image

maana na asili ya dini, kazi zake na nadharia potofu za makafiri kuhusu dini

2.

maana na asili ya dini, kazi zake na nadharia potofu za makafiri kuhusu dini

Dhadharia juu ya mtazamo wa dini asili na maana yake

2.0MTAZAMO WA UISLAMU JUU YA DINI
Mtazamo wa Makafiri juu ya Dini.
Mtazamo wa kikafiri juu ya dini uko katika sehemu kuu tatu zifuatazo;
a)Maana ya dini.
b)Chimbuko, Asili au Chanzo cha dini.
c)Kazi ya dini katika jamii.



1. Maana ya dini.
-Ni imani juu ya kuwepo Mungu Muumba Muweza na Mwenye nguvu juu ya kitu.
Rejea tafsiri ya neno ‘Religion’ katika Kamusi ya Kiingereza.

“Belief in the existence of a supernatural ruling power the creator …..”
Tafsiri:
“Dini ni imani ya kuwepo Mungu Muumba aliyemuweza na mwenye nguvu…..”



2.Chimbuko, Chanzo au Asili ya dini.
-Makafiri wanadai kuwa chimbuko la dini linatokana na mawazo na fikra finyu za mwanaadamu alipokuwa katika maisha ya ujima (primitive age).

-Dini ni fikra na dhana alizoibua mwanaadamu baada ya kushindwa kutatua matatizo ya kijamii, uchumi, siasa, n.k.

-Dini ni dhana iliyoibuliwa na mwanaadamu kutokana na uduni wa maendeleo ya sayansi na teknolojia.
Rejea kitabu cha Kafiri, F. Angels kiitwacho ‘Anti-Duhring’

“Religion arose from primitive conceptions of men……”
Tafsiri:
“Dini imeibuka kutokana na ujima (uduni) wa mawazo ya mwanaadamu……”



3. Kazi ya dini katika jamii.
Ukirejea historia ya Ulaya na nchi za Magharibi, Kanisa kama dini lilitumika kwa kazi zifuatazo;

- Ni chombo kinacholeta unyonyaji, ukandamizaji na dhuluma katika jamii.
Rejea Qur’an (28:4).

-Ni chombo cha kuleta matabaka na ubaguzi kati ya viongozi (mabwana) na waongozwa, matajiri na masikini katika jamii.

-Pia dini inaaminika kuwa ni chombo cha kulinda na kutetea maslahi ya watawala kupitia mafundisho yake.

-Dini inatumika kama chombo cha kuchuma na kujilimbikizia mali kwa wakuu (viongozi) wake kwa kuwatumia wafuasi wake.




Udhaifu wa Mtazamo wa Makafiri juu ya Dini dhidi ya Mtazamo wa Uislamu.
Katika Uislamu dini maana yake ni mfumo, utaratibu, mila kamili wa maisha unaofuatwa na wanaadamu.
Rejea Qur’an (3:83), (3:85), (18:20), (9:33) na (16:9).



Tofauti na Makafiri, Uislamu unatazama dini kama ifuatavyo:

a)Maana ya Dini.
b)Chimbuko, Chanzo au Asili ya Dini.
c)Kazi ya Dini katika jamii.



(a)Maana ya Dini.
- Dini ni mfumo, utaratibu kamili wa maisha unaofuatwa na wanaadamu. Kinyume na mtazamo wa makafiri kuwa dini ni imani juu ya kuwepo Mungu Muumba.

- Hivyo, dini ni utaratibu wowote ule wa maisha wanaofuata watu (mtu) katika kuendesha maisha yake, sio lazima kuamini kuwepo wa Mungu Muumba.
Rejea Qur’an (109:1-6), (9:31), (25:43), (61:8-9) na (17:81).



(b)Chimbuko, Asili au Chanzo cha Dini.
-Dai la makafiri kuwa chimbuko la dini limetokana na fikra finyu na uduni wa maendeleo ya sayansi na teknolojia wakati wa ujima, sio sahihi kwa sababu;

oHakuna kipindi chochote cha maisha, mwanaadamu aliishi katika ujima na fikra finyu, kwani tangu mwanaadamu wa mwanzo alipewa elimu na fani juu ya kuyamudu mazingira yake.

oPia mwanaadamu kila zama aliletewa mwongozo sahihi wa maisha kupitia mafundisho ya mitume unaotoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w).
Rejea Qur’an (2:31) na (2:38-39).

