Hatua na Mambo (Taasisi za Kisiasa) za msingi alizotumia Mtume (s.a.w) katika kuanzisha Dola ya Kiislamu Madinah

Kuanzishwa kwa Dola ya Kiislamu Madinah.

Hatua na Mambo (Taasisi za Kisiasa) za msingi alizotumia Mtume (s.a.w) katika kuanzisha Dola ya Kiislamu Madinah

Kuanzishwa kwa dola ya kiislamu Madina

Kuanzishwa kwa Dola ya Kiislamu Madinah.
- Kabla ya kufika Madinah, Mtume (s.a.w) akiwa mji wa Quba aliamuru msikiti ujengwe uliokuwa Ukiitwa 'Masjid Quba.'
Rejea Qur'an (9:108).
- Mtume alifika Madinah (Yathrib), Oktoba 622 A.D.
- Kwa heshima ya Mtume (s.a.w) Madinah ikapewa jina la Madinatun-Nabii (mji wa Mtume) na Al-Madinah Al-Munawwarah (mji ung'aao).


Hatua na Mambo (Taasisi za Kisiasa) za msingi alizotumia Mtume (s.a.w) katika kuanzisha Dola ya Kiislamu Madinah.

1.Kujenga Msikiti.
- Msikiti ulikuwa ndio Ikulu, mahakama, kituocha jeshi, ukumbi wa bunge (shura), n.k. Qur'an (3:95), (2:150).
- Ulikuwa kituo muhimu cha kiharakati katika kusimamisha na kuendeleza Uislamu. Rejea Qur'an (22:40), (2:114), (72:18) na (9:19).

2.Kujenga Ummah wa Kiislamu.
- Mtume (s.a.w) aliwapatanisha kabila la Aus na Khazraj Madinah waliokuwa na uadui wa muda mrefu baina yao. Qur'an (3:103).
- Mtume (s.a.w) pia aliwaunganisha udugu imara kati ya Muhajirina wa
- Makkah na Answaar wa Madinah na kuwa ummah mmoja. Qur'an (8:75).
- Pia aliimarisha uchumi kwa kuunganisha ummah wa Kiislamu na kuwa kitu kimoja. Qur'an (59:8-9).

3.Kuweka Mkataba wa Madinah (Madinah Charter).
- Mtume (s.a.w) alijieleza katika mkataba huo kuwa yeye ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na ndiye kiongozi mkuu wa Dola ya Kiislamu.
- Mkataba uliainisha vipengele vya amani na wajibu wa kila kundi kati ya makabila ya Mayahudi na Waarabu washirikina wa Madinah na Dola ya Kiislamu Madinah.
- Uliainisha nafasi, majukumu na wajibu wa waumini katika Dola.
- Mkataba uliainisha uhuru wa kila mtu kuabudu kwa mujibu wa imani na dini zao.

4.Kuweka Mikataba ya amani na Makabila ya Mayahudi na mengine yaliyokuwa pembezoni mwa Dola ya Kiislamu Madinah.
- Makabila na koo tatu za Kiyahudi zenye nguvu zilizokuwa pembezoni mwa mji wa Madinah yalikuwa;
?Banu Quraizah
?Banu Qainuqa na
?Banu Nadhir

5.Kuunda Shura na Sekretarieti.
- Mtume (s.a.w) aliteua washauri wake wakuu katika kuendesha Dola ambao Walikuwa Abu Bakr (r.a), Umar bin Khattab (r.a), Uthman bin Affan (r.a), Ally bin Abu Twalib (r.a) na Hamza bin Abdul-Muttalib (r.a).

- Aliteua waandishi maalumu wa kuandika na kutunza mikataba, takwimu, kumbukumbu na nyaraka zote za Dola ya Kiislamu Madinah.

