image

UPENDO ULIOTAFASIRIWA KWA MICHORO

UPENDO ULIOTAFASIRIWA KWA MICHORO


UPENDO ULIOTAFASIRIWA KWA MICHOROBint mfalme akamwambia mama akae kwenye kiti kilichopo pembeni kidogo na kitanda. Kilikuwa ni kiti kikubwa, kizuri kilichotandikwa magotoro yaliyotengenezwa kwa hariri. Kiti kilikuwa na minguu minne yote imetengenezwa kwa madini ya shaba nyekundu. Viigemeo vya kiti kwa kichwani vilitengenezwa kwa dhahabu na kutengeneza umbo zuri mithili ya uwa liliochanua. Vipande vilaini vya hariri vilifunika viegemeo hivyo. Kwa upande wa pembeni viegemeo vya kiti vilitengenezwa kwa vibao vilivyo kunywa vyema ka kuwekewa virungu vilivyotengenezwa kwa lulu. Kwa uzuri wa kiti hiki mama aladini alijisemea kuwa hata kiti cha mfalme hakifikii uzuri huu. Mama aladini aliendelea kufikiri uzuri wa chumba hiki wapi aladini atamuweka mtoto huwu aendane na hadhi yake.


Mama alikaa kwenye kiti na binti mfalme akakaa wenye kitanda. Ijapokuwa ndani kulikuwa na kajikiti kengine kadogo lakini binti huyu hakutaka kukaa kwenye kiti hiko. Hapo mama akapata muda wa kuanza kumthaminsha vyema mkwe wake mtarajiwa. Hakika binti sultani alikuwa ni mzuri. Hakuwa na kichogo, kichwa kilijawa a nywele zilizo shuka mpaka katikati ya mgongo. Wakiwa kwenye mazungumzo mama Aladini aligunduwa kuwa midomo ya binti mfalme imenona vyema, kama ametoka nywa subu ya kongoro. Mama Aladini aliendelea kumthaminisha zadi na kujiridhisha kuwa anafaha zaidi. Binti mfalme hakuwa na macho makubwa ila yalikuwa ni meupe yaliyoonekana vyema, nyusi zilizojipanga na kuchora umbo la mwezi mwandamo. Weusi wa nyusi ulizidi weusi wa nywele zake.


Zilisimama vyema kope zake, na kutengeneza sura iliyoonekana na umbo la duara kama yai la mbuni. Hakuwa na chunusi wala kipele. Binti sultani aligunduwa kuwa mkwe wake anamthaminisha, hapo akatabasamu kidogo. Binti sultani alikuwa anajikubali kuwa na yeye ni katika warembo, ukweli ni kuwa hakujuwa tu ila yeye ni namba moja. Tabasamu la binti mfalme lilimfanya mama aladini afurahi zaidi. Ukimmya ulitawala kwa kuda kidogo kisha binti mfalme akavuja ukimya na kumwambia mama Aladini “karibu sana mam, kuwa huru, nimekuwa nikiisubiri sana siku kama hii” mama aladini aliridhishwa zaidi na sauti ya mkwe wake. Hakuwa na mikwaruzo, wala ukakasi, ilitoka vyema na kutengeneza mawimbi mazuuri ya sauti yanayoweza kupennya kwene masikio na kuingia ndani yana ya sikio la ndani na kutengeneza maana ya kilichozungumzwa. “ahsante sana mwanangu, yaani nimefurahi sana, kukuona ukarimu wako, ila uzuri wa chumba hiki umenistaajabisha sana” ni maneno ya mama Aladini kuonyesha mshangao wake.


“ahasante sana mama, chumba hiki nilikipamba hivi huku nikiwa ninamkumbuka mwanao, kwani tulianza kukutana bwawani akiwa amevaa nguo iliy na rangi ya kijivu. Nilivutiwa na nguo yake lakini ndege wa ajabu alitoea mwenye rangi za kupendeza, ndege huyu alinituwa kichwani na kuelekea juu ya mti alipokuwa mwanao, niliamini kuwa ndege huyu hakuwa ni wa kawaida, ni ndege aliyetumwa kutuunganisha. Toka siku hiyo niliamini kuwa mume wangu si mwingine ila ni kijana yule. Sikuwa nimetambuwa jina lake wala wapi anaishi. Ila kwa uwezo wa mungu nikatambuwa baada ya yale yaliyotokea kati ya mimi na mtoto wa waziri. “


