Nguzo 6 za iman ya dini ya kiislamu kwa mafundisho ya quran na sunnah

Nguzo za Imani.

Nguzo 6 za iman ya dini ya kiislamu kwa mafundisho ya quran na sunnah

Nguzo za imani ya dini ya kiislamu

Nguzo za Imani.
1.Kumuamini Mwenyezi Mungu.
2.Kuamini Malaika wake.
3.Kuamini Vitabu Vyake.
4.Kuamini Mitume Wake.
5.Kuamini siku ya Mwisho.
6.Kuamini Qadar ya Mwenyezi Mungu.



1.Kumuamini Mwenyezi Mungu (s.w).
- Imani juu ya kuwepo Mwenyezi Mungu ni jambo la kwanza kabisa kwa kila mwenye akili timamu kupitia ishara na maumbile mbali mbali yanayotuzunguka.
Rejea Qur'an (3:190).



- Baada ya kumtambua, ni kumuabudu ipasavyo na kutomshirikisha katika sifa na majina yake matukufu na kiumbe yeyote.
Rejea Qur'an (18:109), (31:27), (57:1-7), (59:22-24).
Rejea Kitabu cha 2, EDK, Shule za Sekondari; Uk.8-16.



2.Kuamini Malaika wa Mwenyezi Mungu.
- Malaika ni viumbe wa Mwenyezi Mungu walioumbwa kutokana na nuru kwa lengo la kumtumikia Mwenyezi Mungu (s.w).

- Ni viumbe wa kiroho, wasio na jinsia, wenye mabawa na wenye uwezo wa kujimithilisha na kitu (kiumbe) chochote.

- Hawana matashi ya kibinaadamu kama kula, kulala, kunywa, kuchoka, kuugua na hawana hiari kwa kila wanachoamrishwa na Mwenyezi Mungu (s.w).
Rejea Qur'an (16:49-50), (7:206) na (21:26-27).



3.Kuamini Vitabu vya Mwenyezi Mungu (s.w).
- Kuamini vitabu vya Allah (s.w) ni lazima kwa kila muumini wa kweli kama vilivyoainishwa katika Qur'an, ambavyo baadhi ni;
a)Suhufi ' aliyoteremshiwa Nabii Ibrahim (a.s) na Nabii Musa (a.s).
b)Taurat ' aliyoteremshiwa Nabii Musa (a.s)
c)Zaburi ' aliyoteremshiwa Nabii Daud (a.s)
d)Injili ' aliyoteremshiwa Nabii Isa (a.s) na
e)Qur'an ' aliyoteremshiwa Nabii au Mtume Muhammad (s.a.w).



- Vitabu hivi vimeteremshwa kwa lengo la kuwaongoza wanaadamu katika njia sahihi na iliyonyooka ya maisha yao ili kufikia lengo la kuumbwa kwao.
Rejea Qur'an (57:25) na (5:46).



Sababu ya Vitabu Vilivyotangulia kutajwa ndani ya Qur'an:
1. Qur'an ndiyo Kitabu cha mwisho kilichoteremshwa kwa ajili ya kuwaongoza walimwengu wote.
2. Vimetajwa ili kuwafahamisha waislamu juu ya uwiano, usahihi na upotofu wa mafundisho hayo na yale ya Qur'an.
3. Mwenyezi Mungu (s.w) kutaka kuonyesha nafasi na utata wa vitabu hivyo kutumika zama hizi kama mwongozo wa maisha.
4. Mwenyezi Mungu (s.w) kutaka kuonyesha upungufu, mabadilisho na upotofu uliofanywa ndani ya Vitabu hivyo.
Rejea Qur'an (6:92), (2:75), (4:14), (5:15), (5:48) na (16:64).



4.Kuamini Mitume wa Mwenyezi Mungu (s.w).
- Mitume ni wanaadamu wanaume walioteliwa ili kuwaongoza na kuwa mifano bora ya kuigwa kwa watu (ummah) wao katika kutekeleza ujumbe wao.

