Vyakula kwa wagonjwa wa sukari na utaratibu wao wa lishe
Post hii inakwenda kukufundisha utaratibu wa lishe kwa wagonjwa wenye kisukari pamoja na vyakula salamakwao.
Matibabu ya ugonjwa wa kisukari yanagharimu fedha nyingi. Kwa hiyo ni muhimu kuzuia na kudhibiti athari za kisukari mapema. Ili kudhibiti ugonjwa wa kisukari mgonjwa anapaswa kupatiwa matibabu sahihi, kufuatilia na kupima hali yake ya afya mara kwa mara pamoja na kuzingatia mtindo bora wa maisha na taratibu zinazofaa za ulaji wa chakula.
Zifuatazo ni kanuni za ulaji unaofaa zinazopaswa kuzingatiwa na mgonjwa wa kisukari:
1.Kula mlo kamili (angalau mara 3 kwa siku) kwa kuzingatia muda mahususi aliojipangia kwani hashauriwi kukaa na njaa kwa muda mrefu.
2.Dhibiti kiasi cha nishati – lishe (wanga) katika chakula ili kisizidi mahitaji ya mwili. Kiasi kitegemee mahitaji ya mtu binafsi.
3.Ongeza ulaji wa vyakula vyenye makapi – mlo kwa wingi. Kiasi kikubwa cha nishati-lishe kitokane na vyakula vya asili ya nafaka isiyokobolewa, mizizi na ndizi za kupika. Sukari inayotoka katika vyakula hivi hufyonzwa kwa taratibu na hivyo kupunguza kasi ya ongezeko la sukari katika damu.
4.Punguza kiasi cha vyakula vinavyozalisha nishati lishe kwa wingi hususani vyakula vyenye mafuta kwa wingi.
5.Panga utaratibu wa kula chakula na matumizi ya dawa. Iwapo unatumia insulin au dawa za kushusha kiwango cha sukari katika damu unapaswa kujipangia muda wa kula chakula na kumeza dawa ili kuzuia kupungua kwa sukari katika damu. Epuka kukaa kwa muda mrefu bila kula chakula.
6.Kula mbogamboga kwa wingi katika kila mlo.
7.Kula tunda katika kila mlo.
8.Epuka kunywa pombe.
9.Epuka ulaji wa vyakula vyenye sukari nyingi kama soda, keki, biskuti, pipi na asali.
Kanuni nyingine za kuzingatia ni:
1.Punguza uzito iwapo una uzito uliozidi - au dhibiti uzito wa mwili ili usifikie uzito uliozidi. Ni muhimu kuwa na uwiano sahihi wa uzito wa mwili kulingana na urefu wako.
2.Zingatia usafi na usalama wa chakula
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Kitau cha Fiqh 👉2 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉3 Simulizi za Hadithi Audio 👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉5 Kitabu cha Afya 👉6 kitabu cha Simulizi
Post zinazofanana:
Kazi za madini ya Shaba mwilini.
Post hii inahusu zaidi madini ya Shaba mwilini,ni madini ambayo ufanya kazi mbalimbali mwilini, kama ifuatavyo
Soma Zaidi...Faida za chumvi mwilini (madini ya chumvi)
Post hii inakwenda kukipa faida za madini ya chumvi mwilini.
Soma Zaidi...Vyakula vya kuongeza maziwa kwa mama anayenyonyesha
Post hii itakwenda kukufundisha vyakula ambavyo ni vizuri kwa mwanamke anayenyonyesha ili kumsaidia kupata maziwa kwa wingi.
Soma Zaidi...Vyakula salama na vilivyo hatari kwa mwenye kisukari, na vipi atajikinga na kisukari
Makala hii inakwenda kukupa elimu juu ya vyakula na vinywaji vilivyo salama kwa mtu mwenye kisukari, na ni vyakula vipi ni hatari kwa mwenye kisukari. Pia utajifunza njia za kujilinda na kupata kisukari.
Soma Zaidi...