Posti hii inahusu zaidi vyanzo vya kuwepo kwa sumu mwilini, kwa sababu kuna wakati mwingine tunapata magonjwa na matatizo mbalimbali ya ki afya tunaangaika huku na huko kumbe sababu kubwa ni kuwepo kwa sumu mwilini na vyanzo vya sumu hiyo ni kama ifuatavy
1. Matumizi ya dawa za mara kwa mara.
Kuna wakati mwingine watu wanatumia dawa mara kwa mara kwa sababu ya kuwepo kwa matatizo mbalimbali kwenye mwili na kusababisha kuongezeka kwa sumu mwilini kwa sababu ya matumizi ya dawa.
2. Kuna matumizi ya pombe kupita kiasi.
Kuna watu wanaotumia pombe kupita kiasi , tunajua kwa kawaida kwenye pombe kuna chemicals mbalimbali kwa hiyo kwa sababu ya matumizi ya kupita kiasi kuna uwezekano wa kuongezeka kwa sumu mwilini
3. Mazingira hatarishi kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia, mazingira nayo yanasababisha kuongezeka kwa sumu mwilini kwa sababu ya kuwepo kwa wingi wa viwanda kila sehemu kwa hiyo kuna sumu mbalimbali ambazo zinaweza kusababisha kuwepo kwa sumu mwilini.
4. Kutokuwepo kwa mlo kamili.
Kwa sababu ya hali duni ya watu walio wengi usababisha pia kuongezeka kwa sumu mwilini kwa sababu ya vyakula vinavyotumika.
5. Matumizi ya madawa makali na ya mara kwa mara, Kuna wagonjwa ambao wanaotumia madawa makali na ya Mara kwa mara nayo uongeza Sumi mwilini.
6. Uzito mkubwa kupita kiasi.
Kwa sababu ya uzito mkubwa mafuta mengi huwa yanarundikana hali ambayo usababisha kuongeza kwa Sumi mwilini.
7. Mtindo wa maisha.
Kuna watu wengine wanaishi kwa kutumia vyakula vya mafuta na chemical kila siku na kutumia vinywaji vyenye kemikali nyingi hali ambayo usababisha kuwepo kwa Sumu nyingi mwilini.
8. Matumizi ya njia za uzazi wa mpango.
Kuna wakati mwingine unakuta mama anautumia njia ya kwanza ya uzazi wa mpango inagoma anabadilisha na kufanya nyingine nayo inagoma kwa hiyo anaweza kutumia njia zaidi ya mbili na kwa kutumia chemical mbalimbali ambazyutokana na dawa hizo hali ambayo usababisha kuongezeka kwa Sumu mwilini.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Huu ni ugonjwa wa fangasi wanaosababishwa na mashambulizi ya fangani aia ya yeast waitwao candida.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi njia ambazo zinaweza kutumika Ili kuweza kupunguza kuwepo kwa magonjwa ya zinaa
Soma Zaidi...Posti hii inaelezea ugonjwa wa kisakari, dalili zake,na namna ya kujikinga usipate kisukari au Kama tayari unakisukari ukijikinga madhara yanapungua au kupona kabisa.Kisukari au bolisukari (jina la kitaalamu: diabetes mellitus) ni ugonjwa unaoonyesha viwa
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi Dalili zinazoweza kujitokeza baada ya sehemu ya kupeleka taarifa kwenye ubongo imearibika, kwa hiyo mambo yafuatayo yakijitokeza utajua wazi kuwa kuna matatizo kwenye mfumo wa kupeleka taarifa kwenye ubongo.
Soma Zaidi...Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote
Soma Zaidi...Posti hii inakwenda kukuletea dalili za fangasi wa sehemu za Siri kwa wanaume
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi sababu mbalimbali za kuwepo kwa saratani ya ini, saratani hii imekuwa tishio kwa wengi ila ni vizuri kujua baadhi ya sababu ambazo uchangia sana kuwepo kwa tatizo hili la saratani ya inni.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi njia za kutambua Dalili za macho makavu, kama tulivyotangulia kuona kubwa macho kuwa makavu Usababishwa na sehemu ya kuzalisha maji kwenye jicho kushindwa kufanya kazi na jicho hilo huwa kavu na Dalili zake ni kama ifuatavyo.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dalili za ugonjwa wa inni, hizi ni dalili ambazo ujitokeza kwa mtu Mwenye ugonjwa wa inni, Dalili zenyewe ni kama ifuatavyo.
Soma Zaidi...