Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Nabii Sulaiman(a.s)

Kutokana na histoira ya Nabii Sulaiman (a.s) tunajifunza yafuatayo


(i) Kila muumini anapotunukiwa neema na vipaji vikubwa
zaidi kuliko wengine anatakiwa amshukuru Allah(s.w) zaidi kwa kujitahidi kufanya wema zaidi na ibada maalumu za ziada kuliko watu wengine kwani hiyo ni amana na mtihani kwake. Hili aliliona Nabii Sulaiman(a.s) pale aliposema.

“………….Haya ni kwa fadhila za Mola wangu, ili anijaribu nitashukuru au nitakuwa mwizi wa fadhila, na anayeshukuru anashukuru kwa manufaa ya nafsi yake; na anayekufuru kwa hakika Mola wangu ni mkwasi, karimu (27:40)- Mtume(s.a.w) katika kumshukuru Mola wake, alikuwa akisimama usiku mpaka miguuu yake ikawa inavimba. Maswahaba walipomrai kuwa asijitaabishe hivyo, kwani kashasamehewa madhambi yake yaliyopita naya baadaye, aliwajibu: “Ni siwe mja mwenye kushukuru? ”(ii) Waumini wana dhima ya kuulingania Uislamu mijini na vijijini,ufike katika kila kona ya nchi na ulimwnegu kwa ujumla tukianzia kwenye familia zetu.(iii) Kiongozi wa Harakati za Kiislamu katika jamii hanabudi kuwanamtandao wa waumini na wanaharakati watakao muwezesha kupata taarifa za hakika juu ya hali halisi ya Uislamu kutoka kila kona ya jamii husika.(iv) Nguvu za elimu, Imani thabit,uchumi na nguvu za kujeshi ni nyenzo muhimu sana katika kusimamisha uislamu katika jamii.(v) Hatunabudi kuzichunguza habari tunazozipata juu ya watu kabla ya kuzifanyia kazi- Nabii Suleiman hakumuamini Hud Hud moja kwa moja:-


“Akasema (Suleiman) Tutatazama kama unasema kweli au umo katika waongo. Nenda na barua yangu hii na uwafikishie, kisha uwaache, na utawatazama wanashauriana vipi” (27:27-28)(vi) Baada ya kupa uhakika juu ya jambo ovu,mara moja tuweke mikakati ya kuliondoa kwa kutumia mbinu zinazostahiki.(vii)Kutafuta ushauri kabla ya kufikia maamuzi ni katika sifa muhimu za kiongozi wa kiislamu.(viii)Pamoja na kutafuta ushauri kwa wadau wa jamii yake, kiongozi mweledi ni yule anayeangalia mbali. Malkia wa Sabaa pamoja na kushauriwa na mawaziri wake kuingia vitani, hakupendelea kwa kuzingatia matokeo. Aliona saluhu ni bora zaidi kuliko vita (27:34 - 35).(ix) Nikawaida ya viongozi wa kitwaghuut kuwahonga au kuwarubuni viongozi wa kiislamu kwa kuwakaribisha Ikulu, kuwapa mirunda ya pesa, magari,majumba, vyeo vya bandia n.k.(x) Kiongozi au mwanaharakati wa kiislamu anayefanya biashara na Allah(s.w) kwa kutarajia pepo hahongeki au hawezi kurubuniwa kwa namna yoyote ile. Wanaohongeka ni wanafiki wanaopenda maisha ya dunia zaidi kuliko ya akhera.(xi) Imekuwa ni tabia ya maadui wa kiislamu, wakiwemo wanafiki,kuwapakazia watu wema makosa mbalimbali na kuwaita majina mabaya ya kuwadhalilisha na kuwafadhehesha ili watu wasiwasikilize na kuwafuata. Hufanya hivyo ili kujenga mazingira ya kuwapoteza watu na Dini ya Allah(s.w)(xii)Uchawi ni njia ya Shetani na ni haramu kwa muislamu kujifunza na kuifanyia kazi elimu ya uchawi.

- Waislamu wanaelekezwa na Mola wao kuwa mara kwa mara wajikinge na shari za wachawi, mahasidi na shari za viumbe wake wengine wanaoonekana na wasio onekana, kwa kusoma kwa mazinagiatio Suratul-Ikhlas na Al- muwadhatain(Al-Falaq na An-Nas).