Mtihani penzini

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani

MTIHANI PENZINI

Sikuwa na wasiwasi maana niliamini kuwa nitafanikiwa tu. Siku ile nilioga na kuvaa ngua safi na kuvaa viatu vikubwa vya kuchomeka. Nikatoka kuelekea tulipoahidiana. Nilipofika pale nikakutana na kundi la vijakazi wa kike. Mmoja wao akaniuliza ndiye wewe mgeni, wasiri? Nikamjibu ndio. Hapo wakaniambia niingie kwenye moja ya boksi la mbao kisha likafungwa vyema. Niliweza kujihisi kama nipo kwenye jeneza vile. Wakafunganya na mizigo yao mingine na tukaondoak zetu.

 

Walipofika getini kwnyw jumba la mfalme mabawabu (walinzi wa geti) wakataka kuchunguza kilichomo. Wale wajakazi wakasema kuwa wamebeba nguo za mke wa mfalme. Walinzi wakawaruhusu kupita. Walipofika geti la pili, wakaulizwa tena wakazungumza vilevile. Waliporuhusiwa kupita ghafla mfalme akatokea. Akasema nataka nichunguze mwenyewe vitu vinavyokwenda kwa mkewangu. Hapo nikajua sasa ndio mwisho wangu. Hapo nikaanza kuhisi mkojo unauma. Tumbo likanza kunguruma na woga ukanijaa. Nikaanza kushahadia naa kutubu madhambi yangu.

 

Mfalme akawaambia watue mizigo, na wafungue boksi mojamoja. Kwa mkono wake mfalme akaanza kufungua kila boksi na anapojiridhisha hufunga. Ndipo akafika kwenye boksi ambalo nimo. Alipotaka kufungua mjakazi mmoja akamwambia, “mtukufu, humu kuna nguo za ndani za Malkia, si vyema zikaonekana hadharani, tunakuomba radhi ufunue boksi hili ukiwa peke yako. Basi mfalme alionekana kukubali na hapo nafsi ikatulia kiasi. Mfalme akaagiza maboksi yote yaingizwe ndani.

 

Boksi ambalo nipo nikachukuliwa na kupelekwa kwengine. Baada ya mwendo wa hatua kadha upatao dakika kama 10 boksi likatuliwa na kufungulia. Hapo nikatoka nje na kupata hewa safi. Mke wa Sultani alipiga makofi kwa kunipongeza nna kuniambia nimefaulu mtihani wa kwanza. Hapo nikapiga magoti kumsalimu na kumshukuru kwa tumaini alilonipa. Aliniangalia kwa muda kama wa dakika 2 hivi na kisha kapiga tena makofi na kusema “umefaulu mtihani wa pili” sikujuwa ni mtihani gani.

 

Akanielekeza pa kukaa huku nikisubiria chakula. Kikaletwa chakula, na vinywaji. Niliishia kunywa maji na chakula. Nilikula kiasi kidogo. Sikutaka kula saana nikiwa ugenni. Niligundua vinywaji vile vinatofautiana rang na harufu. Kwakuwa sukjuwa kwa undani vinywaji vile nikaamuwa ninywe maji tu. Baada ya chakula akaja tena mke wa sultani. Alikaa mbele yangu na kupiga tena makofi na kusema “umefaulu mtihani wa tatu” na sasa nitakuozesha mdogo wangu, il a harusi hii itakuwa ya siri, usijefanyiwa fitina na waliokataliwa posa zao.

 

Nikaelekezwa chumba cha kukaa, mke wa Mfalme akaend kuzungumza na mfalme pamoja na watu wa familia yao.wakakubaliana mahari iwe vipande 500 vya dhahabu. Mke wa mfalme alitowa mahari ili kunitolea na harusi ikafanyika. Sitaki kueleza zaidi kuhusu hiyo harusi. Mambo yakawa kama hivyo, muuza mikanda nimekuwa ndugu na Sultani wa Baghadad.

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Aliflela2 Main: Burudani File: Download PDF Views 1793

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani    👉2 Kitau cha Fiqh    👉3 Kitabu cha Afya    👉4 kitabu cha Simulizi    👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉6 Simulizi za Hadithi Audio   

Post zinazofanana:

Ujio wa wageni wa baraka

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani

Soma Zaidi...
Hadithi ya kilema, mtanashati asiye na mkono

Posti hii inakwenda kukuletea hadithi ya kilema, mtanashati asiye na mkono

Soma Zaidi...
Hadithi ya mjakazi wa Mfalme

HADITHI ILIYOSIMULIWA NA MJAKAZI WA SULTANI Mtukufu sultani, nakwenda kukusimulia tukio lililotokea leo hii wakati tulipokuwa tunaburudika.

Soma Zaidi...
Nani muuaji?

Posti hii inakwenda kukusimulia kuhusu muuaji wa mtoa burudani wa sultan

Soma Zaidi...
Deni la Penzi

DENI LA MAPENZI Badisiku ambayo niliamua niuze vitu vya ndani kwangu ili nilipe madeni ya watu, ndipo yule binti akatokea tena.

Soma Zaidi...
Muendelezo wa hadithi ya mshona nguo

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani

Soma Zaidi...
Jaribio la kwanza la aladini

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu

Soma Zaidi...