SIFA ZA CERVICAL MUCUS
Majimaji haya pia huwenda kuambatana na dalili za mashambulizi ya bakteria na fangani endapo yatakuwa na harufu mbaya na rangi ya kijani.
Majimaji haya yasichananywe na uchafu utokao kwenye uke kwa sababu ya bakteria, fangasi ama saratani ya kizazi.
Baada ya hedhi uke huwa mkavu hivyo majimaji haya yanakuwa ni macgache na si yenye mtelezo wowote. Hayana rangi yeyote na wala huwezi kuyapata kwa wingi. Hii huashiria kuwa muda huu mwanamke hawezi kupata ujauzito.
Siku chache baadaye majimaji yataanza kuonekana yakiwa na muonekano wa kuweza kunatanata, majimaji haya sio mepesi kabisa. Huu ni mwanzo wa kuandaliwa mazingira ya kupevushwa kwa yai.
Baada ya siku chache tu yai linakaribia kutolewa, muda huu majimaji haya yanakuwa mepesi, laini, mengi na yenye rangi nyeupe. Haya maji ni kiashiria kuwa sasa yai lipo njiani kutolewa. Huu ni muda muafaka zaidi kwa wanaotafuta mtoto.
Siku moja ama mbili kabla ya yao kutolewa majimaji haya yanafanana sana na majimaji ya weupe wa yai, yaani kama yale majmaji meupe yanayooekana pindi linapopasuliwa yai. Majimaji haya yanaweza kuvutika kwenye vidole na yanateleza sana. Hii ni ishara kuwa yai limekaribia kutolewa eidha kwa siku moja ama mbili.
Punde baada ya yai kutolewa majimaji haya yanaanza kuwa makavu na kupoteza mtelezo. Ama uke unakauka na kuwa mkavu na kurudi katika hali ya kawaida. Na kama mimba ilitungwa majimaji haya yanakuwa na rangi ya maziwa. Hivyo ni vyema kuchunguza vizuri ili kujuwa kama mimba ilitungwa au laa.
Pia ijulikane kuwa kuna wanawake wengine hawana majimaji haya na pia kuna wengine ambao majimaji haya ni mengi sana zaidi ya kawaida. Hivyo katika kuchunguza hali hizi wanawake wa aina hii ni ngumu sana kwao.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi umuhimu wa kunyonyesha kwa akina Mama, kunyonyesha ni kitendo ambacho Mama utumia maziwa yake na kumlisha mtoto pindi tu anapozaliwa mpaka wakati anapoachishwa titi, kunyonyesha huwa na faida kubwa kwa wote yaani Mama na mtoto, zif
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi njia ambazo tunaweza kutumia ili kuweza kupunguza tatizo hili la kutanuka kwa tezi dume, kwa hiyo tunaweza kutumia njia zifuatazo ili kuweza kupunguza tatizo hili kwenye jamii kama ifuatavyo.
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na Utasa wa Mwanaume hutokana na uzalishaji mdogo wa mbegu za kiume, utendakazi usio wa kawaida wa manii au kuziba kwa manii ambayo huzuia utoaji wa mbegu za kiume. Magonjwa, majeraha, matatizo ya kiafya sugu, u
Soma Zaidi...Kukoma hedhi hufafanuliwa kuwa hutokea miezi 12 baada ya kipindi chako cha mwisho cha hedhi na huashiria mwisho wa mizunguko ya hedhi. Kukoma hedhi kunaweza kutokea katika miaka ya 40 au 50. Kukoma hedhi ni mchakato wa asili wa kibaolojia. Ingawa pia in
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukupa njia za kukusaidia kuacha punyeto.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi imani potofu kwa mwanamke mwenye mimba, ni Imani ambazo zimekuwepo kwenye jamii kuhusu wanawake wenye mimba.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi huduma kwa mtoto mwenye shida ya kupumua, mtoto kama ana shida ya kupumua tunaangalia dalili kwanza na baadaye tunaweza kutoa huduma kulingana na Dalili.
Soma Zaidi...Jifunze mengi kuhusu Afya, kuwa nasi kwenye makala hii hadi mwisho.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi sababu mbalimbali ambazo zinamfanya mama au dada kutobeba mimba. Kwa hiyo tutaziona hapo chini kama ifuatavyo.
Soma Zaidi...