-Idadi kamili ya mitume wote wa Mwenyezi Mungu (s.w) haijulikani, bali waliotajwa ndani ya Qur'an ni 25.
Rejea Qur'an (10:47), (6:83-86)
Rejea Kitabu cha 2, EDK, Shule za Sekondari; Uk.23.



Sifa za Mitume.
i.Ni watu walizaliwa, walioa, walikula, waliugua, walikufa, n.k. kama binaadamu wa kawaida isipokuwa Nabii Adamu (a.s).
ii.Walikuwa na kila tabia njema, wakweli, waaminifu na wenye huruma.
iii.Walikuwa na upeo wa Elimu wa hali ya juu kuliko watu wote enzi zao kwa sababu kuletewa kwao wahayi.
iv.Walikuwa Wacha-Mungu wa hali ya juu kuliko watu wote.



Kazi za Mitume.
i.Kufahamisha na kufundisha juu ya uwepo wa Mwenyezi Mungu (s.w) na sifa zake. Qur'an (21:25), (16:36).
ii.Kufahamisha mambo ya ghaibu (Akhera) kama Moto, Pepo, Kiyama, Hisabu, Maisha ya Barzaq (kaburini) n.k.
iii.Kufundisha njia sahihi ya maisha anayoiridhia Mwenyezi Mungu inayopelekea kunusurika na adhabu zake. Qur'an (3:164).
iv.Kusaidiana na wafuasi wao katika kuamrisha mema na kuondosha maovu katika jamii.
v.Kuonya kutokana na adhabu na kubashiria mema kwa wafanyao mema.


5.Kuamini Siku ya Mwisho.
- Ni kuwa na yakini moyoni kuwa kuna maisha mengine baada ya kufa.
?Hatua za maisha baada ya kufa:
a)Kutokwa na roho.
b)Maisha ya kaburini (Barzaq).
c)Kufufuliwa.
d)Kuhesabiwa (Hisabu).
e)Kuishi Peponi au Motoni milele
- Kwa mujibu wa amali zao (vitendo vyao).



6.Kuamini Qadar ya Mwenyezi Mungu (s.w).
-Ni kuwa na yakini moyoni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w) anao mpango wa viumbe vyake vyote alioweka kabla ya kuumba chochote.

- Amekiumba kila kiumbe kwa lengo maalumu na kukikadiria mahitaji yake yote.
Rejea Qur'an (11:6), (57:22), (54:49) na (25:2).



                   



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 2554


Download our Apps
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

NAMNA YA KUCHINJA KATIKA UISLAMU
' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ': "' ' ' '... Soma Zaidi...

Mawazo Tofauti Kuhusiana na Uchaguzi wa Abubakar
Soma Zaidi...

Sifa za Kuwa Mpole na Mnyenyekevu
22. Soma Zaidi...

Kwa nini mkono umekatwa
KUKATWA MKONO NA KURITHI UTAJIRI Basi niliweza kulala kwa mke wangu siku ile na asubuhi nilimuashia kipande 1000 vya dhahabu na kuondoka kuelekea dukani. Soma Zaidi...

Haki na wajibu kwa mayatima
Soma Zaidi...

Darsa za Sira historia ya Mtume (s.a.w) Jaribio la 03
Soma Zaidi...

Maharimu ni wanawake na wanaume walioharamishwa kuoana
Soma Zaidi...

Bani Israil Kuabudu Ndama
Wakati Nabii Musa(a. Soma Zaidi...

quran na sayansi
YALIYOMONENO LA AWALI1. Soma Zaidi...

Mapambano ya Mtume Muhammad dhidi ya Wanafiki na hila zao Madina
Soma Zaidi...

Vipi funga yaani swaumu itapelekea uchamungu na kutekeleza lengo
Funga inavyomuandaa mtu kuwa mcha-Mungu. Soma Zaidi...

Sababu za kushuka kwa Surat al-Kawthar na fadhila zake
SURATUL-KAUTHAR Imeteremshwa maka, na sura hii imeshuka kwa sababu al-aAs ibn Waail. Soma Zaidi...