Upungufu wa damu, dalili zake na vyakula vya kuongeza damu


VYAKULA VYA KUONGEZA DAMUDamu ni tishu iliyo katika kimiminika. Katika miili yetu damu ina kazi ya kusafirisha viinilishe na hewa ya oksijeni na kuondoa hewa chafu ya kabonidaiyoksaidi mwilini. Pia urekebishwaji wa joto na usafirishwaji wa homoni ndani ya mwili hutegemea damu. Kwa ufupi damu in akazi nyingi. Upungufu wowote wa damu mwilini unaweza kuleta athari nyingi mbaya za kiafya mwilini. Makala hii inakwenda kukueleza njia ya kuongeza damu kwa haraka.


Kazi za damu mwilini
1.Kusafirisha viinilishe kutoka katika mfumo wa mmeng’enyo wa chakula kwenda maeneo mbalimbali ya mwili.
2.Kusafirisha hewa ya oksijeni kutokakwenye mapafu kwenda maeneo mengine ya mwli.
3.Kusafirisha hewa ya kabonikaiyoksaidi kutoka kwenye seli na kpeleka kwenye mapafu kwa ajili ya kutolewa nje
4.Kudhibiti joto la mwili kwa kulipooza inapohitajika na kuliongeza inapohitajika
5.Kusafirisha homoni kwenda maeneo mbalimbali ya mwili.


Vyakula vya kuongeza damu mwilini
1.Nyama nyekundu kama nyama ya ng’ombe, mbuzi. Kondoo
2.Maini
3.Nyama ya figo
4.Mboga za rangi ya kijani kama mchicha na apinachi
5.Maharagwe
6.Kunde
7.Mayai
8.Nafaka nyinginezo
9.Njegere
10.Koeosho na karanga
11.Samaki
12.Nyama ya ndege
13.Karoti
14.Matikiti
15.Zabibu
16.Viazi vitamu
17.Matunda yenye uchachu kama machungwa, ndimu na limao.
18.Polipili nyekundu


Dalili za kupungua kwa damu mwilini
1.Uchovu wa hali ya juu
2.Udhaifu wa mwili
3.Ngozi kuwa na rangi ya njano au mauko
4.Kupumua kwa shida
5.Mapigo ya moyo kutokuwa ya kawaida
6.Kizunguzungu na kichwa kuhisi chepesi
7.Maumivu ya kifua
8.Miguu na mikono kuwa ya ubaridi
9.Maumivu ya kichwaSababu za upungufu wa damu mwilini
1.Upungufu wa madini ya chuma mwilini
2.Upungufu wa vitamini A na B-12 mwilini
3.Maradhi kama HIV, UKIMWI, saratani, mardhi ya figo haya huweza kuleta upungufu wa damu
4.Mfumo wa kinga mwilini kuuwa na kuharibu seli hai nyekundu (autoimmune)
5.Uharibifu wa seli hai nyekundu kufanyika kwa haraka kuliko utengenezwaji.
6.Kuwa na maradhi ya sickle cell