Menu



Mapambano ya waislamu dhidi ya Makabila ya kiarabu wakati wa Mtume

Mapambano ya waislamu dhidi ya Makabila ya kiarabu wakati wa Mtume

Mapambano ya waislamu dhidi ya Makabila ya kiarabu wakati wa Mtume

Makabila Mengine ya Kiarabu


Makabila mengi ya Kiarabu yaliyoleta chokochoko dhidi ya Dola ya Kiislamu ya Madinah, Mtume(s.a.w) aliyashughulikia mpaka yakasalimu amri na kulipa jizya. Ukiacha Maquraish makabila ya Kiarabu yaliyokuwa na nguvu sana na kujiamini ni makabila ya Khawaizin na Thaqif yaliyokuwa yakiishi katika maeneo ya mji wa Taif. Makabila haya yalipambana na jeshi la Mtume(s.a.w) katika vita vya Hunain vilivyopiganiwa mwaka wa 8 A.H. mwezi mmoja baada ya Fat-h-Makka. Waislamu walipata ushindi mkubwa sana katika vita hivi vilivyokuwa mwisho wa mapambano na makabila ya Kiarabu kwani yote yalikuja silimu na kuwa chini ya Dola ya Kiislamu. Vita vya Hunain vinaelezwa katika Qur-an:




Bila shaka Mwenyezi Mungu amekunusuruni katika mapigano mengi, na siku ya Hunayni (pia); ambapo wingi wenu ulikupandisheni kichwa, lakini haukukufaeni chochote, na ardhi ikawa dhiki juu yenu; ingawa ilikuwa yenye wasaa, kisha mkageuka mkarudi nyuma (mnakimbia). Kisha Mwenyezi Mungu akateremsha utulivu wake juu ya Mtume wake na juu ya walioamini. Na akateremsha majeshi (ya Malaika) ambayo hamkuyaona, na akawaadhibu wale waliokufuru; na hayo ndiyo malipo ya makafiri. (9:25-26)



Aya hizi zinatupa picha halisi ya tukio la Hunain. Baadhi ya Waislamu mwanzo mwa vita walitelezeshwa na sheitani wakawa na fikra mbaya kuwa watashinda kutokana na ukubwa wa jeshi lao lililokuwa na askari 12,000 waliojizatiti vizuri, wakasahau kuwa ushindi wote unatoka kwa Allah(s.w). Mazingira ya vita yaliwadhihirishia kuwa wingi wao haukuwasaidia chochote. Mwanzoni wengi wa Waislamu walisambaratishwa na maadui na kumuacha Mtume(s.a.w) na waumini wachache kwenye uwanja wa mapambano wakiwa wamezungukwa na jeshi kubwa la maadui.



Mtume(s.a.w) na waumini wachache aliokuwa nao walipigana kwa ujasiri wakiwa na yakini kuwa Allah(s.w) yuko pamoja nao. Waislamu waliokimbia walipokumbushwa kuwa wamemuacha Mtume wa Allah na waumini wachache kwenye uwanja wa vita, walitanabahi na kujitupa tena kwenye uwanja wa vita bila ya woga wowote kwa kutegemea radhi za Allah(s.w) peke yake. Walipofanya hivyo, Allah(s.w) aliwasaidia kwa kuwashushia jeshi la Malaika na wakapata ushindi mkubwa kwa namna ya ajabu kabisa.





                   

Download app yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiw ana App yetu. Bofya liln hapo chini kuweza ku download

Download Now Bongoclass

           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu image Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Sira Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Views 1074


Sponsored links
👉1 Simulizi za Hadithi Audio     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉4 Kitabu cha Afya     👉5 Madrasa kiganjani     👉6 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Historia ya vita vya Muta
hii ni historia ya vita vya Muta. Katika makala hii utajifunza sababu ya vita hivi na yaliyojiri katika uwanja wa vita. Soma Zaidi...

Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Nabii Ismail(a.s)
Kutokana na Historia ya Nabii Ismail(a. Soma Zaidi...

Sifa za waumini zilizotajwa katika Surat Ar-Raad (13:19-26)
Soma Zaidi...

Tukio la kupasuliwa kifua Mtume Muhammad S.A.W
Sura na historia ya Mtume Muhammad S.A.W, sehemu ya 7 Soma Zaidi...

Vitimbi vya Makafiri Dhidi ya Nabii Salih(a.s) na Waumini na kuangamizwa kwao
Makafiri wa Kithamud hawakuishia tu kwenye kuukataa ujumbe wa Nabii Salih(a. Soma Zaidi...

HISTORIA YA BANI ISRAIL
Nabii Musa na Harun walikuwa na kazi kubwa mbili; kwanza, kuwakomboa Bani Israil kutokana na dhuluma waliyokuwa wakifanyiwa na Firaun na Serikali yake, na pili, kuwarudisha kwenye nchi yao takatifu ya Palestina. Soma Zaidi...

Mafunzo yatokanayo na Historia ya Nabii Yunus(a.s)
(i) Allah(s. Soma Zaidi...

KUCHIMBWA UPYA KWA KISIMA CHA ZAMZAMA NA KUNYWA MAJI YA ZAMZAMA KISIMA KILICHO BARIKIWA
KUCHIMBWA UPYA KISIMA CHA ZAMZAMKwa kifupi ni kuwa Abdul-Muttalib alipata agizo kutoka ndotoni kuwa achimbe kisima cha zamzam, na akaelekezwa sehemu ya kupachimba. Soma Zaidi...

Mbinu za Mtume Salih(a.s) Katika Kulingania Uislamu
Kama Mitume waliotangulia, Nabii Salih(a. Soma Zaidi...

KAZI ALIZOFANYA MTUME MUHAMMAD (S.A.W) KABLA YA UTUME
KAZI ALIZOKUWA AKIFANYA MUHAMMAD (S. Soma Zaidi...