Sunan ya an-Nasai


An-Nasai ambaye jina lake kamili ni Abu 'Abdur-Rahman
Ahmad bin an-Nasai alizaliwa katika mwaka 214 A.H na kufariki
303 A.H./315 A.D. An-Nasai alikuwa mwanafunzi wa Abu Dawud na Hadith za kitabu chake kinachojulikana kwa jina la "Sunnan" amezipanga katika muundo alioutumia mwalimu wake.


Kazi ya an- Nasai katika ukusanyaji Hadith imekuwa ni kazi muhimu sana kwa Uma wa Kiislamu lakini kwa kuwa hakuwa mwangalifu sana katika uchujaji wa Hadith sahihi, kazi yake imeangukia katika kundi la Hadith za daraja la pili. Baadhi ya Hadith za kitabu hiki ni dhaifu na zenye kutiliwa mashaka zilizo simuliwa na watu wanaotiliwa mashaka.