Kuendeshwa kwa dola ya kiislamu, Uchumi, ulinzi, haki na sheria, siasa na vikao vya shura

Uendeshaji wa Dola ya Kiislamu Madinah.

Kuendeshwa kwa dola ya kiislamu, Uchumi, ulinzi, haki na sheria, siasa na vikao vya shura

Kuendeshwa kwa dola ya kiislamu, Uchumi, ulinzi, haki na sheria, siasa na vikao vya shura

Uendeshaji wa Dola ya Kiislamu Madinah.
Mfumo wa Mapato na Uchumi katika Dola (Serikali) ya Kiislamu Madinah.
Dola (Serikali) ya Kiislamu Madinah ilipata mapato yake kupitia njia zifuatazo;

1.Zaka na Sadaka ndio ilikuwa njia kuu ya kukusanya mapato ya serikali (Dola) ya Kiislamu iliyowahusu waislamu wote wenye uwezo.

2.Jizya – Ni kodi waliokuwa wanalipa wasiokuwa waislamu wanaume tu wenye uwezo wa kuwa askari kwa ajili ya ulinzi wa Dola.

3.Al-Kharaj – Ni kodi waliolipa wasiokuwa waislamu, walio na mashamba katika Dola ya Kiislamu.

4.Al-fay – Ni mapato yanayotokana na mashamba ya Serikali (Dola) ya Kiislamu Madinah.

5.Al-Ghanimah (Ngawira) – Ni mapato yanayotokana na mali ilitekwa katika vita, iliyolipwa 1/5 ya mali yote ilyotekwa.

6.Ushr – Ni kodi (ushuru) iliyotolewa na waislamu wenye ardhi katika Serikali (Dola) ya Kiislamu kwa kiwango cha 10% kwa maji ya asili (mvua) na 5% kwa maji ya kumwagilia.

7.Zaraib – Ilikuwa ni kodi zilizotozwa na serikali (Dola) ya Kiislamu kwa muda kwa ajili ya maslahi ya nchi.


Msonge wa Uongozi na Siasa katika serikali (Dola) ya Kiislamu Madinah.
Tofauti na serikali zingine, serikali ya Kiislamu ilijengwa katika misingi mikuu mitatu; Tawhiid, Utume na Ukhalifa (nafasi ya mwanaadamu hapa ulimwenguni). Rejea Qur’an (30:20), (3:189), (12:40), (7:54), (4:80), (4:65), (24:55), (2:30).
Mgawanyo na msonge wa uongozi wa Dola ya Kiislamu ulikuwa kama ifuatavyo;

- Qur’an – ilikuwa ndio Katiba kuu (Constitution) ya kuongozea Dola iliyotafsiriwa kivitendo (Sunnah) na Mtume (s.a.w) mwenyewe.

- Mtume (s.a.w.) – alikuwa ndio kiongozi na amiri jeshi mkuu (commander in chief) wa Dola ya Kiislamu aliyesimamia na kuendesha kazi zote za Dola ambapo Msikiti ulikuwa ndio Ikulu ya Dola (State House).

- Shura (Cabinet) – Mtume (s.a.w) aliteua washauri wake wakuu wakaribu, weledi na wazoefu (Baraza la Mawaziri) katika shughuli zote za kuongoza Dola ambao ni Abu Bakr (r.a), Umar bin Khattab (r.a), Uthman bin Affan (r.a), Ally bin Abu Twalib (r.a) na Hamza bin Abdul-Muttalib (r.a) na wengineo.

- Sekretarieti (Secretarial) – Mtume (s.a.w) aliteua jopo la waandishi na watunza kumbukumbu na nyaraka zote za serikali.

- Wali au Gavana – Walikuwa ni wakuu wa majimbo (mikoa) ambao waliteuliwa na Mtume (s.a.w) ili kuhakikisha sheria na haki zinatekelezwa ipasavyo katika majimbo yao.

- Amil – Walikuwa ni wakusanyaji wa Zaka na Sadaka walioteuliwa na Mtume (s.a.w) kila jimbo la Dola ya Kiislamu.

- Kadhi – Mtume (s.a.w) alikuwa ndiye Jaji mkuu wa Dola ya Kiislamu na aliteua Kadhi (Jaji) kila jimbo (mkoa) aliyesimamia haki na hukumu zote kwa mujibu wa Qur’an na Hadith.





