NGUZO ZA IMAN

Jifunze tawhid yaani kumpwekesha Allah subhaanah wata'aala

NGUZO ZA IMAN

.Dhana ya Imani katika Uislamu.
ï‚§Maana ya Tawhiid.
- Ni fani inayohusiana na imani ya kuwepo Allah (s.w) na siku ya mwisho pamoja na vipengele vyote vya nguzo za imani.
- Ni kumpwekesha Allah (s.w) katika kila kitu kwa Upweke na Umoja wake na uweza wake juu ya kila kitu.
ï‚§Matapo (makundi) ya Tawhiid.
- Tawhiid imegawanyika makundi makuu matatu:
1)Tawhiid – Rubbuubiyya: Ni Kumpwekesha Allah (s.w) katika Utawala wake.
2)Tawhiid – Asmaa Wassifaat: Kumpwekesha Allah katika Majina na Sifa zake.
3)Tawhiid – Ibaadah: Kumpwekesha Allah (s.w) katika Uungu na Kuabudiwa.

Maana ya imani kwa mujibu wa Qur’an (Uislamu).
- Ni kuwa na yakini moyoni juu ya kuwepo kitu au jambo fulani lisiloonekana kwa macho bali kwa dalili zinazothibitisha kuwepo kwake.

ï‚§Imani kwa mtazamo wa Uislamu na ule wa dini zingine:
- Katika Uislamu imani ni ile inayodhihirishwa katika vitendo vya mtu tofauti na dini zingine.
- Katika Uislamu imani juu ya kitu au jambo fulani lisiloonekana hutokana na dalili au ushahidi wa kuonesha uwepo wake tofauti na dini zingine.

Nguzo za Imani.
ï‚§Nguzo za imani ya Kiislamu ni Sita:
1.Kumuamini Mwenyezi Mungu (s.w).
2.Kuamini Malaika wa Mwenyezi Mungu (s.w).
3.Kuamini Vitabu vya Mwenyezi Mungu (s.w).
4.Kuamini Mitume wa Mwenyezi Mungu (s.w).
5.Kuamini Siku ya Mwisho.
6.Kuamini Qadar ya Mwenyezi Mungu (s.w) kuwa kheri na shari vyote vinatokana kwake.
Rejea Qur’an (2:285), (4:136), (57:22) na (11:6).

ï‚§Nguzo ya Ihsani.
- Nayo ni ‘kumuabudu Allah (s.w) kana kwamba unamuona na kama humuoni basi yeye anakuona’.
ï‚§Nani muumini wa kweli? (Sifa za muumini wa kweli).
- Ni yule ambaye imani yake inathibitishwa katika matendo ya kila kipengele cha maisha yake ya kila siku.
Rejea Qur’an (2:8-9).

- Ni yule anayejipamba na sifa za waumini zilizoainishwa katika Qur’an na Sunnah katika kukiendea kila kipengele cha maisha yake ya kila siku.
Rejea Qur’an (23:1-11), (25:63-77), (33:35-36), n.k.
- Ni yule anayeendea kila kipengele cha maisha yake kwa mujibu wa vipengele vyote vya nguzo za imani ya Kiislamu.
oHawi muumini wa kweli kwa imani isiyoendana na matendo wala kwa kuamini baadhi ya nguzo za imani.


                   

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Main: Dini File: Download PDF Views 2949

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani    👉2 Simulizi za Hadithi Audio    👉3 web hosting    👉4 Bongolite - Game zone - Play free game    👉5 kitabu cha Simulizi    👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)   

Post zinazofanana:

Kitabu Cha Dua 120

Sifanjema zinamstahikia Allah Mola wa viumbe vyote.

Soma Zaidi...
fadhila za kusoma quran

Fadhila na umuhimu wa kusoma quran 1.

Soma Zaidi...
Umuhimu wa ndoa na kuoa ama kuolwa katika jamii

Matamanio ya jimai ni katika maumbile na hayaepukiki.

Soma Zaidi...
mgawanyiko katika quran

MGAWANYIKO KATIKA QURAN Juzuu, Sura, Aya, Manzil, Qara Wataalamu wa elimu za Qurani katika fani za uandishi na usomaji wameigawanya Qurani katika mafungu ili kuwezesha urahisi kwa wasomaji wa qurani.

Soma Zaidi...
DARSA ZA TAWHID

Jifunze tawhid yaani kumpwekesha Allah subhaanah wata'aala

Soma Zaidi...