Navigation Menu



image

HARUSI YA ALADINI NA BINTI SULTANI

HARUSI YA ALADINI NA BINTI SULTANI


HARUSI YA ALADINI NA BINTI SULTANI



Basi mambo yakawa kama hivyo kila mmoja alikuwa akiiwaza siku ya harusi, huku mfalme akiwaza nikitu gani kingine cha kushangaza atakileta Aladini. Mama aladini aliendelea kuwaza ni uzuri gani wa nyumba atakayojenga Aladini. Binti mfalme ndio hakuweza kulala kabisa kwa furaha aliyo nayo. Alitamani a,ualike Aladini kuja kufurahi lakini isingekuwa ni maadini mema kwa mujibu wa dini. Binti hakuwa na mawazo mengi juu ya maendeleo alichowaza ni afanye nini ili Aladini aweze kumpenda zaidi. Waziri akiwa na msimamo tofauti wa wengine yeye aliwaza mbinu ya kuweza kusitisha harusi. Loo! Aladini alielekea kwenye pango ili aweze kuona kama kuna chochote ataweza kufikiri.


Aladini hakuwa na nguvu za kuingia kwenye Pango na wala pia hakutaka kugundua zaidi kama pete aliyonayo inamuingiza ndani. Alichofanya yeye ni kukaa pale nje ya lile pango huku akiwaza mambo mablimbali. Katika mawazo Aladini aliona kama mbele yake kuna uwanja mji mzima upo mbele yake. Maeneo yote ya mjini yalikuwa mbele yake na aliweza kuyatambuwa kwa majina. Katika maono hayo Aladini alianza kuangalia maeneo mazur ya kuweka nyumba yake. Hatimaye maeneo matatu yalikuwa ni machaguzi. Katika maono hayo pia Aladini akaona ikulu mbalimbali zimewekwa mbele yake, naye akaanza kuangalia moja baada ya nyingine.


Aladini akiwa katika hali hiyo aliona vitanda, mabostani na thamani za ndani mbalimbali mbele yake. Aladini akaanza kuchaguwa bostani zuri, na thamani anazoona zinafaha zaidi kuwa kwake. Aladini pia akiwa katika hali hiyoa liona aina mbalimbali za mavazi na akaanza kuchaguwa mavazi kwa ajili yake, mkewe, mfalme na mama yake. Aladini aliendelea kuona vitu baada ya vitu hatimaye akasituka, kumbe alikuwa katika mawazo makubwa sana. Mawazo ambayo yalimjengea taswira ya vitu alivyovijitaji. Aladini aliamini huenda hayakuwa ni mawazo ama ndoto ila ni maono. Baada ya muda Aladini akaondoka na kuelekea nyumbani.


Ilipofika usiku Aladini akamuita jini wa mshumaa na kumueleza atekeleze kila ambacho alichaguwa kwenye maono yale aliyoona aiwa kule mapangoni. Ila akampa sharti ya kuwa asigunduwe mtu yeyote mjini, yaani afanye siri. Jini liliahidi kutekeleza ndani ya masiku matatu. Basi siku zikazidi kuendelea kwenda kwa upole sana kwa upande wa Aladini na binti mfalme. Mama Aladini aliona siku zinakwenda kwa kasi sana. Hatimaye siku tatu za jini kukamilisha mipango zikawadia. Aladini akaenda kuhakikisha kila kitu na akajiridhisha kwa ubora wa hali yajuu. Aladini akaagiza dirisha moja la nyumba liboolewe na libakie kama halukukamilikaa wakati wa ujenzzi.
Hatimaye alhamisi ikawadia Aladini akamuagiza jini wa mshumaa amletee baadhi ya mavazi na akamuagiza vitu vingine. Loo! Iku ya ujumaa ikaungia na muda wa harusi ukawadia. Aladini kavaa mavazi ya harusi na kuongozana na mama yke pamoja na kundi la vijana wa mtaani. Aladini akiwa amepanda farasi wa rangi nyeupe. Viatu vya farasi vilikuwa vya dhahabu vilivyowekwa malalio ya hariri laini. Kiti cha farasi kilikuwa na godoro laini la hariri, na kuwekwa vishikizo vilivyoonekana kupendeza sana kwa rangi. Kamba ya farasi ilikuwa imesokotwa vyema na kuchovywa kwenye mafuta ya miski nyekundu. Kamba ilinukia na kupendeza.


