image

Kwanini vidole gumba vilikatwa

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa y

KWA NINI VIDOLE GUMBA VILIKATWA?

Baada ya harusi niliendelea kukaa pale kwa muda wa miezi mitatu hata bila ya kurudi kwangu au kuwasiliana na ndugu zangu. Siku moja mkewangu akanieleza kuwa ana ujauzito. Nilifurahi sana, nilimkumbatia kwa furaha. Habari njema zikamfikia mke wa Sltani, basi akaandaa tafrija ndogo ya pale ndani kama kusherekea furaha ya mdogo wake kuata ujauzito. Katika tafrija hiyo muda wa kula ulipofika vyakula mbalimbali vikaletwa.

 

Nikanawa mikono na kuanza kula. Mkewangu hakuwepo alitokakidogo. Nilitamani hata awepo nipate kumlisha. Nilianza kula na kunywa kisha kikala Zerbajeh, nilipogusa tu chakula kile badhi ya wajakazi walikunja sura, Mke wa Sultani akanieleza kuwa mke wako anachukia sana harufu ya chakula hiko, na ndo umeshaanz akula, hivyo itakubidi uvumilie kwa lolote litakalo tokea. Sisi katu hatuta ingilia ugomvi wenu. Basi nilijitahidi kunawa vyema kwa sabuni. Baada ya tafrija kwisha nikarudi kujipumzisha.

 

Ghafla nikaona mkewangu amebadilika sura, na kuniambia “yaani mtu kama wewe unakula zerbajeh bila hata ya kunawa”? nikamueleza mkewangu kipenzi mbona nimenawa” kama umenawa na hii harufu ninayoipata ni ya nini” “ nimejitahidi kunawa ila hii harufu haikati kwa urahisi” haya ni maneno tuliokuwa tukijibizana.

 

Looo!!! Looo!!!! huwezi amini kumbe kubishana ndipo nikawa nauchochea moto wa kifuu. “nilikuona mstaarabu, nikakupenda, na nakupenda sana kipenzi, lakini kwa hili katu siwezi kuvumilia….,” mtu mstaarabu kama wewe unakula bila kunawa jamani, hapana …!! hapana…!!! kwa hili lazima nikupe adhabu, itabidi ukatwe vidole vyako. Ulivyokulia bila ya kunawa.

 

Aliagiza wajakazi wanifunge wanipeleke kwa hakinu ili nikakatwe vidole. Wakanifunga kamba na kunifungia kwenye chumba. Nilikaa kwa siku 10 kwenye kachumba hako huku nikawa ninakula mlo mmoja tu kwa siku. Siku ya kumi akawaambia wajakazi wanitoe, akaninusa mikono yangu na kujiridhisha kuwa harufu imekoka. Hapo akaagiza dawa ziletwe na mkasi, bendeji na vitu vingine. Akawaambia wajakazi wanikamate madhubuti, na hapo akanikata vidole gumba vyangu vyote

 

“nakukata hivi vidole vilivyokuacha ukala zerbajeh bila ya kunawa. Nataka ukumbuke kuwa chakula hiki, utakapokula unawe mara 40 kwa alita, mara 40 kwa sabuni na mara 50 kwa maji. Vinginevyo nitamaliza na vingine. Nilijiwazia mambo mengi hata nikasema huwenda ni huu ujauzit ndio unamsumbuwa. Lakini ujauzto ndi anikate vidole. Baada ya hapo alilia sana na akachukuwa dawa akanipaka na kuendelea kuniuguza.

 

Niligunduwa kuwa ananipenda sana, japo sikupatapo kujuwa hasa kilichomtokea hata akachukia sana chakula hiki. Milipanga siki moja nije nimuulize. Baada ya wiki kama 3 vidonda vyangu vilipona na hapo akaja mke wa sultani na aliponikuta akapiga tema makofi na kuniambia kuwa “umefaulu mtihani wa nne” sasampohuru kuondoka. Sikuwa naelewa maneno ya mke waSultani kuhusu mitihani ile lakini pia nilifurahi.

 

Jioni mke wangua akanipatia pesa nyingi na vipande vya dhahabu na kunieleza kuwa nikanunue nyumba nzuri ya ssi kuishi. Nilifanya hivyo, nilitafuta nyumba nzuri sana nje kidogo ya mji na sasa nina watoto wawili. Nimeamua leo kuja kufurahi na watu wa mjini ndipo nikakutana na shuhuli hii.

 

Baada ya huyu bwana kusimulia habari yake, basi mjakazi wa Sultani akamwambia Sultani, Je! Hadithi hii si yenye kushangaza kuliko hadithi ya mtoa burudani? Hapo sultani akasema “ni nzuri ila bado haijashinda hadithi ya mtoa burudani” kufikia hapo tabibu akapiga magoti na kusema “mtukufu Sultani, nitasimulia hadithi ya kushangaza zaidi kuliko mazungumzo yaliyo tangulia, kama utaikubali zaidi iwe kafara la tukio la leo. Hapo tatibu akaanza kusimulia hadithi yake

           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 718


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

HADITHI YA MLEVI
Soma Zaidi...

Aladini na binti wa mfalme
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya mshumaa wa ajabu Soma Zaidi...

Hadithi ya Kaka wa pili wa kinyozi
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

Kwanini vidole gumba vilikatwa
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa y Soma Zaidi...

Jaribio la tatu la aladini
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

Wagen wa Ajabu
UJIO WA WAGENI WA BARAKA. Soma Zaidi...

Hadithi ya Kinyozi kaka wa kwanza
Soma Zaidi...

Alif lela ulela
Posti hii inakwenda kukusimulia hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

Hadithi ya kinyozi kaka wa pili
Soma Zaidi...

ALADINI NA BINTI WA MFALME.
ALADINI NA BINTI WA MFALME. Soma Zaidi...

Deni la Penzi
DENI LA MAPENZI Badisiku ambayo niliamua niuze vitu vya ndani kwangu ili nilipe madeni ya watu, ndipo yule binti akatokea tena. Soma Zaidi...

ALIF LELA U LELA KITABU CHA PILI
Download kitabu Hiki Bofya hapa KITABU CHA PILI HADITHI ZA ALIF LELA U LELA UFUPISHO WA ALIF LELA U LELA KITABU CHA KWANZA. Soma Zaidi...