Makafiri wa Kiquraish walikuwa na tabia ya kumghasi Mtume(s.
Makafiri wa Kiquraish walikuwa na tabia ya kumghasi Mtume(s.a.w) kwa kumuuliza maswali mara kwa mara. Lengo lao likiwa kumshusha hadhi Mtume(s.a.w) endapo atashindwa kujibu maswali hayo. Mchezo huu walikuwa wakiufanya kwa kushirikiana na Mayahudi. Walikuwa wakijifunza kutoka kwa Mayahudi baadhi ya mambo ya kale kisha hurejea kumuuliza Mtume(s.a.w) maswali. Miongoni mwa maswali waliyomuuliza Mtume(s.a.w) ni juu ya vijana wa Pangoni na habari za Dhulqarnain.
Vitabu vingi vya historia vinabainisha kuwa kisa cha vijana wa pangoni kilitokea katika mji wa Ephesus uliokuwa ndani ya Ufalme wa Urumi. Mji huu ulijulikana sana kutokana na kushamiri sana dini ya ushirikina. Watu wa huo mji waliabudia masanamu, mwezi, jua na sayari.
Baada ya Nabii Isa(a.s) kuja na mafundisho yake ya kumpwekesha Allah(s.w) yalienea hadi Ephesus. Wakatokea vijana wakayaamini na kuachana na ibada za kishirikina. Hili mfalme akaliona ni hatari kwa maslahi yake. Akawaita vijana hao ili kuwatisha warejee kwenye ukafiri na ushirikina. Lakini vijana hawakukubali kuiacha haki. Baada ya kuonyesha umadhubuti wao Mwenyezi Mungu aliwazidishia imani na kuzitia nguvu nyoyo zao. Qurâan inatuambia:
â...........Hakika wao walikuwa ni vijana waliomuamini Mola wao. Basi tukawazidishia uongofuâ (18:13).
Na tukazitia nguvu nyoyo zao waliposimama (mbele ya mfalme wao kafiri) wakasema: âMola wetu ni Mola wa mbingu na ardhi. Hatutamuabudu kabisa Mungu mwingine badala yake. (Hapo) bila shaka tutakuwa tumesema uovu uliopindukia kiasiâ (18:14).
Kwa msimamo wao huo mfalme alitaka kuwadhuru, basi vijana wakakimbilia pangoni. Humo walikaa miaka mia tatu (kwa hesabu ya miaka ya jua) au miaka 309 kwa hesabu ya mwendo wa mwezi.
Vijana hao walipokimbilia katika pango na wakasema: âMola wetu; tupe rehema zinazotoka kwako na tutengenezee uwongofu katika (kila) jambo letuâ. Tukaziba masikio yao (wakalala hawasikii habri yoyote) katika pango hiyo kwa idadi ya miaka mingiâ (18:10 -11).
âNa walikaa katika pango yao miaka mia tatu na wakazidisha (miaka) tisaâ (18:25).
Kisha tukawafufua ili tujulishe ni lipi katika makundi mawili lililohisabu sawa sawa muda waliokaaâ (18:12).
Baada ya kulala kwa miaka hiyo 309 ndipo walipozindukana. Mambo yalikuwa yamebadilika katika nchi na mateso kwa ajili ya kufuata mafundisho ya Mwenyezi Mungu yalikuwa hayapo tena. Lakini wao hawakuwa na habari. Walidhani wamelala muda mfupi tu. Hivyo walipoamka wakawa na hofu ile ile iliyowapeleka pangoni. Kuhusu hofu yao na kutokujua muda waliolala Qurâan inasema:
.................Akasema msemaji wao: âMumekaa muda gani?â Wakasema: âTumekaa siku moja au sehemu ya sikuâ (wengine) wakasema: âMola wenu anajuwa zaidi muda mliokaa. Basi mtumeni mmoja wenu pamoja na fedha yenu hii mjini na akatazame chakula chake kipi ni tahara zaidi akuleteeni katika chakula chake. Na afanye mambo haya kwa busara wala asikutajeni kabisa kwa yoyote. âKwani wao wakikujueni mlipo watakupigeni mawe au watakurudisheni katika Dini yao; na hapo hamtafaulu abadanâ (18:19-20).
