1.
1.0 NJIA ZA KUMJUA MWENYEZI MUNGU (S.W).
Njia za Kumtambua Mwenyezi Mungu (s.w).
a)Nafasi ya Fitrah (maumbile).
- Kila Mwanaadamu amepandikizwa hisia za kimaumbile zinazomtambua Mungu kupitia ujuzi wa kutambua mema na maovu.
- Mwanaadamu akipatwa na raha au misukosuko na huzuni hukiri uwepo wa Mwenyezi Mungu (s.w).
Rejea Qurโan (17:67), (30:30) na (91:7-8).
b)Vipaji vya Binaadamu.
- Vipaji vya akili na milango ya fahamu na fani zingine za elimu ni nyenzo pekee zikitumiwa vilivyo humuwezesha mtu kumjua Mola wake.
Rejea Qurโan (3:190-191), (35:28).
c)Nafsi ya mwanaadamu.
- Mfumo mzima wa mwili wa mwanaadamu na utendaji wake wa kazi wa ajabu wa viunge mbali mbali vya mwili kama kuyeyusha chakula tumboni, msukumo wa damu mwilini, n.k. ni ishara tosha juu ya uwepo wa Mwenyezi Mungu (s.w).
Rejea Qurโan (51:20-21)
d)Mazingira.
- Utegemezi na uhusiano wa kimahitaji ya kutumia rasilimali ya kuishi kati ya mimea, wanyama na binaadamu (ecological balance).
- Maumbile mengine kama mbingu, ardhi na yote yanayoonekana na yasiyooneka katika mazingira yanayotunguka.
Rejea Qurโan (3:190).
e)Wahyi (Ufunuo).
- Wahyi ndio nyenzo kuu ya kumwezesha mwanaadamu kumtambua Mwenyezi Mungu (s.w) kwa usahihi unaotakikana.
- Elimu, vipaji na ujuzi au sayansi pekee haviwezi kumwezesha mwanaadamu kumtambua Mungu kwa baadhi ya maeneo, mfano nguzo za imani, n.k.
Umeionaje Makala hii.. ?
MGAWANYIKO KATIKA QURAN Juzuu, Sura, Aya, Manzil, Qara Wataalamu wa elimu za Qurani katika fani za uandishi na usomaji wameigawanya Qurani katika mafungu ili kuwezesha urahisi kwa wasomaji wa qurani.
Soma Zaidi...FADHILA ZA BAADHI YA SURA Umuhimu na ubora wa baadhi ya sura na aya.
Soma Zaidi...