Siri ya kifo yafichuka

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi za alifu lela ulela

SIRI YA KIFO YAFICHUKA

Kijana akaanza kueleza kuwa huyu binti ni mkewangukabisa na ni mtoto wa mjpomba wangu, na huyo mjomba ni huyu mzee. Mimi na mkewangu tuliiishi vyema sana. Mkewangu alinipenda sana na miaka yote tulioishi sikuweza kumuona na tabia mbaya hata siku moja. Niliweza kuzaa nay watoto watatu. Siku moja alikuwa anaumwa, maradhi haya yali dumu kwa muda uliokaribia mwezi mmoja kisha akapata nafuu kidogo. Haikuchukuwa muda mrfu akaumwa tena baada ya siku kadhaa akapata nafuu tena.

 

Siku moja alinipa matumaini kuwa kuwa amepata nafuu sana. Sasa akaniambia kuwa ana hamu na tunda epo na hatokwnda kuoga mpaka ale tunda hilo. Kwa kuwa nilikuwa nampenda sana mke wangu. Nilikwenda kumtafutia tunda epo popote pale. Nilihangaika sana kwenye mabostani mengi ya mjini. Lakini bila mafanikio. Siku hiyo nilirudi mtupu kwa mke wangu. Loo siku hiyo mke wangu hakwenda kuoga. Basi siku ilofata nikatoka tena kwenda kutafuta tunda epo. Wakati nilipokuwa nimekata tamaa kabisa ya tunda ndipo nikakutana na mze mmoja akanileza kuwa kuna mji matunda hayo yanapatikana. Basi nikafunga safari kulekea huko.

 

Safari ilinichukuwa siku tatu hata kufika na kurudi na nilinunua matunda matatu kwa gharama ya vipande 15 vya dhahabi. Cha ajabu niliporudi mke wangu hakuwa tena na hamu ya tunda epo. Lakini alichukuwa matunda yale na kuyaweka kwenye kabati. Siku tatu zikapita bil mke wangu kugusa yale matunda. Basi siku ya nne nilipokuwa mtaani nilikutana na kijana mmoja mtanashati sana akiwa na tunda la epo. Kijana yule nikamuuliza wapi amepata ili nikanunue mengine. Kijana akanieleza kuwa “nimepewa na mpenzi wangu kama zawadi, mumewe alikwenda mbali safari ya siku tatu kununua maepo matatu kwa thamani ya vipande 15 vya dhahabu. Na mkewe ambaye nimpenzi wangu wa siri akanipatia kama zawadi.

 

Niliposikia maneno haya nilistaajabu sana na kuvurugwa moyo wangu. Nilitoka mbio hadi kwa mke wangu. Nilipoangalia kabatini nilikuta tunda moja halipo na yamebakia mawili. Nilistaajabu na kuyasadikisha maneno ya yule kijana. Nilimkamata mkewangu na kmchoma kisu cha tumbo kisha nikamchinja na kumkatakata vipande na kuvifunga kama ulivyoona kwenye boksi. Baadaye nilianza kujuta sana na kulia sana.

 

Kitu cha ajabu siku ya tatu niimkuta mwanagu analia sana. Nilikuwa na uhakika kuwa hatambui kuwa kama mama yake nimemchinja. Basi nikamuuliza mwanangu kipi kinakuliza?. akanieleza kuwa “naogopa mama akirudi atanipiga, matunda yake matatu nimechukuwa mmoja, nikaenda nalo kucheza. Mkaka mmoja akaninyang’anya na kunipiga, nikamwambia kuwa ni la mama ameletewa na baba kutoka mbali safari ya siku tatu na amenunua kwa thamani ya vipande vitatu vya dhahabu. Yule mkaka akakimbia nalo” basi hapo hapo nikamwambia mwanangu anyamaze.

 

Dah nikagundua kuwa yule kijana alikuwa ni muongona ndiye chanzo cha kifo cha mke wangu. Niliia sana sanaaaa. Baba mkwe wangu ambaye ni mjomba wangu huyu hapa akaja. Nikamueleza kila kitu naye alilia sana. Hivyo khalifa mimi ndiye niliyemuuwa huyu binti, tafadhal niadhibu mimi niweze kulipa deni la nafsi ya mke wangu. Baada ya kusikia habari hii khalifa akamueleza waziri Mansur. “Nenda ukanitafutie huyu kijana, ninakupa siku tatu tu, na endapo hutamleta nitakuchinja kama alivyochinjwa huyu binti”.



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2021-11-08     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1675


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

Mtoto wa tajiri na mtoto wa maskini ( sehemu ya nne)
Post hii inahusu zaidi watoto Hawa wawili wakiwa kwenye kituo cha mapumziko ambapo mtoto wa tajiri anabugia soda aliyopewa na yule mwalimu pia tumbo linaanza tena na anaanza kuendesha Soma Zaidi...

Hadithi ya binti wa kwanza na mbwa
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

Hadithi ya Binti mfalme
Posti hii inahusu zaidi hadithi ya Binti mfalme ni hadithi ya kusisimua, kuhusu hadithi hii ni kwamba mfalme alihitaji mtoto wa kiume ila wanawake wote hawakumpata ila alitokea mke mdogo mmoja wa mfalme akajifungua watoto wawili mapacha mmoja wa kiume na Soma Zaidi...

Kifo cha mtoa burudani wa sultani
Posti hii inakwenda kukusimulia kuhusu hadithi ya kifo cha mtoa burudani wa sultan Soma Zaidi...

Dalili za U.T.I
'UTI (urinary tract infection) no ugonjwa wa maambukizi katika mfumo wa mkojo na maambukizi haya husababishwa na bacteria, fangasi,na virus. Pia unaweza athiri rethra, kibofu Cha mkojo na figo.lakini Mara nyingi UTI huathiri Hadi mfumo wa uzazi na w Soma Zaidi...

Namna ya kuishi na vidonda vya tumbo
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu namna ya kuishi na vidonda vya tumbo Soma Zaidi...

Usuluhishaji wa walio dhurumiwa
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

Ndoa ya Sinbad na binti mfalme
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa safari saba za Sinbad Soma Zaidi...

Kujiandaa kwa ajili ya kumuona daktari
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu baadhi ya mambo ya kujiandaa kwa ajili ya kumuona daktari Soma Zaidi...

Hadithi ya aladini na taa ya mshumaa wa ajabu
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi ya aladini na taa ya mshumaa wa ajabu Soma Zaidi...

Dalili za kupata uvimbe kwenye kizazi (fibroid)
Post hii inaenda kufundisha kuhusiana na uvimbe wa kizazi kwa wanawake. Uvimbe wa kizazi no uvimbe ambao hutokea kwenye tumbo la kizazi ambao unaweza kuwa ndan ya kizazi uvimbe huu ndan ya mwanamke hujulikana kama (uterine myoma au fibroid). Uvi Soma Zaidi...

Ndoto ya mgonjwa, binti mfalme
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...