HISTORIA YA MTUME YUNUS(A.S)


Nabii Yunus(a.s) ni miongoni mwa Mitume wa Allah(s.w) waliotajwa katika Qur-an. Yunus(a.s) ametajwa katika Qur-an kwa majina matatu:

(i) “Yunus” (37:139) Na hakika Yunus alikuwa miongoni mwa Mitume.(ii) “Dhun-Nun”

Na (Mtaje) Dhun-Nun (Yunusi) alipoondoka hali amechukiwa, na akadhani ya kwamba hatutamdhikisha. Basi (alipozongwa) aliita katika giza (akasema): Hakuna aabudiwaye isipokuwa Wewe, Mtakatifu “Hakika mimi nilikuwa miongoni mwa wenye kudhulumu (nafsi zao).” (21:87)(iii) “Sahibul-Hut” (Mmezwa na Chewa)

Basi subiri kwa hukumu ya Mola wako, wala usiwe kama mmezwa na Chewa (Yunusi). (Kumbuka) alipolingana, (alipomwita Mwenyezi Mungu), na hali ya kuwa amezongwa (barabara).(68:48)Majina ya “Dhun-Nun” na “Sahibul-Hut” yana maana ya “Mwenye kumezwa na samaki (chewa).” Nabii Yunus (a.s) ameitwa majina hayo mawili kutokana na historia ya maisha yake ya Da’awah iliyompelekea mpaka akamezwa na samaki mkubwa (chewa) kisha akatapikwa ufukoni akiwa hai kwa uwezo wa Allah(s.w).