image

Kuamini qadar na qudra katika uislamu

Kuamini Qadar ya Allah (s.

Kuamini qadar na qudra katika uislamu

Kuamini qadar na qudra katika uislamu

Kuamini Qadar ya Allah (s.w)

Maana ya Qadar

Kilugha: maana yake ni kipimo, kiasi au makadirio.

Rejea Qur’an (54:49), (25:2), (36:39).

Kisheria: ni mpango (plan) wa Allah (s.w) unaohusu kutokea, kuwepo na hatima ya maumbile na viumbe vyake vyote na matukio yatakayopelekea kutokea na kuondoka kwake.
Rejea Qur’an (57:22), (6:59)Maana ya Qudra

Ni uwezo wa Allah (s.w) usio na mipaka katika kufanya chochote na lolote atakavyo

kwa kuliambia “kuwa” na linakuwa.Umuhimu wa Kuamini Qadar ya Allah (s.w)

(i) Kuamini Qadar ya Allah (s.w) ni nguzo ya sita katika nguzo za imani ya

Kiislamu.

(ii) Kuamini Qadar ya Allah (s.w) kikweli kweli ndio msingi wa imani sahihi ya muumini juu ya mipango na uwezo wa Allah (s.w).
(iii) Kutoamini Qadar ya Allah (s.w) ni miongoni mwa makosa yatayoharibu itikadi ya mja juu ya utendaji na mwenendo wake.
(iv) Hakuna chochote kitakachofanyika au kutokea kwa viumbe isipokuwa kimeandaliwa na kupangwa na Allah (s.w).


Mtazamo wa Uislamu juu ya Qadar

a) Ni makosa makubwa kudhani kuwa mtu anaweza kufanya jambo lolote lile kinyume na Qadar ya Allah (s.w).


b) Ni makosa makubwa mtu kumlaumu Allah (s.w) kwa maovu anayoyatenda kuwa ndiye amemkadiria kuyafanya.

c) Allah (s.w) anayajua yote atakayoyafanya mja hadi hatima ya maisha yake siku ya Qiyama hata kabla ya mtu huyo hajazaliwa.
Rejea Qur’an (11:6)d) Isidhaniwe kuwa maadamu mtu amechagua kumuasi Allah (s.w) basi Allah (s.w)

hana uwezo wa kumzuia, bali atafanya hivyo tu iwapo lipo katika Qadar ya Allah.e) Utatanishi wa Qadar huondoka kwa kuzingatia maeneo makuu mawili;

i. Eneo la hiari (uhuru) ambalo mtu huchagua kufanya jambo jema au baya atakalo.
ii. Eneo lisilo la hiari kwa mtu kuamua kufanya jambo lolote atakalo, mfano;

kuchagua wazazi wa kumzaa, sehemu, muda wa kuzaliwa, jinsia, n.k.f) Mtu ataulizwa au ataadhibiwa kwa matendo ya hiari tu ambayo ana uhuru nayo wa kuchagua lipi afanye na lipi asifanye.


g) Mwanaadamu hataulizwa kamwe matendo yasiyokuwa hiari kwake, mfano; kwa nini aliumbwa mweusi, mrefu, wa kike, wa kiume, kabila au nchi fulani, n.k.
Kueleweka vibaya kwa Qadar na Qudra ya Allah (s.w)

Baadhi ya Waislamu na watu wengine wanapotosha maana na nafasi ya Qadar na Qudra ya Allah (s.w) kama ifuatavyo;

i. Kuacha kutekeleza wajibu wao kwa Allah kwa kusingizia kuwa “imeshaandikwa

kwenye kitabu cha Allah kuwa sisi hatutatekeleza au tutatekeleza jambo fulani”ii. Baadhi ya watu wanaojiita waislamu kuacha kutekeleza amri za Allah (s.w) kama swala, funga, n.k. kwa kusingizia kuwa hawajajaaliwa kufanya hivyo na watatekeleza pindi watakapojaaliwa.

iii. Baadhi ya watu, miongoni mwa waislamu hufanya maovu kwa shangwe kwa kudai kuwa hivyo ndivyo alivyokadiriwa na Allah (s.w) na wasingeweza kukwepa Qadar yake.

iv. Baadhi ya watu kudai kuwa, “Allah (s.w) mwenyewe ameshajua na ameshapanga kuwa watu wa motoni au peponi, hivyo hakuna haja ya wao kufanya uovu au wema”.

v. Watu wengine wanadai kuwa, “Allah (s.w) amewapendelea wengine kwa kuwapangia kwenda peponi huku akiwadhulumu wengine kwa kuwapangia kwenda motoni.
Madai haya hutiliwa nguvu hata kwa ushahidi wa aya za Qur’an kama ifuatavyo;

Rejea Qur’an (39:36-37), (29:62), (2:284), n.kUpotofu na udhaifu wa madai haya juu ya Qadar na Qudra ya Allah

- Kwanza, Allah (s.w) humuongoza mtu kwenye jambo alitakalo mwenyewe kulifanya ikiwa jema au ovu.
Rejea Qur’an (16:33), (43:76), (42:30), n.k- Pili, Allah (s.w) atamwadhibu mtu kwa matendo yake ya hiari na uhuru wa kuchagua kufanya uovu na kumpa malipo ya peponi kwa kuchagua kufanya wema.
Rejea Qur’an (16:28), (17:15), (76:3-7), (91:1-10), (10:9), (47:17), (18:13), n.k- Tatu, mtu kamwe hataadhibiwa kwa matendo ambayo hakuwa na hiari na uhuru nayo, kama kuzaliwa kipofu, kilema, mwanamke, mwanamme, kabila fulani, n.k. Rejea Qur’an (2:286), n.k.- Nne, Allah (s.w) ni mjuzi wa kila jambo lililotokea na litakalotokea, hivyo anajua wanaadamu watakaojifanyia wema na kwenda peponi na watakaojifanyia uovu na kwenda motoni.
Rejea Qur’an (11:6), (6:59), (65:12), n.k.- Tano, suala la kuongoka au kupotea ni la mtu mwenyewe kujichagulia kwani Allah (s.w) amebainisha njia zote, ya uongofu na ya upotofu kisha Allah (s.w) humupeleka huko alikochagua mtu mwenyewe.
Rejea Qur’an (91:7-8), (47:17), (76:1-3), n.kMaana ya kuamini Qadar ya Allah katika maisha ya kila siku

(i) Muumini kwa kujua kuwa fursa, bahati, vipaji na neema alizonazo, amekadiriwa na

Allah (s.w) hanabudi kuvitumia ipasavyo ili kufukia lengo la kuumbwa kwake.(ii) Mja akijua kuwa neema yeyote aliyonayo ni dhamana na ataulizwa kwayo, hatalalama ikiwa amepewa chache au nyingi, kwani ndio makadirio ya Allah (s.w).


(iii) Mja ataweza kutumia vyema neema zote kwa kutaraji matunda na malipo yake kutoka kwa Allah (s.w) pekee aliyempa.(iv) Mja anapofikwa na misukosuko iliyo nje na uwezo wake wa kibinaadamu huwa mwenye uvumilivu na subira kwa kujua ni Qadar ya Allah (s.w).
Rejea Qur’an (57:22-23), (2:155-156)(v) Mja pia huwa jasiri kusimamia haki na kupigania dini ya Allah (s.w) kwa kuwa ndiye mkadiriaji na mdhibiti pekee wa kila jambo.
Rejea Qur’an (9:51)
                              

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1062


Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-