Binti mfalme akaendelea kusema “toka siku ile niliyokutana na mwanao nilianza kukibadili chumba hiki, na kukiweka katika hadthi inayofanana na thamani ya mwanao kwenye moyo wangu. Hata hivyo nahisi hata robo yake sikiweza kuifikia, ndipo nikaamuwa kutengeneza mdori kwa wenye sura ya mwanao nipate kumuona kila siku, kila saa kila wakati. Nilidiriki kutuma mashishushu waje kumchora mwanao bila yeye kugundua. Kama unavyoona mapazia, kitanda na kila unachokiona ni ishara ya upendo wangu kwa Aladini.” binti mfalme alizungumza maeno haya mpaka machozi yakaanza kumtoka. hakika nguvu ya mapenzi haina mfano, mama aladini alikuwa akizidi kushangaa kwa kila anachokion, sikia na shuhudia hapa ndani.


Bunti mfalme akaendelea kusema “baadaye nikagunduwa kuwa waziri ana njama ya kuniozesha mtoto wake, nililia sana ila machozi yangu hayakuweza kubadili maamuzi ya baba. Nikaamuwa kukipamba chumba hiki na kuweka picha ya ndege yule aliyetukutanisha ili iwe kumbukumbu ya moyo wangu. Amini ninachokwambia kuwa chumba hiki sikupata kumuingiza mtu yeyote ila ni wewe tu. Na huwa nikilala pindi ninapomkumbuka Aladini. Hata baba yangu hatambui uwepo wa chumba hiki katika ikulu hii” mama Aladini alithibitisha uwepo wa nguzu za giza la mapenzi kwa mtoto huyu. “sikui Aladini amemroga binti wa watu” ni aneno aliyojisemea mama Aladini huku akimkumbatia mkwewe na kumfuta machozi.


Wawili hawa waliendelea kuzungumza hata ukafika muda wa kuondoka. Mama Aladini aliondoka kwenye chumba na kurudi kwa mfalme ili kupata maelekezo nini kitafuata. Mfalme akamueleza kuwa mwambie mwanao ajinadae ijumaa ya wiki ijayo ndi harusi yao. Mama Aladini aliondoka kwa furaha, lakini kwa upande wa waziri hakukuwa hata na tone la furaha, ila majuto, hasira na ukatili ndio vilitawala zaidi. Mama Aladini lifika kwa mwanaye kipenzi na kumpatia habari za furaha. Aladini alifurahi sana. Pia mama Alimueleza kila alichokiona na kugundua yaliyokuwemo kwenye moyo wa binti mfalme. Aladini laifurahi zaidi. Aladini alimuahidi mama yake nitajenga ikulu nzui kuliko ikulu zote duniani, chumba kizuri kuliko nyumba vyote duniani.
Mama aladini alimuangalia mwanaye kwa macho ya ukali na mshangao. Aladini hujatembea popote, hiko chumba kizuri utakijuaje, ukweli ni kuwa Aladini alikusudia baadhi ya aliyoyaona kule kwenye pango yawepo kwenye ikulu yake na mengineyo. Hivyo mambp yakawa kama hivyo na Aladini akaanza kujenga ikulu lake kwa ajili ya mrembo binti mfalme.
           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 174


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Ujumbe wa Siri kwenye kitabu cha ajabu
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

UPENDO ULIOTAFASIRIWA KWA MICHORO
Soma Zaidi...

Hadithi ya aliyekatwa vidole gumba
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

Hatma ya kijana mchonganishi
Soma Zaidi...

NANI MUUAJI?
Download kitabu Hiki Bofya hapa NANI MUUWAJI? Soma Zaidi...

JARIBU LA PILI LA ALADINI
Soma Zaidi...

FAMILIA MPYA BAADA YA HARUSI
Soma Zaidi...

Mshenga wa aladini mbele ya mfalme kwa mara ya pili
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

SIRI
Hii ni game ya maandishi bila ya kutumia vioneshi (graphics). Soma Zaidi...

NJE YA JUMBA LA KIFAHARI JUMBA LA ALADINI
Soma Zaidi...

Siri ya wageni wale
SIRI YA WAGENI WALE INAFICHUKA Tambua ewe kijana changu, mimi na baba yako tulikutana zamani sana. Soma Zaidi...

KIFO CHA MTOA BURUDANI WA MFALME
Hapo zamani katika mi wa Baghadani wakati wa utawala wa Sultani Harun Rashid alikuwepo kijana mmoja aliyekuwa karibu sana na Sultani kwa kuwa alikuwa akimpa burudani. Soma Zaidi...