Mfumo wa Ulinzi na Usalama katika Dola ya Kiislamu Madinah.
Dola (serikali) ya Kiislamu Madinah iliposimama na kuanza kazi za kuongoza jamii iliandamwa na maadui wa kila aina. Mtume (s.a.w) aliweka mikakati na mbinu madhubuti za kuilinda na kuihami serikali yake ikiwa ni pamoja na;

i.Misafara ya Kujihami (Patrol) na Upelelezi.
Mtume (s.a.w) aliweka watu maalum kwa ajili ya kulinda mipaka ya Dola na kupeleleza harakati za maadui dhidi ya Uislamu na waislamu.
Rejea Qur’an (4:71).

ii.Kuweka Mikataba ya amani.
Mtume (s.a.w) aliweka mikataba ya amani na makabila ambayo hayakusilimu yaliyopembezoni mwa Dola ya Kiislamu kama, Banu Dumra, Mudlaj, n.k.
Rejea Qur’an (9:13-15).

iii.Kupigana vita.
Njia hii ililazimika kutumika baada ya kuzidi uonevu, dhuluma na choko choko za wazi dhidi ya Waislamu na Uislamu.
Rejea Qur’an (2:193), (9:111) na (9:29)

iv.Sera ya wazi juu ya wanafiki.
Mtume (s.a.w) alichukua tahadhari na hatua dhidi ya wanafiki waliojidhihirisha wazi kutengana na ummah wa waislamu kwa kuwatenga.
Rejea Qur’an (9:73), (9:84) na (9:80).

v.Sera ya Uislamu juu ya amani.
Mtume (s.a.w) alitekeleza na kuelekeza mafundisho ya Uislamu juu ya kutunza na kulinda amani kama fursa na dhamana katika kueneza Uislamu.
Rejea Qur’an (8:61), (16:90), (2:84), (8:5-8).



vi.Uhusiano wa Kiplomasia na nchi za nje.
Mtume (s.a.w) aliweka sera ya wazi juu ya uandikashaji na utekelezaji wa mikataba mbali mbali na maadui wa Uislamu kama Aqaba, Hudaybiyah, n.k.
Rejea Qur’an (5:8), (42:40-42), (60:8).

Madhumuni ya Dola ya Kiislamu.
1.Kujenga maisha ya mwanaadamu yaliyo katika misingi ya (Tawhiid) Ucha-Mungu na matendo mema.
2.Kuondosha uovu, dhuluma, ukandamizaji, maasi, ukatili, tabaka, unyonyaji, uonevu, n.k katika jamii. Qur’an (57:25).
3.Kutumia mamlaka katika kusimamia na kuendeleza maadili katika maisha ya jamii. Qur’an (22:25).
4.Kusimamia na kulinda haki na uadilifu kwa wanaadamu wote na viumbe wengine.



                   

Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass

Nyuma Endelea


Je umeipenda post hii ?

Ndio            Hapana            Save post
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Sira Main: Dini File: Download PDF Views 1400

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉2 Madrasa kiganjani    👉3 kitabu cha Simulizi    👉4 Kitau cha Fiqh    👉5 Kitabu cha Afya    👉6 Simulizi za Hadithi Audio   

Post zinazofanana:

MTUME MUHAMMAD (S.A.W) AANALELEWA NA BABU YAKE MZEE ABDUL-ALMUTALIB AKIWA NA UMRI WA MIAKA SITA (6)

KULELEWA NA BABU YAKE:Mzee ‘Abdul Al-Muttalib alimchukuwa mjukuu wake na wakarejea Makkah na aliendelea kuishinae na kumlea kwa mapenzi makubwa sana.

Soma Zaidi...
Kujengwa upya al Kabah baada ya kuwa na mipasuko.

Sira na historia ya Mtume Muhammad s.a.w sehemu ya 18. Hapa utajifunza kuhusu tukio la kujengwa upya kwa al kaaba 🕋

Soma Zaidi...
Kuangamia kwa Mtoto na Mke wa Nuhu(a.s)

Tukirejea Qur’an (11:36-48) na (23:26 -29) tunapata maelezo juu ya mchakato wa kuangamizwa makafiri na kuokolewa waumini katika kaumu ya Nabii Nuhu(a.

Soma Zaidi...
Mfumo wa ulinzi na usalama katika fola ya uislamu madinah

Dola ya uislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Kulelewa kwa Mtume, maisha yake ya Utotoni na kunyonya kwake.

Historia na sura ya Mtume Muhammad S.A.W sehemu ya 06. Hapa utajifunza kuhusu historia ya Mtume akiwa mtoto.

Soma Zaidi...