Viatu vya ajabu

VIATU VYA AJABU VYAONDOKA NA MKONO WANGU Aliponieleza sifa za viatu anavyotaka nikamsogelea kwa ukaribu na kumkazia macho kama nataka kumpiga vile kisha nikamuuliza “wewe ni nani, na ni nani amekutuma, vina nini hasa viatu hivi” alibakia kimya ...

Viatu vya ajabu

VIATU VYA AJABU VYAONDOKA NA MKONO WANGU
Aliponieleza sifa za viatu anavyotaka nikamsogelea kwa ukaribu na kumkazia macho kama nataka kumpiga vile kisha nikamuuliza “wewe ni nani, na ni nani amekutuma, vina nini hasa viatu hivi” alibakia kimya kwa muda kidogo kisha aksema “baba anakutafuta, anakuhitaji uende nyumbani”. nikamuahidi kuwa nitakwenda siku ya ijumaa. Basi akaniahidi kuwa atakuja na ndugu yake kesho kuja kunielekeza nyumbani kwao.



Kesho yake nikaandaa pale ndani chumba kingine kitupu. Nikaweka vyakula na vinywaji. Alipokuj tukaendelea kuburudika na wageni wangu watatu wenzie wamefunika sura zao. Mmoja kati yao alitoka nje, kisha baada ya muda akarudi. Basi kumbe alikwenda chukuwa dawa bila ya sisi kujuwa akiweka kwenye kinywaji na tukalewa, na kuja kuamka ni usiku na nilipowasha taa nikakuta pembeni yangu kuna kichwa cha yule binti wa siku zote aliyetaka viatu. Sikuweza kuwaona wenzie wawili.



Nilishituka sana kuona binti amekufia kwangu, nikafunga duka na kuchimba shimo uwani nikamfanyia maiti yake maandalizi yote na kumzika kwa siri. Usiku huohuo niliondoka na kurudi misri. Nikawa kila baada ya miezi 6 nalipa pesa ya ada ya kile chumba. Nilikaa misri kwa muda wa miaka mitatu hata nikajiridhisha kuwa huwenda mpaka sasa wakawa wamesahau kilichotokea. Nikaamuwa kurudi tena Yemeni ili nikamalize kazi yangu ya kuwatafuta wale watu. Pia kukutana na yule mzee aliyenitafutaga.



Nilifika Yemeniwakati wa usiku, nikaingia dukani kwangu na kuanza kusafisha, alama za michirizi ya damu zilikuwa zikionekana. Nilisafisha, sasa nilipokuwa naamsha viti ndipo nikaokota pete. Pete ilikuwa na picha ya kichwa cha mamba kwa juu. Picha ya kichwa cha kunguru na kambale kwa upande wa pembeni kulia na ushoto. Nikaamuwa kuiuza pete ile nipate pesa za kuanzia maisha. Nikaenda kwa sonara wa kwanza akasema hanunui pete ila maana ni ya thamani sana.



Nikaenda kwa sonara mwengine akaniambia nisubiri. Akaondoka kidogo na kwenda alikokwenda kisha akarudi. Akanieleza kuwa hawezi kununua. Kume aipotoka alikwenda kutoa taarifa kuwa pete iliyoibiwa imeonekana. Usiku askari wakanifamia na kunibambikia kesi ya wizi vinginevyo nitaje jinsi nilivyoipata pete ile. Mbele ya kadhi nilishindwa kueleza ukweli nikiamini kuwa nikieleza ukweli ndio nitauliwa. Nikamueleza niliiba kwa binti mmoja.



Baada ya hapo kadhi akanipa hukumu ya kukatwa mkono wangu. Nilishukuru kukatwa mkono ili kunusuru kichwa changu. Walinikata mkono, nilipata maumivu makali sana, damu ilitoka na nikapoteza fahamu. Nilipokuja kushituka nikajikuta nipo kwenye kitanda. Nilijiuguza pale kwa muda wa siku tatu. Siku ya nne akaja mzee mmoja mrefu mwenye sura ya heshima. Kwa kumuangalia utajuwa kuwa ni mchamungu, pia ni tajiri. Akaniambia “mwanangu, najua hii pete hukuiiba, naelewa fika hii pete haiwezi kuibiwa, hivyo basi nieleze historia yako na hadi likatokea hili la kutokea”. nikaanza kumueleza mpaka mwisho, kuanzia wageni wa baba, hata nikafika Yemeni na haliyotokea.



Nilipomaliza kusimulia yule mzee alikuwa akitokwa na machozi kisha akaema kwa hakika umesema vyema kwa hakika hukudanganya. Nilitambua historia yako hata kabla hujaitaja. Nilitaka kuthibitisha ukweli wa maneno yale, yaliyonenwa na wageni wale, yapata miaka 10 iliyopita. Mwananfu kuwa na amani hapa ulipofika ni kwenu, na jihisi upo kwa baba yako. Natambua yaliyomkuta baba yako, mwanangu na wewe. Nitakueleza kuanzia tafsiri ya waliyoyatenda wageni wale kwenu, na maswali mlioyashindwa kuyajuwa kuhusu wageni wale.


Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Aliflela2 Main: Burudani File: Download PDF Views 1022

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Simulizi za Hadithi Audio    👉2 kitabu cha Simulizi    👉3 Madrasa kiganjani    👉4 Bongolite - Game zone - Play free game    👉5 Kitabu cha Afya    👉6 Kitau cha Fiqh   

Post zinazofanana:

Jaribio la kwanza la aladini

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu

Soma Zaidi...
Alif lela ulela

Posti hii inakwenda kukusimulia hadithi za alifu lela ulela

Soma Zaidi...
Kwa nini vidole vimekatwa

HADITHI YA ALIYEKATWA VIDOLE GUMBA Mimi nilikuwa mfanyabiashara mdogo sana, katika mji wa Baghdad.

Soma Zaidi...
Upendo uliotafsiriwa kwa michoro

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu

Soma Zaidi...
Hadithi iliyosimuliwq na mlevi mbele ya sultani

Posti hii inakwenda kukusimulia hadithi iliyosimuliwa na mlevi mbele ya sultan

Soma Zaidi...