image

Siku ya Taqwiya na kusimama Arafa

5.

Siku ya Taqwiya na kusimama Arafa

5.Siku ya Tarwiyya



Mwezi 8 Dhul Hija imeitwa siku ya Tarwiyyah kwa sababu siku hii, Mahujaji wanaandaa mali kwa ajili ya safari ya siku zinazofuatia mpaka mwezi 13 Dhul-Hija. Siku ya mwezi 8 Dhul -Hija, wenye kuhiji Hija ya aina At-Tamattu, watavalia tena Ihram wakiwa hapo hapo Makka kwa nia ya Hija, na wataanza tena Talbiya na kujiunga na Mahujaji wenzi wao kwa safari ya Mina.


Mtume (s.a.w) hakufanya Tawaf kabla ya kuondoka kwenda Mina. Muda wa kwenda Mina uwe ni kabla ya swala ya Adhuhuri. Mtume (s.a.w) aliswalia Mina swala ya Adhuhuri, Asr, Magharibi na Ishaa na aliswali kwa Qasr yaani kwa kuswali kwa rakaa mbili swala zote za rakaa nne kwa nyakati zake. Hapana shughuli maalum ya kufanya hapa Mina katika siku hii, bali Haji anatakiwa azidishe kuleta Talbiyyah na hasa kila swala ya faradhi. Mahujaji watalala Mina, wataswali swala ya Al-fajir humo humo, na baada ya jua kuchomoza wataanza safari ya kuelekea uwanja wa Arafa huku wakileta Talbiyyah.



6.Siku ya Arafa (mwezi 9, Dhul-Haji)



Arafa ni bonde lililozungukwa na vilima pande tatu. Kufika katika bonde hili siku ya 9 Dhul-Hija kabla ya jua kuchwa ni kitendo cha nguzo za Hija. Hatakuwa na Hija yule ambaye hatadiriki kufika katika uwanja huu angalau muda mfupi kabla kuchwa kwa jua. Ama kwa yule aliyezuiliwa njiani au aliyekuwa na kipingamizi cha msingi, akashindwa kufika Arafa kabla ya kuchwa jua la siku ya mwezi 9 Dhul-Hija, basi Hija yake itakamilika iwapo atadiriki kufika katika uwanja wa Arafa kabla ya alfajir ya siku ya kuchinja - mwezi 10 Dhul-Hija kwa ushahidi wa Hadith ifuatayo:



Mtume (s.a.w) amesema: “Yeyote aliyediriki swala yetu hii - swala ya Al-fajir ya siku ya kuchinja - na akawa nasi mpaka tukachinja na akawa amesimama Arafa, mchana au usiku, amekamilisha Hija yake”.



Pia Mtume (s.a.w) amesema:
Hapana Hija bila ya Arafa. Yule atakaye kuja kwenye siku ya al-Jam (siku ya kulala Muz-dalifa), kabla ya Al-fajri ya siku ya kuchinja, atakuw a amekamilisha matendo muhimu ya Hija.


Amri ya kusimama Arafa imebainishwa katika Qur-an katika aya ifu atayo:


Kisha miminikeni kutoka mahali wamiminikapo watu wote, (napo ni Arafaat) na ombeni samahani kw a Mwenyezi Mungu, Hakika Mw enyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe na Mwingi wa kurehemu ” (2:199).



Shughuli kubwa ya kufanya katika uwanja wa Arafa ni kumkumbuka Allah (s.w) na kukumbuka siku ya kukutana naye siku ya Kiyama. Jua lilipopinduka, yaani ilipoingia Adhuhuri, Mtume (s.a.w) alitoa khutuba iliyofafanua na kuwakumbusha Waislamu mambo mbali mbali katika hukumu za Kiislamu. Khutuba hii haikuwa na kikao cha katikati kama khutuba za Ijumaa na Idd. Baada ya khutuba, Bilal (r.a) aliadhini kwa ajili ya swala. Mtume (s.a.w) aliongoza swala na akaswali Adhuhuri pamoja na Al-asr kwa rakaa mbili mbili. Baada ya rakaa mbili za Adhuhuri, Mtume (s.a.w) alitoa salamu na hapo hapo Bilal alisimama na kutoa Iqama kwa swala ya al-Asr. Baada ya swala Mtume (s.a.w) alisimama katika kitako cha mlima uitwao “Jabalur-Rahman” (Mlima wa Rehma), akiwa ameelekea Qibla aliinua mikono yake mpaka kwenye usawa wa kifua kuomba dua (mbali mbali) kwa unyenyekevu kamili mpaka kuchwa kwa jua. Akasema Mtume (s.a.w), kuwa kuomba dua ni kitendo cha msingi katika siku ya Arafa. Tunajifunza katika Hadith ifu atayo:



Amr bin Shuayb(r.a) amesimulia kutoka kwa baba yake, naye aliyepokea kutoka kwa babu yake kuwa Mtume (s.a.w) amesema: “Dua iliyo bora kuliko zote ni dua iliyoombwa siku ya Arafa, na maneno yaliyo bora zaidi niliyosema na waliyosema Mitume wengine kabla yangu ni :-
“Hapana Mola ila Allah, aliye Mmoja siye na Mshirika. Yeye ni Mfalme na Msifiwa pekee na Yeye ni Muweza juu ya kila kitu ”. (Tirm idh, Ma lik).




                   






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 278


Sponsored links
👉1 Simulizi za Hadithi Audio     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉4 Kitau cha Fiqh     👉5 Kitabu cha Afya     👉6 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

swala ya idi na nmna ya kuiswali swala ya idi
6. Soma Zaidi...

HUKUMU ZA KUSOMA QURAN, HUKUMU ZA TAJWID, HUKUMU ZA NUN SAKINA, MIM SAKINA, QLQALA NA IQLAB, TANWIN NA MADA
Soma Zaidi...

Hutuba ya ndoa wakati wa kuoa
Soma Zaidi...

NASAHA ZANGU NNE KWAKO KUHUSU QURAN, MAUTI, DUA NA MENGINE
Soma Zaidi...

fadhila za kusoma quran
Fadhila na umuhimu wa kusoma quran 1. Soma Zaidi...

mgawanyiko katika quran
MGAWANYIKO KATIKA QURAN Juzuu, Sura, Aya, Manzil, Qara Wataalamu wa elimu za Qurani katika fani za uandishi na usomaji wameigawanya Qurani katika mafungu ili kuwezesha urahisi kwa wasomaji wa qurani. Soma Zaidi...

Umuhimu wa ndoa na kuoa ama kuolwa katika jamii
Matamanio ya jimai ni katika maumbile na hayaepukiki. Soma Zaidi...

KUMUAMINI MWENYEZI MUNGU
Jifunze tawhid yaani kumpwekesha Allah subhaanah wata'aala Soma Zaidi...

Namna ya kutufu, na masharti ya mwenye kutufu
3. Soma Zaidi...

NDANI YA SHIMO LA KABURI
Download kitabu Hiki Bofya hapa NDANI YA PANGO LA MAKABURI Mmoja wapo akatowa kamba na kulifunga jeneza vizuri na kuanza kulishusha chini ya mapango kwa kamba ile. Soma Zaidi...

2.3.Kuamini Vitabu Vya Mwenyezi Mungu (s.w Quran, tawrat, Zabur na injili
2. Soma Zaidi...

Je mahari inashusha hadhi ya mwanamke?
Je, Mahari inashusha hadhi ya mwanamke? Soma Zaidi...