapa ninakwenda kukuorodheshea kwa ufupi vyanzo hivi vya minyoo kwa ujumla wao na makundi yao:
1.kula kitu kisichooshwa kwema kwa maji yaliyo safi na salama. Wakati mwingine kuosha tu haitoshelezi, maana unaweza kuosha kwa maji ambayo yana vimelea vya minyoo, hivyo unajikuta hukufanya kitu. Kwani minyoo wanaishi ardhini, kwenye majani na kwenye maji.
2.Kunywa maji ambayo si masafi na si salama. Maji machafu yanaweza kuwa na mayai ama lava wa minyoo hii. Maji ambayo yamechanganyika na choo kikubwa yanakuwa na mazalia ya minyoo hii. Ni vyema kuchemsha maji hata yachemke, yapozwe na yahifadhiwe vyema kwa matumizi ya nyumbani na hata biashara.
3.Kula nyama ambayo haikuiva vyema, ama nyama mbichi. Upikaji wa nyama yeyote unatakiwa uwe wa makini sana. Kuhakikisha kuwa nyama imewiva vyema. Kuna baadhi ya nyama zinashauriwa kuwa makini sana katika kuzipika kama nyama ya ngurue na ya punda. Pia kuna aiana za samaki nao wanahitajika kuwapika vyema kama samaki aina ya kaa.
4.Kutembea pekupeku kwenye ardhi yeye minyoo. Minyoo huweza kuishi kwenye udongo, na ikitokea my akatembea bila ya viatu katika eneo hili, minyoo hawa wanaweza kupenya kwenye ngozi yake na kuingia mwilini.
5.Kula udongo, tunaona sana mara nyingi watu wanakula udongo, ukweli ni kuwa sio kila udongo unakuwa na minyoo. Kama utakuwa umeandaliwa vyema unaweza kuwa hauna minyoo. Lakini kula udongo kunaweza kusababisha minyoo. Pia kuna madhara makubwa sana ya kiafya katika kula udongo.
6.Kinyesi cha wanyama na binadamu. Hivi ni vyanzo vizuri sana vya minyoo. Kwani minyoo wanaweza kuishi kwenye kinyesi vyema na kwa muda mrefu zaidi kuliko maeneo mengine.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi Ugonjwa wa ukoma ni Ugonjwa unaosababishwa na bacteria anayejulika kama mycobacterium leprae.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi magonjwa ya kurithi ambayo hubebwa na vinasaba vya urithi kutoka kizazi kimoja kwenda kingine.magonjwa haya hata hivyo ,si kila kasoro huwa ni ugonjwa kwa mtu mfano ,ualbino na kitoweza kutofautisha rangi kama vile nyekundu na kija
Soma Zaidi...Mnamo mwaka 2016 World Health Organization (WHO) iliitisha kikao cha dharura mnamo mwezi tarehe 1 mwezi wa pili mpaka tarehe 13 mwezi wa nne.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi sababu mbalimbali za kuwepo kwa saratani ya ini, saratani hii imekuwa tishio kwa wengi ila ni vizuri kujua baadhi ya sababu ambazo uchangia sana kuwepo kwa tatizo hili la saratani ya inni.
Soma Zaidi...Kaswende ni maambukizo ya bakteria ambayo kawaida huenezwa kwa kujamiiana. Ugonjwa huu huanza kama kidonda kisicho na maumivu kawaida kwenye sehemu zako za siri, puru au mdomo. Kaswende huenea kutoka kwa mtu hadi mtu kupitia ngozi. Kaswende ya Mapema
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi matibabu ya kutibu ugonjwa wa maumivu chini ya kitovu.
Soma Zaidi...Post hii fupi inakwenda kukujuza juu ya tatizo la fangasi na nini ufanye.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi namna ya kuzuia maambukizi kwenye tumbo na utumbo mdogo, hizi ni njia ambazo zinapaswa kufuatwa ili kutokomeza kabisa maambukizi kwenye tumbo na utumbo mdogo.
Soma Zaidi...Jibu ni hapana, matehayawezi kuambukiza HIV. Lakini swali unalotakiwa kulijibu je ni kwa nini mate hayaambukizi. Makala hii itakwend akukupa majibu haya
Soma Zaidi...Huwenda ukawa ni moja kati ya watu wanaotaka kujuwa juu ya dalili za ukimwi. Kama wewe ni katika watu hawa tambuwa kuwa kuna dalili za VVU (hiv) na dalili za ukimwi. Makala hii itakwenda kukuletea dalili kuu za mwanzo za VVU na HIV kuanzia wiki tatu za mw
Soma Zaidi...