Pumu ni ugonjwa ambao huathiri sehemu ya kupitisha hewa kwenda kwenye mapafu ya binadamu kitaalamu huitwa bronchioles. Mtu mwenye pumu huwa na michubuko sugu mwilini kwenye mirija yake ya kupitisha hewa. Hali ambayo husababisha kuvimba kwa kuta za mirija
Kuna makundi mawili ya pumu nayo ni:; 1.pumu ya ghafla (acute). Hii huwa ya Kawaida ambapo humfanya mgonjwa aweze kustahimili 2.pumu sugu; hii hufanya njia kuwa nyembamba zaidi kutokana na kuziba kwa kuta na Hali hii ikizidi nyia huwa nyembamba zaidi.
Sababu zinazopelekea kupata ugonjwa wa pumu;
-matatizo ya kinasaba
-maendeleo ya kiuchumi
-uvutaji wa sigara na tumbaku kipind mama akiwa mjamzito kupelekea mtoto kupata pumu.
-magonjwa ya mapafu Kama bronchitis
-vyanzo vya mzio ( allergens) Kam vile vumbi, vinyesi vya wanyama na baadhi ya vyakula.
-uchafuzi wa mazingira Kama Moshi na baadhi ya harufu Kali.
-baadhi ya kemikali kwenye maeneo ya kazi hasa kwenye viwanda Kama vya rangi chuma sementi na zege
-baadhi ya wagonjwa wanaotumia dawa za shinikizo la damu
Visababishi au uwezekano wa kupata pumu;
-kuishi sehemu yenye baridi na vumbi
-msongo wa mawazo
-kuishiwa na pumzi na kupumua kwa shida
-historia ya pumu au historia ya kurithi
-Aina ya matatizo katika njia yake ya kula
Dalili za pumu
-kuishiwa na pumzi na kupumua kwa shida
-kutoa sauti Kama mluzi wakati wa kupumua
-kifua kubana
-kushindwa kuongea endapo ugonjwa utakuwa sugu
-kukohoa Sana asa wakati wa asubuh na usiku
Vipimo madactari huangalia vitu mbalimbali ili kujiridhisha Kama mgonjwa ana pumu navyo ni;
1.kipimo Cha Cha damu
2.kipimo cha kuchunguza uwezo wa mgonjwa kutoa hewa nje Mara baada ya kuvuta.
3.x-ray ya kifua.
Mgonjwa wa pumu anashauriwa kuwa na dawa wakati wote ambayo itakuwa inamsaidia pale ambapo atakuwa anashindwa kutoa au kuvuta hewa.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
Posti hii inahusu zaidi Aina ya mkojo usiokuwaa wa kawaida uwa na vitu vifuatavyo, ukiona dalili kama hizo wahi mapema hospitalini Ili upatiwe huduma.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi umuhimu wa mate mdomoni, mate ni majimaji ambayo hukaa mdomoni na husaidia katika kazi mbalimbali mdomoni.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa mtu anayetokwa na damu ya pua
Soma Zaidi...Somo Hili linakwenda kukueleza sababu za kwanini mbu hawezi kuambukiza ukimwi
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu madhara ya upungufu wa vitamin
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa mtu aliyekunywa sumu
Soma Zaidi...Post hii inahusu Aina za kuungua, kuungua ni Hali ya kubabuka kwa ngozi ya mwili na kusababisha madhara mbalimbali
Soma Zaidi...Vipi utamsaidia mti ambaye amepaliwa na maji? Post hii itakwenda kukifundisha jambo hili.
Soma Zaidi...