Hadithi ya Kaka wa pili wa kinyozi

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani

HADITHI YA KAKA WA PILI WA KINYOZI

Kaka yangu wa pili alikuwa ni mtu wa maneno mengi sana. Alikuwa ni masikini lakini ni mcheshi sana. Watu wengi walimpenda wazee na watoto, vijana na mabinti. Kaka alikuwa ni maarufu sana kwenye kitongoji alichokuwa akiishi. Kulikuwa na shutuma kuwa kaka anatoka na wake wa wenzie. Ijapokuwa shutuma hizi hazikuwa ni za kweli lakini zilikuwa ni hatari. Na hii ni kutokana na maneno mengi ya kaka na ucheshi wake. Pia kaka hakuwa mtu mwenye tabia njema kama mimi na hakuwa ni mwenye kufanya ibada kama mimi.

 

Siku moja alikutana na bibi mmoja akamtaka wazungumze kidogo. Huyu ni bibi ambaye alikuwa ni mtu wa mtaani. Hakuwa akionekana sana wakati wa mchana. Hakuwa akijulikana sana na watu, na hakuwa akijulikana kazi yake wa la anapoishi. Ila kaka alikuwa akifahamiana na huyu bibi kwa kuwa walikuwa wakikutana mara kadhaa. Kwa kuwa kaka yangu alikuwa ni mtu wa maneno mengi aliweza kufahamiana na watu wengi. Basi katika mazungumzo bibi alimwambia kaka kuwa kuna itajiri atampatia maana amemuona ni mtu mcheshi na watu.

 

Bibi aliongeza kuwa amemchaguwa kaka kwa kuwa anaamini atakapokuwa tajiri ataweza kunufaisha watu wengi. Kaka alikubali mazungumzo ya bibi yule. Bibi akaongeza kumwambia kaka kuwa kunaq sharti moja tua nalo ni kufanya kila nitakacho kuambia mimi tu na usiniulize swali lolote. Kwa kuwa kaka alipenda utajiri na alitaka kuwa tajiri alikubali sharti hili bua hata ya kuuliza maana yake. Baada ya mazungumzo ya bibi na kaka waliondoka kwa pamoja na kuelekea kwenye kutafuta utajiri.

 

Wakaenda mpaka katikati ya mji wakaingia kwenye jumba mija kubwa sana. Ijapokuwa kaka alikuwa ni mwenyeji wa mji lakini hakupatapo kulifahamu jumba hili kama lipo hapa. Hakupata hata kuliona siku moja. Akamfuata bibi yule nyuma hata wakaingia ndani. Wakakaribishwa na manukato mazuri sana, harufu ilioje ya manukato hayo. Kaka alianza kujihisi yupo dunia ya maajabu. Alikaribishwa na wabinti wa mirika, uzuri ulioje wa wabinti hao. Ukumbi ulikuwa na mapambo ya dhahabu na mazuri mazri. Kwenye mkeka mkubwa ilio na mapambio mazuri alikaa mwanamke mmoja mzuri sana.

 

Wale wabinti watatu waliokuja kumpokea yule bibi pamoja na kaka walikaa pamoja nao. Wabinti walikaa mbele ya dada mkubwa. Yule mwanamke mkubwa na mrembo kuliko wote alinyanyuka na kumpiga kofi kubwa sana mgongoni. Kaka alikaribia kukasirika na kutoa maneno ya ukali, yule bibi akamtuliza kaka na kumwambia usisubutu kufanya chochote hata niwambie. Na hii ni ndogo yapo mengine mengi. Baada ya kuangaliana kwa muda kidogo yule mwanamke akaagiza aletewe mvinyo wa zabibu.

 

Alikunywa kwa muda kisha akawapa pamoja na wale wabinti wanywe. Baada ya kuanza kulewa wakaanza kumpiga mabao kaka pamoja na kumrusha rusha pale ndani kwenye makochi na masofa. Kaka alikaribia kukasirika na kurusha makonde, ila kwa bahati nzuri wakatulia. Kisha yule bibi akamfata kaka na kumwambia kuwa huyu mwanamke amekupenda, na yupo tayari kukupa utajiri wake wote. Ila kuna mambo mawili yamebaki, ila tambua hutapigwa tena. Jambo la kwanza unatakiwa unyolewe ndevuzako. Kaka alikataa lakini kwa kufikiria utajiri aliamua kuachana na ndevu ili apate utajiri.

