image

Kifo cha Khalia Uthman kilivyotokea

Kifo cha Khalia Uthman kilivyotokea

Khalifa Uthman Kufa Shahidi



Ni dhahiri wahaini wa Serikali waliona wakati umefika wa kufanya lile walilokusudia tangu pale walipoweza kumtoa Gavana wa Kufa na kumuweka wanayemtaka bila kuadhibiwa. Wakaibua mbinu ya kutuma watu watatu kwenda Madinah kuwasilisha malalamiko yao. Watatu hao walitoka Misri, Basra na Kufa. Walipofika Madinah baadhi ya maswahaba walimshauri Khalifa kuwa wauwawe lakini kwa msimamo ule ule wa kutotaka kumwaga damu ya Waislamu, Khalifa alikataa na kusema nitawasikiza. Khalifa aliwasikiliza kisha akatoa hutuba ndefu ambayo ndani yake alijibu shutuma zote. Baadhi ya sehemu ya hutuba hiyo ya kihistoria ni kama ifuatavyo:


Ninalaumiwa kwa kuwapenda ndugu zangu. Sio dhambi kwa mtu kumpenda ndugu yake. lakini sijamfanyia mtu udhalimu kwa sababu ya kupenda ndugu. Sijatumia chochote kwa ajili ya ndugu zangu kutoka kwenye mfuko wa Serikali...


Imesemwa kuwa nimewateua vijana wadogo maafisa. nimefanya hivyo kwa kuzingatia mchango wao katika uislamu. Hakuna anayekanusha uaminifu wao na mchango wao katika Uislamu, na Waislamu. Kuteuliwa kwa Usamah na Mtume (s.a.w.) kuwa kamanda wa jeshi ni ushahidi kuwa ujana sio kipingamizi cha kupewa uafisa.


Imedaiwa nimempa gavana wa Misri ngawira yote ya Afrika kaskazini kama zawadi. Ni kweli lakini niliposikia jamii haikupendezwa na jambo hili nimezichukuwa fedha zote kutoka kwa gavana na kuziweka kwenye mfuko wa Serikali (Baitul Mal).


Inadaiwa kuwa nimetenga mbuga za malisho ya Serikali kwa ajili ya wanyama wangu. Naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu, sitafanya hivyo. Katika mbuga hizo (mashamba hayo) ni wanyama wa Serikali tu (Baitul-Mal) ndio wanaolishwa humo, wote mnafahamu kuwa nilipopewa ukhalifa nilikuwa na wanyama wengi kuliko yeyote Arabia nzima. Leo nina ngamia wawili niliowaacha ili wanisaidie wakati wa Hija. Ingekuwaje, nitenge malisho ya Serikali kwa ajili yangu wakati wanyama wenyewe sina.
Watu wananilaumu kwa kuchoma nakala za Qur’an. Qur’an tukufu ni kitabu cha Mwenyezi Mungu aliteremshiwa Mtume (s.a.w.). Maswahaba waliokiandika chini ya usimamizi wa Mtume wako hai. Nimepeleka ile nakala ya Qur’an iliyokusanywa na maswahaba.


Inasemwa kuwa nimemrudisha Hakam Madina ambaye alipelekwa uhamishoni na Mtume. ukweli ni kwamba Mtume alimhamisha Hakam kutoka Makka kwenda Taif. Baada ya kumwombea Mtume alimruhusu aishi Madina. Nimetekeleza ruhusa iliyotolewa na Mtume (s.a.w.)....”


(Mwisho wa Hotuba yake akasema). Niambieni kama kuna kitu kisichokuwa cha kweli kati ya niliyosema.....39


Ingawa Khalifa alijibu shutuma zote kwa ufasaha, ukweli na uwazi, wawakilishi wa wapinzani walirudi na kusema uongo kuwa Khalifa amepuuza madai yao.


Ndipo wakaja makundi ya watu elfu, elfu kutoka Misr, Basra na Kufa na kupiga kambi karibu na Madina. Waliotoka Basra walipiga kambi Dhikhasha, waliotoka kufa walikaa ‘Awas na waliotoka Misri walikaa Dhi-Murwah. Makundi ya wahaini hawa walishindwa kuingia Madina moja kwa moja kwa sababu walipokuwa wanakaribia Madina, Khalifa alikusanya wakazi wa Madina na kuwahutubia kuwa:


Wananikusudia mimi, karibuni hivi watakumbuka wakati wa ukhalifa wangu na kuujutia, wataona siku moja ni kama mwaka kwa sababu ya vurugu umwagaji damu na uasi utaoenea nchi nzima.40


Wananchi walichukua silaha na kuzuia uvamizi wa mji wao. Hali hii ndiyo iliyolazimisha wahaini kukaa nje ya Madina.


Wahaini hawa walikuwa na agenda moja tu, ya kumwondoa Khalifa madarakani kwa hiyari au kwa nguvu. ndiyo maana walipofika tu Madina kila kikundi kilimkabili waliyemtaka awe Khalifa kwani katika hili walitofautiana. Ibn Sabaa na Wamisri walimtaka Ali. Watu wa Kufa walimtaka Zubair na watu wa Basra walimtaka Talha. Maswahaba wote hawa walikataa na kuwaambia kuwa Mtume (s.a.w.) aliwaambia makundi ya Dhikhasha, ‘Awas na Dhi-murwah yamelaaniwa.41


Khalifa aliwatuma maswahaba maarufu akiwemo Ali kusikiliza malalamiko yao. Waliwakilisha matakwa yao pamoja na kutaka Muhammad Ibn Abubakar awe gavana wa Misri badala ya Abu Mussa. Khalifa alikubali bila kuuliza kisha akawaahidi kuwa atatekeleza maombi yao. Ali naye akasisitiza hivyo hivyo. Pamoja na kuwakubalia matakwa yao walivamia msikiti na kumuua Khalifa Uthman akiwa nasoma Qur’an.




                   






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 290


Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

HISTORIA YA NABII LUT(A.S) NA WATU WA SODOMA NA GOMORA
Mtume Lut(a. Soma Zaidi...

Kuendeshwa kwa dola ya kiislamu, Uchumi, ulinzi, haki na sheria, siasa na vikao vya shura
Uendeshaji wa Dola ya Kiislamu Madinah. Soma Zaidi...

Kuanzishwa kwa mahakama na mahakama ya Kadhi wakati wa makhalifa
Soma Zaidi...

HISTORIA NA MAISHA YA NABII ISMAIL(A.S)
Ismail(a. Soma Zaidi...

HISTORIA YA NABII IBRAHIM
Soma Zaidi...

Njama za Mayahudi Kutaka Kumuua Nabii Isa(a.s)
Njama za kutaka kumuua Nabii Isa(a. Soma Zaidi...

Kuanzishwa kwa Polisi na magereza kati uislamu wakati wa Makhalifa
Kuanzishwa kwa Polisi. Soma Zaidi...

Imam Abu Daud na Sunan Abi Daud
Soma Zaidi...

HISTORIA YA MTUME MUHAMMAD (S.A.W) KATIKA HARAKATI ZA KULINGANIA DINI
Soma Zaidi...

Si Yesu Aliyesulubiwa (yesu hakufa msalabani wala hakusulubiwa
Katika Qur,an tukufu, Mwenyezi Mungu aliye muweza na mjuzi wa mambo anathibitisha kuwa aliyesulubiwa si Nabii Isa(a. Soma Zaidi...

Darsa za Sira historia ya Mtume (s.a.w) Jaribio la 04
Soma Zaidi...

HISTORIA YA MTUME AL-YASA’A(A.S)
Mtume Alyasa’a(a. Soma Zaidi...