Surat al Baqarah ni katika sura ambazo tunapaswa tuwe tunasoma mara kwa mara. Post hii itakufundisha kuhusu fadhila za sura hii.
Surat al-baqarah
Amesema Mtume “…Mwenye kuisoma katika nyumba yake usiku hatoingia shetani nyumba hiyo kwa muda wa siku tatu, na mwenye kuisoma mchana hatoingia shetani nyumba hiyo kwa michana mitatu” (amepokea Ibn hiban, tabrany na Bayhaqiy).
Ayat al-qursiy.
Amesema Mtume “katika surat al-baqarah kuna aya iliyobora kuliko aya zote haitasomwa aya hiyo kwenye nyumba yenye shetani ila atatoka kwenye nyumba hiyo, (aya hiyo ni) ayat al-kursy) (amepokea Al-Haakim na Bayhaqiy)
Aya za mwisho za surat al-baqarah
Amesema Mtume hakika Allah ameimalizia surat al-baqarah kwa aya zilizo tukufu (zilizotoka) kwenye hazina chini ya ‘arshi basi jifundisheni aya hizo na muwafundishe wake zenu na watoto wenu. Kwani mna ndani ya aya hizo dua, qiraa na dua” (amepokea Al-Haakim kutoka kwa Abuu Dhari).
Pia Amesema mtume “aya mbili za mwisho za surat al-baqarah mwenye kuzisoma usiku zitamtosheleza” (amepokea bukhari,Muslim, Ahmad na Ibn Maajah kutoka kwa ibnmas’ud)
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
SURATUN-NASR Sura hii imeteremka wakati Mtume (s.
Soma Zaidi...(ii)Qur-an Yenyewe Inajieleza kuwa ni Ufunuo Kutoka kwa Allah (s.
Soma Zaidi...SURATUL-KAUTHAR Imeteremshwa maka, na sura hii imeshuka kwa sababu al-aAs ibn Waail.
Soma Zaidi...Hapa utajifunza kuhusu hukumu ya Idh-har katika usomaji wa Quran.
Soma Zaidi...Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa
Soma Zaidi...