Aladini alivaa joho lenye ukosi uliochovywa kwnye rangi ya dhahabu na kutengeneza ukosi mgumu wa kupendeza. Michirizi ya rangi ya dhahabu ilionekana kushuka mkabala na mashepele mawili ya joho. Aladini alionekana kijana mtanashati sana siku hiyo tofauti na mazoea. Viatu alivyovaa Aladini vilikuwa na sura ya ndege kwa mbele. Huwenda alitaka kumkumbusha binti mfalme kuwa bado anaikumbuka ile siku waliokutana. Kwa hakika Aladini alipendeza sana, kofia aliyoivaa utadhani ilikuwa ni kipande cha lulu kilichowekwa kichwani mwa Aladini. Hakuwa na nywele ndevu ila zilioneana zimetengenezwa vyema na kinyozi maridadi. Aladini alitembe kwa mwendo wa furaha sana na kutabasamu kama vile anaramba asali.


Ugeni ukafika kwa mfalme na vijana wa mtaani wakawekwa chumba maalumu na kusubiria mari ya kuanza kula. Aladini mbele ya mfalme alipata nafasi ya kusalimiana na mfalme akiwa kama baba mkwe, salamu ya kukumbatiana. Aliwasili sheh mkubwa aliyevaa mavazi yaliyovutia sana. Ndoa ikafungwa na vifijo, nderemo na shangwe zilienea ikulu nzima. Aladini alipelekwa kwa mkewe chumba ambacho aliingizwa mama Aladini siku ile. Hakukuwa na mabadiliko sana kutokakana na maelezo ya mama. Kwa mara ya kwanza Aladini anaukamata mkono wa binti mfalme na kuomba dua kubwa.


Vijana wa mtaani walikula vyakula vya thamani sana wakasshiba na kusaza. Mtoto wa waziri akuweza kuhudhuri harusi hio,na hata baba yeke. Mfalme aligundua na hakuwa na kinyongo. Aladini aliendelea kufurahia siku ya kwanza ya harusi. Aladini aliishi ndani ya ikulu kwa muda wa siku tatu akifurahi yeye na binti mfalme. Mama Aladini alipata nafasi ya kumuona malkia na kuongea naye sana. Urafiki kati ya mfalme na mama aladini ulianza kukuwa kwa kasi. Huwenda ni kwa sababu mfalme alikuwa na sehemu pekee kwa ajili ya mama Aladini toka mwanzo, ila Aladini aliharibu mipango.


Baada ya siku tatau kuisha mfalme alishangaa kuona mjengo mrefu sana kaskazini mwa ikulu yake. Mfalme alishangaa sana ni lini mjengo ule umejengwa na ni nanai amethubutu kujenga mjengo ule. Mgalme akwa katika mawazo hayo alishtuliwa na salamu ya Aladini akiwa na mkewake. Aladini akamjulisha Mfalme kuwa nahitaji kuzungumza naye. Katika mazungumzo hayo Aladini alitaa kuhusu mjengo uleulio mbele ya macho ya mfalme. Aladini alitaka mfalme pamoja na binti yake wafahamu zaidi kuhusu mjengo ule.







           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Aliflela2 Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 425


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Simulizi za Hadithi Audio     👉4 Madrasa kiganjani     👉5 Kitau cha Fiqh     👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    

Post zifazofanana:-

HADITHI YA KAKA WA SITA WA KINYOZI
Soma Zaidi...

Kwa nini vidole vimekatwa
HADITHI YA ALIYEKATWA VIDOLE GUMBA Mimi nilikuwa mfanyabiashara mdogo sana, katika mji wa Baghdad. Soma Zaidi...

Mtihani penzini
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

UGENI WA DHATI
Soma Zaidi...

Hatima ya kijana mchonganishi
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

ALADINI NA BINTI WA MFALME.
ALADINI NA BINTI WA MFALME. Soma Zaidi...

Hadithi ya Kaka wa nne wa kinyozi
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

Hatma ya kinyozi maishani mwangu
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

KIFO CHA AJABU
Download kitabu Hiki Bofya hapa KIFO CHA MTOA BURUDANI WA SULTAN. Soma Zaidi...

KIFO CHA MTOA BURUDANI WA MFALME
Hapo zamani katika mi wa Baghadani wakati wa utawala wa Sultani Harun Rashid alikuwepo kijana mmoja aliyekuwa karibu sana na Sultani kwa kuwa alikuwa akimpa burudani. Soma Zaidi...

Mshenga wa aladini mbele ya mfalme
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

Familia mpya baada ya harusi
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...