Je, Nabii Isa(a.s) ni Mtoto wa Mungu?


Mwenyezi Mungu si kiumbe. Yeye ndiye Muumba wa kila kitu kilicho na kisicho na uhai. Kuzaa ni sifa za viumbe vya Mwenyezi Mungu, hivyo Mungu si baba mzazi wa Yesu wala si baba wa mwanadamu yeyote. Qur,an tukufu inatuamrisha:Sema: Yeye Mwenyezi Mungu aliye mmoja (tu). Mwenyezi Mungu ndiye mwenye kuhitajiwa na viumbe. Hakuzaa wala hakuzaliwa. Na wala hafanani na yeyote(112:1-4)Ama katika Biblia, neno Baba limetumika kuonesha sifa ya ulezi wa Mwenyezi Mungu kwa viumbe wake, hivyo, Mwenyezi Mungu kuitwa Baba haimaanishi kuwa kamzaa Yesu au binadamu yeyote miongoni mwetu. Na ndiyo maana akasema:Wala msimwite mtu baba duniani, Maana Baba yenu ni mmoja aliye wa mbinguni, wala msiitwe viongozi;maana kiongozi wenu ni mmoja, naye ndiye Kristo(Mathayo 23:9-10)Na katika maandiko mengine ya Biblia, Yesu amenukuliwa akisema: Basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliye mbinguni; Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje, hapa duniani kama mbinguni (Mathayo 6:9-10)Kwa maana hii, Mwenyezi Mungu ni Baba wa watu wote, si baba wa Yesu tu. Ni Baba yetu, ila si kwamba katuzaa, bali ulezi wake wa kutujaalia riziki za kila aina na kutupatia elimu na teknolojia ya kuweza kuzitumia neema na riziki hizo. Hivyo Isa(a.s) si mwana wa Mungu wa kuzaa, bali ni kiumbe wake aliyemuumba kwa neno la ‘Kuwa’, likawa kama alivyo muumba Adamu.

Bila shaka mfano wa Isa mbele ya Mwenyezi Mungu ni kama Adamu; alimuumba kwa udongo, kisha akamwambia “Kuwa”, akawa.(3:59)