- Hivyo katika Uislamu, chanzo na asili ya dini ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w) kwa ushahidi wa aya na hadith mbali mbali.



(c)Kazi ya Dini katika jamii.
-Mtazamo wa Makafiri, dini ni chombo cha unyonyaji, dhuluma na kujenga matabaka katika jamii, dai hili ni la kweli au sio la kweli kama ifuatavyo;

-Ukweli wa dai hili ni sahihi kwa dini zote za wanaadamu kama Ushirikina, Utawa na Ukafiri.

-Udhaifu wa dai hili, ni kuwa dini sahihi ilikuwa na kazi ya kuikomboa jamii kutokana na aina zote za ukandamizaji, utabaka, dhuluma, n.k.

- Hivyo katika Uislamu, dini ina kazi ya kuiongoza jamii katika maisha ya haki, uadilifu na usawa na kupigana na aina zote za dhuluma na ukandamizaji.
Rejea Qur’an (57:25), (28:4) na (7:103-105).



Kwa nini mwanaadamu hawezi kuishi bila ya dini?
Mwanaadamu yeyote hawezi kuishi bila ya dini hata kama atadai kuwa hana dini kwa sababu zifuatazo;
1.Maana halisi ya dini.
Dini ni utaratibu wa maisha anaofuata mwanaadamu katika kuendesha maisha yake ya kila siku kibinafsi na kijamii.



2.Umbile la mwanaadamu ni la kidini.
Umbile la mwanaadamu limefungamana na kanuni na sheria za maumbile yote yanayomzunguka.
Rejea Qur’an (30:30), (3:83).



3.Vipawa alivyotunukiwa mwanaadamu.
Tofauti na wanyama na viumbe wengine, mwanaadamu ametunukiwa vipawa vya ziada vifuatavyo;
i.Akili na Ufahamu wa hali ya juu.
Vinamsaidia kufikiri na kutafakari mambo yanayomhusu yeye mwenyewe na mazingira yanayomzunguka.



ii.Utambuzi binafsi (self-consciousness).
Humuwezesha kuhusianisha yeye na mazingira (viumbe) yanayomzunguka.



iii.Uwezo wa kujielimisha na kuelimika.
Elimu ni nyenzo pekee inayomuwezesha mwanaadamu kuyamudu mazingira kwa ufanisi.



iv.Uhuru wa kufanya atakalo.
Mwanaadamu amepewa vipaji, elimu na ujuzi, ilivimuwezeshe kubainisha njia sahihi ya kufuata katika maisha yake ya kila siku.



                   





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 616


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Simulizi za Hadithi Audio     👉5 Kitau cha Fiqh     👉6 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Taratibu za mahari katika uislamu
Soma Zaidi...

ihram na nia ya Hija na Umra
1. Soma Zaidi...

Presha ya kupanda (hypertension) dalili zake, na njia za kukabiliana nayo
Soma Zaidi...

Haya ndio matendo ya hija
Soma Zaidi...

mgawanyiko katika quran
MGAWANYIKO KATIKA QURAN Juzuu, Sura, Aya, Manzil, Qara Wataalamu wa elimu za Qurani katika fani za uandishi na usomaji wameigawanya Qurani katika mafungu ili kuwezesha urahisi kwa wasomaji wa qurani. Soma Zaidi...

DARSA ZA TAWHID
Jifunze tawhid yaani kumpwekesha Allah subhaanah wata'aala Soma Zaidi...

namna ya kuswali swala ya dhuha
7. Soma Zaidi...

Athari na faida za kumuamini Allah katika maisha ya mwanadamu duniani na akhera
Athari za Kumuamini Mwenyezi Mungu (s. Soma Zaidi...

Sababu za kushuka sura kwenye quran na fadhila za sura mbalimbali kwenye quran
Soma Zaidi...

Hadithi aliyoisimulia Kijakazi kwa sultan
Soma Zaidi...

nmna ya kufanya Talbiy kwa mwenye kuhiji
2. Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula Mbegu za maboga
Soma Zaidi...