Home Afya Shule ICT Burudani Dini Maktaba Maswali Madrasa Apps Blog Legacy Login

NDANI YA JUMBA LA ALADINI


image


Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu


NDANI YA JUMBA LA ALADINI

Hatimaye Aladini anaingia ndani, Loo! Alitamani kupiga kelele, huku ameziba mdomo wake kwa mshangao. Uzuri wa ndani ulikuwa mara dufu ya nje. Ukumbi kubwa ilio katika umbo la duara. Mlango mkuu wa kuingilia kwenye ukumbi ulukuwa na pazia la rangi ya kijivu. Maashindi ya kiarabu yaliyopangiliwa na kutengeneza umbo la uwa zuri lililoonekana kuchanua. Maandishi yalikuwa ya rangi za kuchanganyika huku rangi ya zambarau ikitawala vyema. “Marhaban bikum” yaani karibuni sana, yalikuwa ndio maneno yaliyoandikwa yalivyosomeka.

 

Zuria la rangi nyekundu lilitandikwa na kuenea ukumi mzima. Zuria lilikuwa na michirizi ya zambarau na kutengeneza madoa makubwa ya rangi ya buluu. Zuria lilichanganya rangi nyingine na kutengeneza mauwa majubwa yaliyo mazuri. Rangi za mauwa hayo zilifanana sana na rangi za magoya ya kanga. Yaani madoa meupe na meuzi. Madirisha makubwa yaliyongaa vyema na kuonyesha kwa ufasaha kilicho nje. Michirizi ya madirisha ilikuwa inavutia kama vile ni mikufu ya dhahabu iliyoning’inizwa kweye vipete vya madirisha.

 

Mapazia yaliyokunywa mafundo yalining’inia kwenye madirisha. Aladini aliliendea dirisha moja na kufungua pazia. Loo! Lilikuwa ni pazia zuri sana, lenye rangi ya kijivu kama lile pazia kubwa. Pazia lilikuwa na picha ya ndege yule aliyeunganisha roho mbili hizi. Alikuwa ni ndege mzuri sana kwa kumuangalia. Vipete kwa kuning’inizia pazia vilikuwa vya rangi ya ugoro iliyo wiva sana iliyochanganyika na michirizi ya rangi ya samawati na kutengeneza mabadilishano ya rangi kama pundamilia aliyenona. Pazia lilifunika diisha na kushuka kwa chini na kutengeneza sura ya kuvutia.

 

Meza kubwa iliyozungukwa na viti iliwekwa katikati ya chumba. Ibila shaka ni meza ya kulia chakula, kwani vitu vilivyoonekana kwenye meza vinasadivu yaliyomo. Masinia 6 yaliyofunikwa na makawa ya rangi ya samawati, yenye micirizi ya kahawiya kwa chini. Masinia yalingaa kama ni almazi iliyowekwa. Kabaesni kadogo kalikojaa vijiko, visahani na vitu vingine. Maji safi yalionekana kwenye jagi. Ni masafi sana kiasi cha kuonyesha kana kwamba jagi ni tupu. Aani anaonekana aliye upande wa pili kama ni kioo. Harufunzuri ilikuwa ikitokea kwnye meza kubwa.

 

Viti vikubw avyenye magodoro ya harir vilizunguka meza na kutengeneza duara lama kiota cha mayai ya kuku anayelalia. Viti vizuri vilivyokuwa vya rangi za kupendeza na kuwekwa vikuku nya lulu pembeni ya kila kimoja. Basi uzuri ulioje wa ndani ya jumba hili. Juu karabai mishumaa mikubwa ya rangi nyekundu na njano ilining’inizwa ikiwa kwenye matovu makubwa ya rangi ya zamabarau. Matovu yalionekana kuwa na vijiwe vya ranirangi vikining’inia hakuna aliyejuwa ni madini ya aina gani. Ila vijiwe hivi ifikapo usiku kuakisi mwanga kutoka kwenye mishumaa na kugeuka kama taa zinazowaka.

 

Mjakazi mkubwa aliyeandaliwa na mama Aladini akaanza kupanga kundi la wajakazi na wafanyakazi kila mmoja kwenda kwenye eneo lake la kazi. Mjakazi mwingine aliye mrefu zaidi na mzuri sana akamchukuwa Aladini na mke wake kuwapeleka kwenye chumba chao. Walikutana na mfululizo wa mapazia yasiyopungua 5 ynye rangi mbalimbali za kupendeza. Hatimaye wakakaribishwa na harufu nzuuri iliyotoka nyuma ya pazia lenye rangirangi kama uwa la waridi. Mjakazi akawakaribisha na kurudi nyuma, huku akimuashiria binti sultani sasa ni kazi kwake kuongoza njia.

