picha

Umuhimu wa kutumia dawa za ARV

Posti hii inahusu zaidi umuhimu wa kutumia dawa za ARV kwa wathirika wa virusi vya ukimwi .pia tutangalia kwa undani mambo ya kuzingatia kwa wathirika wanaotumia ARV .pamoja na kujali watu wanaotumia dawa hizo .

 Umuhimu wa kutumia dawa za " ARV" kwa wathirika wa VVU.

  1. Kutokana tulivyoeleza apo juu kuhusu umuhimu au matumizi kwa watu wanaotumia dawa za "ARV" .ambazo ni dawa za kupunguza makali ya virusi vya ukimwi .dawa hizi utakuwa kutumia kwa usahihi.mtu anayeishi na virusi vya ukimwi hutumia dawa hizi kwa maisha yake yote.Endapo mwathrika ataacha kutumia dawa hizo ,anaweza kupata madhara zaidi kama vile kufhoofu kiafya ,magonjwa nyemelezi na kifo  ARV haziui virusi bali hufubaza virusi na kupunguza kasi ya kuongezeka.dawa hizi ufanya kinga ya mwili kuimarika.jukumu la kumwanzishia mwathrika dawa za kupunguza makali ya VVU ni  la kitabibu mkwa hiyo,kuna umuhimu wa kupinda afya ili kukua hali halisi ya afya zetu.     
  2. Huwaondolea wathirika wa VVU mateso ya kushambuliwa na maradhi nyemelezi ..maradhi   nyemelezi ni kama .saratani ,kifua kikuu,fangasi,kuharisha na homa kali ya mapafu
  3. Huimarisha afya za wanaoishi na VVU.   Kutokana na ilo watu wenye virusi vya ukimwi afya zao huwa vizuri kama vile watu wasio na ugonjwa wa UKIMWI. Hivyo hivyo mtu anaetumia hizi dawa inabidi awe anafanya sana mazoezi ya mwili .ili kuweza kulinda seli zake ziweze kufanya kazi.
  4. Wathirika wa VVU wanaweza kuishi maisha ya kawaida na kushiriki shughuli zao za kiuchumi na kukiongizia kipato.kutokana na hilo watu wanaotumia hizi dawa wanauwezo wa kuongoza maisha yao ya kila siku 

        5. Hupunguza kasi ya kuzaliana kwa wingi kwa VVU.hata hivyo hurefusha maisha.

      .  Mambo ya kuzingatia kwa waathrika wanaotumia "ARV"

Kama tulivyoona apo mwanzo wathirika wa VVU ni kundi linaloitaji kuishi kwa kufuata taratibu zilizoainishwa na watahalamu wa afya.mambo ya kuzingatia ni kama yafuatayo.

1.waathirika ni lazima wafuate ushauri wa kitaalamu wa kitibabu au watahalamu wa afya.

2.waathrika wanapaswa kutumia ARV kwa dozi sahii na kwa muda sahii .dawa zitumike kama ilivyoelezwa na daktari au mtaalamu wa afya .hii itasaidia kuboresha afya na kupunguza uwezekano wa VVU kuwa sugu kwa dawa zinazotumika.

3.waathrika wachukue tahadhari kwa kujikinga ili wasipate maambukizi mapya na kuambukiza wengine.ili kuondoa idadi ya maambukizi katika jamii.

4.mwathirika asiache kutumia dawa kwa muda na kisha kurudia tena  dawa hizo bila ushauri wa daktari au mtaalamu wa afya.

5.waathirika wa VVU watoe taarifa kwa daktari au watoe huduma kuhusu matatizo na athari za "ARV" endapo zitajitokeza.

6.waathirika waepuke kufuata imani na mila potofu za jadi au za dini zinazozuia kuwa mfuasi mzuri wa ARV 

7.waathirika wafuate ratiba ya kwenda kiliniki ya dawa za "ARV" bila kukosa ili kupata ushauri nasaa.

8.waathrika wazingatie ushauri kanuni za afya kwa mfano ,kuzingatia usafi wa mwili,lishe bora na mazingira safi.

9.waathirika wanashauriwa kuendelea kuishi kwa matumaini na wasikate tamaa .

10.mtumiaji wa "ARV" harusiwi kishirikiana dawa zake na mtu mwingine.

      jinsi watu wanaotumia dawa za "ARV"

1. Wathirika wa VVU wanaotumia ARV wanahitaji kuthaminiwa katika jamii zao na kuwaona kama watu wengine bila kuwabuguzi na kuwatenga.ili kuwajali watu wanaotumia dawa hizo.ni muhimu sana kuwasaidia pale wanapoitaji msaada.

2.pia kuambatana nao wanapoitaji kuaindikizwa kwenda kiliniki kuchukua dawa zao.pia inabidi tuwafaliji  wajione na wenyewe kama watu wengine wanapoitaji huduma hizo.

3.tuwasaidie wanapoitaji kuelekezwa matumizi sahihi ya  " ARV" ili wasiweze kwenda kinyume badae wasije kupata athari zozote katika jamii zetu.

4.kuwapatia chakula bora na kwa wakati.pia inabidi tuwandalie chakula chenye kuwaongezea vitamin ndani ya mwili wao.ili waweze kuijenga miili ya sawa .chakula lazima kiwekwe kwenye mazingira masafi na yenye virutubisho.kifunikwe na kisiwe cha balidi sana.

5.kuwakumbusha muda sahihi wa kumeza dawa pale wanaposahau.

6.kuwahamasisha kuendelea na matumizi ya dawa.

7.kuepuka kuwanyanyapaa walioathirika na VVU.pia ni muhimu sana kuzingatia na kufuata ushauri unaotolewa na daktari au mtaalamu wa afya kwa ktumiaji hi wa ARV .

 

 

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Dawa Main: Post File: Download PDF Views 4194

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 web hosting     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Simulizi za Hadithi Audio     👉4 Dua za Mitume na Manabii     👉5 Kitau cha Fiqh     👉6 kitabu cha Simulizi    

Post zinazofanana:

dawa ya kutibu infection kwenye kizazi nisaidie doctor

Je unasumbuliwa na maambukizi na mashambulizi ya virusi na bakteria kwenye sehemu za siri ama via vya uzazi?. Posti hii inakwenda kuupa ushauri.

Soma Zaidi...
Dawa za mitishamba za kutibu meno

Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu dawa za mitishamba za kutibu meno

Soma Zaidi...
Fahamu kuhusu dawa ya pyrantel pamoate

Post hii inahusu zaidi dawa ya pyrantel pamoate ni dawa ambayo usaidia kutibu minyoo ambayo kwa kawaida ukaa kwenye utumbo mdogo.

Soma Zaidi...
Fahamau madhara ya flagyl (Metronidazole)

Flagyl ni nini? Flagyl (metronidazole) ni antibiotic. Inapigana na bakteria katika mwili wako. Flagyl hutumiwa kutibu maambukizo ya bakteria ya uke, tumbo, ngozi, viungo na njia ya upumuaji.

Soma Zaidi...
Dawa ya chango na maumivu ya hedhi

Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu dawa ya chango na maumivu ya hedhi

Soma Zaidi...
IJUE DAWA YA AMOXLINE (antibiotic) NA MATUMIZI YAKE

Posti hii inahusu zaidi dawa ya amoxline .jinsi inavyofanya kazi mwilini.pamoja na matumizi yake.

Soma Zaidi...