Umuhimu wa kutumia dawa za kujikinga na maambukizi ya ukimwi

Posti hii inahusu zaidi umuhimu wa kutumia dawa za kujikinga na maambukizi ya ukimwi, ni faida ambazo upatikana kwa watu wanaodhani wameambukizwa na virus vya ukimwi na kuweza kujikinga.

Faida za kutumia dawa za kujikinga na maambukizi ya ukimwi.

1. Kwanza kabisa wanaweza kujua afya zao wakoje, kwa sababu mtu akija kupewa dawa hizi ni lazima awe amepima kama ana maambukizi kama Hana anapewa dawa kwa kipindi cha mwezi mmoja au siku ishilini na nane na kama amekutwa na maambukizi anaendelea na dawa kama wateja wengine, kwa hiyo ni vizuri kwa sababu usaidia mtu kuja hali ya afya zao.

 

2. Inawasaidia wahudumu wa afya na watu wengi kuwa macho kuhusu maambukizi ya ukimwi, kwa sababu watu wanakua kuwa maambukizi yapo na wanakuwa macho kujikinga na ugonjwa huo na mara nyingi utawakuta wamevaa gloves Ili kujikinga.

 

3. Kuwasaidia wakina Mama wajawazito kutowaambukiza watoto wao kwa sababu dawa za kuzuia maambukizi utumiwa na akina Mama Ili kuzuia mtoto asipate akiwa tumboni , anapozaliwa na wakati wa kunyonya kwa hiyo ni vizuri kabisa dawa hizi zitumike, hasa kwa wahudumu wa afya walio wajawazito wanapaswa kuwa makini na kupima mara kwa mara kwa sababu ya usalama wa watoto walioko tumboni.

 

4. Kwa hiyo ni vizuri kabisa kwa wahudumu wa afya na watu wote walio kwenye hatari za kupata maambukizi ya ukimwi kupima mara kwa mara Ili kuweza kujua afya zao na kwa sababu ya mazingira yao, kwa mfano wanaofanya biashara za ngono,wanaovuta sigara kwa kutumia sindano Moja kwa watu zaidi ya mmoja na sindano hiyo utunzwa kwa matumizi ya siku nyingine, wanaume wanaojamiiana na wanaume wengine,wafungwa, watu wanaoishi kwenye kambi za wakimbizi. Wote Hawa wako kwenye hatari ya kupata ugonjwa wa ukimwi upimaji wa afya ni muhimu.



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/05/22/Sunday - 08:38:59 am     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 632


Download our Apps
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-