 

Wakaja wabinti wawili na kuanza kumnyoa ndevu zake zote hata akawa kama mtoto asiye na hata maoteo ya ndevu. Walipomaliza kumnyoa wakampata mafuta mazuri na kumpulizia manukato. Kaka alikuwa ananukia sana. Kisha akapelekwa mbele ya yule mdada mkubwa. Yule dada alifurahi sana na akanyanyuka akaanza kushika kichwa za kaka. Kaka alijisikia raha sana, kisha yule mwanamke akachukuwa mvinyo na kuendelea kunywa. Yule bibi akamwambia kaka kuwa muda si mrefu huyu mwanamke ataanza kulewa, hivyo akinyanyua umfatilie nyma, akikimbia mkimbize mpaka atakkapoingia kwenye chumba akilala, utajiri wako utaanzia hapo. Ila hakikisha humkimbizi mpaka umkamate. Unatakiwa umfatilie nyuma nyuma, na usiwe naye karibu.

 

Basi kama alivyo sema yule bibi, haukupita muda yule dada akaanza kulewa na wale wabinti wawili wote wakaondoka. Kisha yule mwanamke akanyanyuka ghafla na anza kukimbia. Yule bibi akamkumbusha kaka kwa kumwambia usithubutu kumkamata, na kaa naye mbali ila usimpoteze. Kaka akaanza kumfatilia, mara aingie chumba hiki mara kile mara uani mara atoe maneno yasiyo eleweka, ilimradi karaha. Kaka akiwa ana kfatilia, ilifika wakati akaanza kukimbia kwa kasi na kaka akawa anamkimbia, akasahau kuwa ameambia wake naye mbali, kaka alimkimbiza hata akakaribia kumkamata, vile ataka kumkamata tu akaingia mlango wa uwani. Kaka alipoingia naye mlago wa uwani akajikuta yupo katikati ya mji na watu wengi wana mwangalia.

 

Kaka alikuwa maenyolewa ndevu, amepakwa rangi kichwani na amenyolewa nyusi. Nguo alizovaa zilikuwa kama za kituko vile. Watu walianza kumshangaa kaka na wengine kumtupia mawe. Nyumbaaliyotoea ilikuwa ni ya kiongozi wa serikali. Basi kaka akakamatwa na kupelekwa kwa kadhi. Hukumu ikatoka kaka apigwe fimbo nyingi na ahamishwe mji. Basi baada ya viboko vikali kaka akatiwa kwenye gari la punda na kuenda kutupwa mbali na mji. Nilifatilia na kumchukuwa kaka yangu. Haya yote yalimpata kutokana na maneno yake mengi na kuwa msahaulifu wa sheria. Sasa ninakwenda kukusimulia kilichomkuta kaka yangu wa tatau.

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2021-11-08     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 967

Post zifazofanana:-

Ugonjwa wa kisonono
Posti hii inahusu zaidi ugonjwa wa kisonono, ni ugonjwa unaosababishwa na mdudu ambaye kwa kitaalamu huitwa Neisseria gonococcal. Soma Zaidi...

Faida za uyoga mwekundu
Posti hii inahusu zaidi faida kuhusu uyoga mwekundu ni uyoga unaopatikana katika sehemu mbalimbali na pia kuna waliofanikiwa kupandikiza na kuweza kuvuna ila uyoga huu una siri mbalimbali kama tutakavyoona. Soma Zaidi...

Kwanini mdomo unakuwa mchungu
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu sababu za mdomo kuwa mchungu Soma Zaidi...

Faida za chumvi mwilini (madini ya chumvi)
Post hii inakwenda kukipa faida za madini ya chumvi mwilini. Soma Zaidi...

Mtazamo wa uislamu juu ya dini
Kwenye kipengele hichi tutajifunza mitazamo ya kikafiri juu ya dini. Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula magimbi/ taro roots
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula magimbi Soma Zaidi...

Fahamu kuhusu madhara ya uzito mkubwa
Posti hii inahusu zaidi madhara ambayo yanaweza kutokea kwa mtu mwenye uzito mkubwa,kwa kawaida ili mtu aweze kuwa na uzito wa kawaida ni vizuri na kiafya kupima urefu ukilinganisha na uzito wa mtu. Soma Zaidi...

TUNAKUTAKIENI RANADHANI MUBARAKA
Wikibongo inawatakia waislamu wote heri ya mfungo wa ramadhaji Soma Zaidi...

Je ?kipimo kikionyesha misitar miwili mmoja hafifu mwingine umekolea ni mimba au sio
Kipimo chamimba cha mkojo, huonyesha nestory miwili kuwa una mimba, na mmoja kuwa huna mimba. Sasa je ukitokea mmoja umekoleana mwingine hafifu? Endelea na pasti ' hadi mwisho Soma Zaidi...

Funga za Sunnah na umuhimu wake
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Ishara na dalilili za Kichaa Cha mbwa
Posti hii inazungumzia kuhusiana na Kichaa cha mbwa ni virusi hatari vinavyoenezwa kwa watu kutoka kwa mate ya wanyama walioambukizwa. Virusi vya kichaa cha mbwa kawaida hupitishwa kwa kuuma. Soma Zaidi...

Dalili za minyoo na sababu zake
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za minyoo na sababu zake Soma Zaidi...