Historia imebainisha kuwa kipindi hicho vijana hao wanaamka toka usingizini wenyeji wa mji wa Ephesus na Roma yote, walikuwa na ubishani juu ya ukweli wa kufufuka na siku ya malipo. Basi kwa tukio hili ikawa ni fundisho na uthibitisho wa ukweli wa ahadi ya kufufuliwa.
âNa namna hivi tuliwatambulisha (kwa watu) ili wapate kujua ya kwamba ahadi ya Mwenyezi Mungu (ya kufufuliwa viumbe) ni kweli, na kwamba Kiama hakina shaka.............â (18:21).
Maelezo zaidi juu ya vijana wa pangoni rejea Qurâan (18:9-26).
Mafunzo yatokanayo na kisa cha vijana wa Pangoni
Kutokana na kisa cha vijana wa pangoni tunajifunza yafuatayo:
Suala la vijana wa pangoni kulala miaka 309 kisha wakaamka ni la muujiza kama Qurâan yenyewe inavyobainisha:
Je! Unafikiri ya kwamba (wale) watu wa pangoni na (wenye habari) zile zilizoandikwa (vitabuni) walikuwa ajabu katika ajabu zetuâ? (18:9).
Si jambo la kawaida mtu kulala kwa muda mrefu (miaka 309) hali wala hanywi na bado akawa hai. Siku 20 zaweza kuwa kiwango cha juu ambazo aweza kukaa mtu bila kula wala kunywa na bado akawa hai. Lakini tunaambiwa vijana wa pangoni walikaa siku 309. Na sio kwamba walikufa wakaoza ndio wakafufuka. Bali walikuwa wazima wakigaragara pangoni.
âNa unadhani wamacho na hali wamelala. Na tunawageuza upande wa kulia na upande wa kushoto (wanapogaragara usingizini). Na mbwa wao kanyoosha mikono yake kizingitini. Kama ungewaona hakika ungegeuka upesi kuwakimbia na hakika ungejazwa khofu juu yaoâ (18:18).
Huu ni muujiza wa kuonesha kuwepo kwa Allah na Uwezo wake. Aya tuliyoinukuu inatubainishia kuwa Allah(s.w) alijaaliya mazingira walimokuwa wamelala yakawa ni ya kutisha. Kwa hivyo
kwa muda wote wa miaka 309 hakuna aliyethubutu kufika karibu yao, hivyo kutogundila.
Imani ya kweli juu ya Allah(s.w) hujenga ujasiri wa hali ya juu. Mtu akishamkubali Allah(s.w) kuwa ndiye Muumba wake na Mwenye Mamlaka yote juu ya Uhai wake hana sababu tena ya kumuogopa na kumtetemekea mwingine. Kufanya hivyo itakuwa ni kwenda kinyume na imani yenyewe ya Kiislamu.
Mara nyingi maadui wa Uislamu wamekuwa wakitumia kisingizio cha vijana na uchache wa watu kutaka kuendesha udhalimu na ukandamizaji dhidi ya Waislamu. Wamekuwa wakisema hao ni vijana wachache. Kana kwamba jambo lolote lifanywalo na vijana ni baya. Lakini habari hizi za vijana wa pangoni zinaweka wazi kuwa vijana walikuwa na imani thabiti na Mwenyezi Mungu akawaongezea uongofu. Aidha wametajwa katika Qurâan ili iwe mfano kwetu.
Ukizingatia ukweli kwamba habari za vijana wa pangoni zilitokea zaidi ya miaka 309 kabla ya kuja Mtume(s.a.w) na kwamba sehemu ya tukio lenyewe ni mbali sana na mazingira alimokulia Mtume(s.a.w); maelezo ya Mtume ni ushahidi tosha wa utume wake. Katika mazingira alimokulia Mtume(s.a.w) hatutegemei apate taarifa sahihi za vijana wa pangoni kwingine zaidi kuliko kwa Allah(s.w). Na hili Qurâan yenyewe inalishuhudia katika aya ifuatayo:
âNi sisi tunakusimulia habari zao kwa kweli. Hakika wao wlaikuwa ni vijana waliomuamini Mola wao. Nasi tukawazidisha uwongofuâ (18:13).
Umeionaje Makala hii.. ?
(i) Suratul- âAlaq (96:1-5)âSoma kwa jina la Mola wako aliyeumba Aliyemuumba mwanaadamu kwa âalaq.
Soma Zaidi...Dola ya kiislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...