2.3.Kuamini Vitabu Vya Mwenyezi Mungu (s.w Quran, tawrat, Zabur na injili

2.

2.3.Kuamini Vitabu Vya Mwenyezi Mungu (s.w Quran, tawrat, Zabur na injili

2.3.Kuamini Vitabu Vya Mwenyezi Mungu (s.w

2.3.Kuamini Vitabu Vya Mwenyezi Mungu (s.w)
Vitabu vya Mwenyezi Mungu vilivyotajwa ndani ya Qur'an ni;
1.Suhufi ' aliteremshiwa Nabii Ibrahim (a.s) na Nabii Musa (a.s).
2.Taurat ' aliyoteremshiwa Nabii Musa (a.s)
3.Zaburi ' aliyoteremshiwa Nabii Daud (a.s)
4.Injili ' aliyoteremshiwa Nabii Isa (a.s) na
5.Qur'an ' aliyoteremshiwa Nabii au Mtume Muhammad (s.a.w).3. Kuhifadhiwa na Kulindwa Vitabu.
Qur'an imebaki katika asili yake kama ilivyoteremsha bila kubadilishwa chochote na wanaadamu ndani yake.
Rejea Qur'an (15:9) na (41:42)

Vitabu vingine vimepotea katika asili yake kwa kupunguzwa, kuongezwa na kupotoshwa asili ya ujumbe wake na mikono ya wanaadamu..4. Hitoria ya Kushushwa Vitabu.
Historia ya kushushwa Qur'an inajulikana vyema mfano; namna, sehemu, muda/kipindi na sababu ya kuteremshwa kila aya.

Vitabu vingine historia ya kushushwa kwao haijulikani, mfano; muda, nama, sababu au sehemu.
Lengo la kushushwa Vitabu vya Mwenyezi Mungu (s.w).

Ni kuwa mwongozo sahihi wa maisha ya mwanaadamu katika kufuata maamrisho na kuacha makatazo yote ya Mwenyezi Mungu (s.w) hapa ulimwenguni.
Rejea Qur'an (2:38-39), (2:185) na (5:44).Maana ya Kuamini Vitabu vya Mwenyezi Mungu (s.w) katika maisha ya kila siku.
Waumini wa kweli wa vitabu vya Mwenyezi Mungu (s.w) ni wale wanaoendesha kila kipengele cha maisha yao ya kila siku kwa mujibu wa mwongozo uliopo katika vitabu hivyo.Sababu za kutokubalika Vitabu vilivyotangulia kuwa Mwongozo sahihi wa maisha ya mwanaadamu zama hizi.
1.Vitabu vilivyotangulia vimeingiliwa na mikono na matashi ya wanaadamu kiasi cha kupoteza au kupotoshwa ujumbe wake wa asili.

2.Lugha ya vitabu vilivyotangulia imetoweka na kusahaulika duniani kiasi kwamba hata kingelikuwapo kimojawapo katika lugha yake asili, ujumbe wake usingelifahamika kwa watu.

3.Vitabu vilivyotangulia vilikuwa ni mwongozo kwa watu maalum na kwa wakati maalum tu, havikuwa mwongozo kwa walimwengu wote na nyakati zote.
Sababu za Qur'an kuwa mwongozo sahihi pekee wa maisha ya mwanaadamu.
1. Qur'an yote ni maneno ya Mwenyezi Mungu (s.w) peke yake, hivyo ni mwongozo wa uhakika.
2. Ujumbe wa Qur'an umeelekezwa kwa walimwengu wote na zama zote zilizobakia hadi siku ya Qiyama.Maana ya Kuiamini Qur'an katika maisha ya kila siku.
Maana halisi ya kuiamini Qur'an kama Kitabu pekee cha mwongozo sahihi wa maisha ya mwanaadamu (muumini) ni kufanya yafuatayo;
i.Kuwa na yakini pasina shaka yeyote kuwa Qur'an yote ni maneno ya Mwenyezi Mungu (s.w) peke yake.
Rejea Qur'an (2:2).ii.Kuufahamu vyema ujumbe wa Qur'an na kuuheshimu inavyostahiki kwa kujizatiti katika kujifunza kuisoma na kuijua ipasavyo.
Rejea Qur'an (73:4) na (7:204-205).iii.Kulifahamu vyema lengo la Qur'an na kuiendea kwa lengo lake tu.
Rejea Qur'an (14:1), (2:185) na (16:64).iv.Kuitekeleza Qur'an katika kukiendea kila kipengele cha maisha yetu ya kila siku kwa mujibu wa lengo lake tu.
Rejea Qur'an (5:44, 46-47).                   

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 791

Post zifazofanana:-

MAMA YAKE MTUME MUHAMMAD (S.A.W) ANAMLEA MTUME MUHAMAD AKIWA NA UMRI WA MIAKA MINNE (4)
KULELEWA NA MAMA YAKE ALIPOFIKA MIAKA MINNEMtume (s. Soma Zaidi...

Masomo ya Dua na Faida zake Dua
Soma Dua mbalimbali hapa, Soma Zaidi...

Kibri cha Ibilis na Uadui Wake Dhidi ya Binadamu
Ibilis ni katika jamii ya majini aliyekuwa pamoja na Malaika wakati amri ya kumsujudia Adam inatolewa. Soma Zaidi...

KUAMINI VITABU VYA ALLAH (S.W)
Mtu hawi Muumini wa kweli mpaka awe na yakini juu ya vitabu vya Allah (s. Soma Zaidi...

UMBILE LA MBINGU NA ARDHI
'Katika kuumbwa mbingu na ardhi na mfuatano wa usiku na mchana,ziko alama (hoja) za kuonyesha kuwepo Allah (s. Soma Zaidi...

Hadithi aliyoisimulia Kijakazi kwa sultan
Soma Zaidi...

Kutowatii Wazazi katika kumuasi Allah (s.w)
"Na (wazazi wako) wakikushurutisha kunishirikisha na (yale) ambayo huna ilimu nayo, usiwatii; lakini kaa nao kwa wema hapa duniani (Maadamu ni wazee wako, ila usiwafuate tu mwenendo wao mbaya); Shika mwenendo wa wale wanaoelekea kwangu, kisha marejeo yenu Soma Zaidi...

NI UPI MKATABA WA AL-FUDHUL NA ASILI YAKE, ATHARI ZAKE NA WALOHUSIKA
MKATABA WA AL-FUDHULBaada ya vita hivi viongozi wa pande mbili hizi waliamuwa wakae chini na wakubaliane kuweka kanun i na utaratibu utakaozuia kutotokea uonevu kama huuu tena. Soma Zaidi...

HADITHI YA MZEE WA KWANZA NA MBUZI
Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA MZEE WA KWANZA NA MBUZI WAKE. Soma Zaidi...

Hukumu ya Mtu asiyefunga kwa makusudi mwezi wa ramadhani
Soma Zaidi...

Mambo ya kuzingatia kabla ya kugawanya urithi
Soma Zaidi...

HISTORIA YA MTUME ILYASA(A.S)
Mtume Ilyasa ni mmoja wa Mitume waliotumwa kupitia kizazi cha Bani Israil. Soma Zaidi...