picha

Kazi za protini mwilini ni zipi?

Virutubisho vya protini vina kazi nyingi mwilini. Zifuatazo ndio kazi protini mwilini

Kazi za protini mwilini ni zipi?


KAZI ZA VIRUTUBISHO VYA PROTINI MWILINI



Kwa kuwa sasa tunajua vyanzo vya protini sana ni vyemna tukaziona kazi za protini ndani ya miili yetu. Waandishi wengi wamekuwa wakiandika kazi za protini, na kuziorodhesha katika kazinyingi. Lakini katika makala hii itakuletea kazi zilizo kuu za protini.


1.Kujenga mwili; protini huhusika katika kujenga mwili, na uponaji wa vidonda na majeraha. Mwili kukua vyema na kujengenka vyema protini inahitajika katika kuhakikisha hili linafanyika. Ulaji wa protini ya kutosheleza uanaweza kuufanya mwili uwe katika umbo jema na lililojengeka vyema. Endapo mwili utapata majeraha protini itahusika katika kuziba majeraha na vidonda katika eneo husika. Kama wanavyosema mwili haujengwi kwa matofali, lakini unaweza kusema kuwa protini ndio tofali la kuujenga mwili.


2.Hutumika katika kutengeneza antibodies; hizi ni chembechembe za protini zinazopatikana kwenye damu. Chembechembe hini ni muhiu sana katika mfumo wa kinga. Hizi huweza kuulinda mwili dhidi ya mashambulizi ya maradhi na watutu waletao maradhi. Protini inahitajika ili kutengenezwa kwa chembechembe hizi kufanyike. Hivyo unaweza kusema kuwa protini ni muhumu katika mfumo wa kinga mwilini.


3.Utengenezwaji wa hemoglobin; hemoglobin ni aina za protini, na hii huhusika katika usafirishaji wa hewa ya oksijen na kabondioxide ndani ya miili yetu. Hemoglobin ni chembechembe ambazo ninakazi ya kuchukuwa hewa ya okijeni baada ya mtu kuivuta na kuipeleka kwenye moyp ambapo husambazwa, kwenda maeneo mengine. Kisha hemoglobinhukusanya hewa chafu nyenye kabondaiyokasaidi na kuipeleka kwenye mapafu. Ijapokuwa hemoglobin ni chembehembe za protini lakini pia imetokana na madini ya chuma. Upungufu wa madini ya chuma unaweza kuathiri mfumo wa damu.


4.Utangenezwaji wa enzymes. Hizi ni chembechembe zinazotambulika kama biological catalyst, yaani ni vichochezi vya kuchochoea michakato ya kikemikali iendelee kufanyika ndani ya miili etu. Enzymes huchukuwa nafasi kubwa katika kumenge’enya chakula katika hutau zote na katika maeneo mbalimbali ndani ya mwili. Enzmes zinaweza kupatikana mdomoni, tumboni na katika utumbo mdogo. Umeng’enywaji wa chakula ili tupate vurutubisho enzymes hutumika.


5.Utengenezwaji wa homoni; ili mwili uweze kutengeneza homoni unahitaji protini. Homoni ni chembechembe za kikemikali ambazo husaidia katika kufanya kazi nyingi na tata mwilini. Utengenezwaji wa mayai kwa wanawake na mbegu za uzazi kwa wanaume unahitaji homon. Urekebishwaji wa sukari pia unahitaji homoni. Ilijasho liweze kutoka homoni huhusika katika kurekebisha joto mwilini. Homoni zinakazi nyingi sana mwilini. Lakini jambo la msingi kufahamu hapa ni kuwa homoni hutengenezwa kwa protini.


6.Utengenezwaji wa nywele na vinyweleo na kope pia hutokana na protini. Kama nilivyotangulia kukueleza kuwa protini ni matofali ya kuijenga miili yetu na hii ndio maana yake. Hata nywele zetu kama hatutapata protini ya kutosha katu huwezi kuna na nywele nzuru, na zenye afya ya kutosheleza. Nywele zinaweza kuwa katika hali isiyo ya kawiada ka hutapata protini ya kutosha.




                   


Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 2018-08-01 Topic: Vyakula Main: Afya File: Download PDF Views 2762

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh    👉2 web hosting    👉3 Dua za Mitume na Manabii    👉4 kitabu cha Simulizi    👉5 Simulizi za Hadithi Audio    👉6 Bongolite - Game zone - Play free game   

Post zinazofanana:

Faida za kula uyoga

Kula uyoga kwa faida kubwa, ja unazijuwa faida za kula uyoga kiafya

Soma Zaidi...
Faida za kula Nanasi

Nanasi ni katika matunda matamu lakini mazuri pia kiafya, je unazijuwa faida zake kiafya

Soma Zaidi...
Faida kula fenesi

Somo hili linakwenda kukuletea faida za kiafya za kula fenesi

Soma Zaidi...
Vinywaji salama kwa mwenye kisukari

Vijuwe vinywaji salama kwa mgonjwa wa kisukari

Soma Zaidi...
VYAKULA VYA PROTINI, FATI NA MAFUTA

Je! unatambuwa madhara ya vyakula vya protini na mafuta? ungana nasi kwenye somo hili

Soma Zaidi...
Vyakula vya kuongeza maziwa kwa mama anayenyonyesha

Post hii itakwenda kukufundisha vyakula ambavyo ni vizuri kwa mwanamke anayenyonyesha ili kumsaidia kupata maziwa kwa wingi.

Soma Zaidi...
Kazi kuu tatu za vitamini C mwilini

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu kazi kuu tatu za vitamini C

Soma Zaidi...