Kuamini Mwenyezi Mungu sio suala la Kibubusa au Kufuata Mkumbo.


Makafiri wanadai kuwa kuamini kuwepo kwa Mwenyezi Mungu (s.w) ni ububusa na kufuata mkumbo bila ya udadisi na kutumia akili. Dai hili sio la kweli kwa sababu zifuatazo;


Kwanza, Mwenyezi Mungu (s.w) ametuma Mitume mbali mbali kwa wanadamu ili kuwafundisha na kutoa dalili za kuwepo kwake bila ya shaka yeyote kwa dalili za wazi ili kumfahamu na kuweza kumuabudu ipasavyo.
Rejea Qur’an (4:165).Pili, Vipawa, ufahamu na akili alivyopewa mwanaadamu ni kumuwezesha kumtambua Muumba wake na kuweza kumuabudu inavyostahiki. Hivyo kutotumia akili katika kumtambua Mwenyezi Mungu kupitia ishara mbali mbali ni kustahiki adhabu.
Rejea Qur’an (3:190), (30:21), (7:179), (8:22) na (12:105).Tatu, Mitume wa Mwenyezi Mungu pamoja na kuwafundisha wafuasi wao juu ya uwepo wa Mwenyezi Mungu, hawakuwataka kuamini na kufuata bila ya hoja na dalili za wazi bali walionyesha ishara na miujiza kuthibitisha ujumbe wao.Nne, Msisitizo wa Elimu katika Qur’an kuwa faradhi ya kwanza kama nyenzo pekee ya kumuwezesha mwanaadamu kumjua na kumuabudu Mola wake na kuweza kuyamudu mazingira yanayomzunguka na kuweza kusimamisha Ukhalifa ardhini.Tano, Maana ya neno “imani” ambalo lina maana ya ‘kuwa na yakini moyoni pasina shaka’ yeyote juu ya jambo fulani kwa kuwa na ujuzi nalo na pia kupitia dalili na ishara za kutosha za kuonyesha kuwepo kwake.