 

Mjakazi akabakia pale pale, binti sultani akafungua pazia, Loo! Kitasa cha dhahabu kikawakaribisha. Aladini kwa mkono wake akafungua kitasa, mlango ukafunguka. Hatimaye wawili hawa wapo ndani, kinanukia sana chumba chao. Uzuri wa chumba na mapambo hakukuwa na tofauti sana ya kile chumba cha binti Sultani. Tofauti ni kuwa vitu vyake vilikuwa ni vya thamani sana. Hatimaye kwa uchovu wa safari wawili hawa wakaamuwa kupumzika na mlango ukafungwa.

 

Atimaye siku ikaenda hivyo na muda wa chakula ukafika, wakapata chakula kizuri. Mama Aladni aliendeela kuwa pale, ijapokuwa hakupendelea kuishi pale. Alitarajia baada ya ujio wa Sultani arudi nyumbani kwake. Mama Aladini ijapokuwa mambo yote alikuwa akiyashuhudia kwa macho yake lakini hakuwa akiamini hasa uhalisia na nini itakuwa hatima ya mambo yale. Hivyo hakutaka kulekeza maisha yake ya mwanzo kirahisi. Masi ambo yakawa hivyo na usiku ukaingia na hatimaye kukakucha.



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Madrasa kiganjani       ðŸ‘‰    2 ICT       ðŸ‘‰    3 Mafunzo ya html kwa kiswahili       ðŸ‘‰    4 Magonjwa na afya       ðŸ‘‰    5 Hadiythi za alif lela u lela       ðŸ‘‰    6 Jifunze fiqh    


Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS

Imeandikwa na Drsky Tags Burudani , simulizi , ALL , Tarehe 2021-11-08     Share On facebook or WhatsApp Topic school Zaidi Dini AFYA ICT Burudani Tags Uzazi maswali Afya mengineyo dini HIV Sira vyakula Matunda HTML php Alif Lela 1 Alif Lela 2 FANGASI Dawa SQL Tips Quran Sunnah fiqh DARSA Magonjwa Tajwid tawhid simulizi Dua Academy Wahenga chemshabongo WAJUWA Michezo ICT Imesomwa mara 993



Post Nyingine


image Hadithi ya chongo wa pili mtoto wa mfalme
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

image Hadithi iliyosimuliwa na mshona nguo
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

image WAKATI WA KUFUMBUKA SEHEMU YA 2
Post hii ni mwendelezo wa hadithi ambayo Kwa jina inaitwa wakati wa Kufumbuka, ni mwendelezo wa pale maria anawekwa mbele ya wazee Ili akili kwamba John sio mtoto wa Mzee maganga ila maria akikumbuka wazi kwamba John ni mtoto wa Mzee maganga anakataa kukiri na anaangua kilio na watoto pia wanaangua kilio na pia wanaamua kumpeleka Mari kwenye mizimu Ili iweze kuamua. Soma Zaidi...

image Mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme sehemu ya tano
Posti hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme sehemu ya tano, baada ya bibi kuachana na mke mdogo wa mfalme alienda kwa kijana wa kiume wa mfalme na kuona udhaifu wake kwamba anapenda sana mali. Soma Zaidi...

image Hadithi ya mzee wa pili na mbwa wawili weusi
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

image Ndani ya jumba la aladini
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

image WAKATI WA KUFUMBUKA SEHEMU YA 1
Post hii inahusu zaidi hadithi mpya na nzuri inayoitwa wakati wa Kufumbuka, ni hadithi inayohusu maisha ya kawaida ambapo watu ushindwa kudhamini watu wa karibu nao na kuona watu wa mbali ndio wenye maana ila shida zikifika ndipo wanaona umuhimu wao. Soma Zaidi...

image Hadithi ya tabibu wa mfalme
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

image Kifo cha mtoa burudani wa sultani
Posti hii inakwenda kukusimulia kuhusu hadithi ya kifo cha mtoa burudani wa sultan Soma Zaidi...

image Mtoto wa tajiri na mtoto wa maskini ( sehemu ya tatu)
Post hii inahusu zaidi mtoto wa tajiri na mtoto wa maskini wakipanda gari kuelekea shule kuanza maisha mapya. Soma Zaidi...