image

Vita vya wenyewe kwa wenyewe baada ya kif cha khalifa Uthman

Vita vya wenyewe kwa wenyewe baada ya kif cha khalifa Uthman

Vita vya Wenyewe kwa WenyeweKipindi cha Ukhalifa wa Ali hakikuwa na wapinzani kutoka nje ya Dola ya Kiislamu. Na inaweza kusemwa kuwa hakukuwa na upinzani kwa sababu hapakuwa na kiongozi aliyechaguliwa kwa utaratibu unaokubalika na kwa sababu hii inakuwa vigumu kusema kulikuwa na upinzani ila kulikuwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe. Ni vigumu kusema kuwa Ali alikuwa ameteuliwa kwa utaratibu wa Uislamu kuwa Khalifa. Wahaini wale baada ya kumuua Khalifa Uthman, mji wa Madinah na Serikali yake ilikuwa chini yao kwa muda wa siku sita na swala ya Ijumaa waliendesha wao.


Siku ya sita Ali alitangazwa kuwa Khalifa na wauwaji. Wauwaji hawa hawa ndio waliofundisha kuwa Ali ni “wasi” wa Mtume. Aisha, Talha na Zubeir ni vigumu kusema kuwa waliupinga Uislamu walipopigana na Ali katika vita vya Ngamia. Vile vile ni vigumu na haiwezekani Muawiya alipokataa kumtii Ali alikuwa amekosea hivyo alipinga Uislamu alipopigana na Ali katika vita vya Siffin. Tunachoweza kusema wakati wa Ali kulikuwa vita vya wenyewe kwa wenyewe. Katika vita hivyo, nani alipigania Uislamu, nani alipigania kundi lake, au ukoo wake au udugu au kabila lake n.k. ni maoni ya kila mwana historia baada ya kujua mkondo wa matukio ya kihistoria.


Jambo la kusikitisha ni kuwa kipindi cha Khalifa Ali kilitawaliwa na mapigano baina ya wenyewe kwa wenyewe. Baina ya Khalifa na Aisha, Talha na Zubair, Khalifa na Khawarij na Khalifa na Muawiya Gavana wa Syria. Matukio yalichukua mkondo ufuatao.


Baada ya kuuawa kwa Khalifa Uthman na kutawazwa kwa Ali baadhi ya jamaa wa Khalifa walikwenda Makka kueleza tukio lilivyokuwa, mama wa waumini Bi Aisha alistushwa sana na tukio hili, lakini lililotisha zaidi ni hatua ya Khalifa ya kuahirisha adhabu ya waliyomuua Khalifa Uthman kwa hoja kuwa kwanza arudishe amani nchini kisha ndipo awaadhibu wauwaji. Hoja hii ilikuwa ni ngumu kueleweka hasa ukizingatia mambo matatu.


Kwanza muanzilishi wa ghasia na hatimaye kufikia kifo cha Khalifa Uthman alifundisha imani ya “wasi” wa Ali. Pili hilo ndilo lililomuweka Ali madarakani na tatu, wauwaji hawa pamoja na kuambiwa waondoke Madina siku ya tatu ya Ukhalifa wa Ali kundi la Ibn Sabaa lilikhalifu amri ya Khalifa na kuendelea kubaki Madina kwa kisingizio cha urafiki. Mama wa waumini ambaye alikuwa anarudi Madinah kutoka kwenye Hija, alirudi Makka na kuwaomba watu kwenda kulipiza kifo cha Khalifa. Maswahaba maarufu Talha na Zubeir walimuunga mkono na wakawa naye. Wapiganaji 2,000 walipatikana. Lakini walipokuwa wanakwenda Madinah wakapata wazo la kupitia Basra kupata watu wengi. Walipokuwa njiani kuelekea Basra watu wengi wakaungana naye na alipofika Basra alikuwa na watu 3,000 chini ya Bendera yake.


Gavana wa Basra, Uthman bin Hunif alituma watu ili kujua lengo la ziara ya Bibi Aisha Basra. Wajumbe wa Gavana walifahamishwa kuwa yeye mama Aisha na Waislamu wengine walitaka kuwakumbusha Waislamu juu ya wajibu wao kwa Khalifa aliyeuawa. Na dhima yao ni kuwaadhibu wauwaji. Kusikia hivi Gavana alizuia msafara usiingie Basra. Kwa hiyo akaita mkutano na kuwaamuru watu wake wawapige Mama Aisha na wenzake baada ya kupata maelekezo kutoka kwa Khalifa Ali. Watu wake waligawanyika, kuna waliomuunga mkono yeye na wapo waliomuunga mkono Aisha. Mama Aisha alitoa Hotuba ambayo iliwezesha kuwateka nusu ya watu ambao mwanzoni walimuunga mkono Khalifa. Kuona hivi mama Aisha alitaka suluhu, lakini upande wa gavana kulikuwa na watu wa Ibn Sabaa ambao suluhu hawakuitaka - Hakim bin Hublan akiwa kiranja wa kundi hili lisilotaka suluhu alivamia jeshi la Mama Aisha(r.a) hata kabla ya ruhusa ya gavana wake na uchokozi huu vita vikaanza, gavana akatekwa, Hublan na wenzake wengi wapatao 600 wakauawa na Basra ikatekwa na kuwa chini ya Bibi Aisha, Talha na Zubeir.
                   
           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 223


Download our Apps
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Tamko la suluhu baada ya vita vya Siffin
Soma Zaidi...

MTUME MUHAMMAD (S.A.W) AANALELEWA NA BABU YAKE MZEE ABDUL-ALMUTALIB AKIWA NA UMRI WA MIAKA SITA (6)
KULELEWA NA BABU YAKE:Mzee ‘Abdul Al-Muttalib alimchukuwa mjukuu wake na wakarejea Makkah na aliendelea kuishinae na kumlea kwa mapenzi makubwa sana. Soma Zaidi...

Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Nabii Shu’ayb(a.s).
Kutokana na kisa cha Nabii Shu’ayb(a. Soma Zaidi...

Uteuzi wa Uthman bin Al-'Afan khalifa wa Tatu baada ya Mtume
Soma Zaidi...

Mawazo Tofauti Kuhusiana na Uchaguzi wa Abubakar
Soma Zaidi...

Allah(s.w) Amnusuru Ibrahim (a.s) na Hila za Makafiri
Pamoja na kudhihirikiwa na ukweli wa udhaifu wa miungu wa kisanamu, watu wa NabiiIbrahiim(a. Soma Zaidi...

Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Nabii Daud(a.s)
Kutokana historia ya Nabii Daud (a. Soma Zaidi...

Harun(a.s), Achaguliwa Kuwa Msaidizi Musa(a.s) na kumkabili (kumlingania) firauni
Nabii Musa(a. Soma Zaidi...

HISTORIA YA NABII SHU’AYB(A.S)
Nabii Shu’ayb(a. Soma Zaidi...

HISTORIA NA MAISHA YA MTUME IDRISA (A.S)
Mtume aliyemfuatia Nabii Adam(a. Soma Zaidi...

Mafunzo yatokanayo na upinzani wa maquraish dhidi ya uislamu
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

KIKAO CHA KUMFUKUZA MTUME MUHAMMAD KUTOKA MAKKAH (MAKA), KIKAO ALICHOHUDHURIA IBLISI
KIKAO CHAKALIWA KUJADILI HATMA YA MUHAMMAD KATIKA MJI WA MAKAHiki ni kikao kizito hakijapata kutokea toka muhammad katika ji wa maka. Soma Zaidi...