6.Kuandaa Ummah wa Kiislamu Kijeshi na Kiusalama.
- Mtume (s.a.w) aliwaanda na kuwahimiza waislamu kuwa wakakamavu na hodari katika shabaha, mieleka na kutumia silaha.
- Kila Muislam alikuwa mpiganaji na mpelelezi dhidi ya maadui wa waislamu na Dola ya Kiislamu. Rejea Qur'an (4:71).
- Aliunda na kuweka vikosi vya doria na ulinzi kuzunguka mipaka ya Dola ya Kiislamu Madinah. Qur'an (8:26).

7.Kuimarisha Uchumi.
- Mtume (s.a.w) aliwahimiza waislam kufanya kazi kwa bidii ili kujiimarisha Kiuchumi na kuendeleza Dola.
- Utoaji wa Zaka, Sadaka na mapato mengine yalihimizwa na kukusanywa Kijamii na kuboresha huduma za jamii.
Rejea Qur'an (22:41).

Mafunzo yatokanayo na Kuanzishwa kwa Dola ya Kiislamu Madinah.
Kutokana na mambo ya msingi aliyoyafanya Mtume (s.a.w) katika kuanzisha Dola ya Kiislamu Madinah tunajifunza yafuatayo;

1.Hatunabudi kuanzisha na kuendesha vituo vya harakati, msikiti ukiwa ndio kitovu cha msingi.

2.Mshikamano, kuhurumiana na kupendana kwa vitendo baina ya waislamu ndio nyenzo pekee katika kuhuisha na kuendeleza harakati za Kiislamu.

3.Hatunabudi kuishi vizuri, kuwahesimu na kuwatendea haki, wasiokuwa waislamu hasa wale wasiopiga vita waislamu na Uislamu wazi wazi.

4.Ni wajibu kwa kila muislamu kuwa mkakamavu, jasiri na kujifunza mafunzo ya kijeshi na kuwa tayari kulinda na kuupigania Uislamu katika jamii.

5.Hatunabudi kuwajua vema maadui wa Uislamu na Waislamu, mbinu na silaha zao na kuchukua tahadhari dhidi yao.

6.Ni wajibu kuimarisha uchumi wetu kwani ndio nyenzo muhimu na ya msingi katika kuendesha harakati za Kiislamu.

7.Uongozi bora, makini na uwajibikaji wa kila mmoja kulingana nafasi yake ndio kiungo muhimu katika kuendesha harakati za Kiislamu.



                   

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 334

Post zifazofanana:-

WAJUE FANGASI, AINA ZAKE, DALILI ZAKE NA MATIBABU YAKE
Fangasi huweza kuishi na kuathiri maeneo mbalimbali ndani ya mwili. Soma Zaidi...

Mambo ya kuzingatia kabla ya kugawanya urithi
Soma Zaidi...

quran na sayansi
2; mbegu ya uhai uliyo changanyikaUmbile la mwanadamu limepitia hatua nyingi sana kama tutakavyoendelea mbele kuonalakini ukiachilia mbali na hatua zote alizopitia mwanadamu wakati wa kuumbwa lakiniumbile la mwanadamu bado limebakia kuwa dhalili kama ALLA Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula Nanasi
Soma Zaidi...

Dua sehemu 03
Zijuwe njia ambazo Allah hujibu Dua yako. Tambua kama umejibiwa dua yako au bodo, soma darsa za dua hapa. Soma Zaidi...

Hadithi ya kinyozi mwenyewe
Soma Zaidi...

Mapambano ya Dola ya kiislamu dhidi ya maadui wa kikristo (warumi) wakati wa Mtume
Soma Zaidi...

swala ya witri na namna ya kuiswali
3. Soma Zaidi...

HISTORIA YA NABII ADAM
Soma Zaidi...

More
Bila shaka umefurahishwa na huduma zetu, Je unataka huduma zaidi, Bofya kityfe cha Open hapo chini. Soma Zaidi...

COMMON CAUSES OF DIABETES
Diabetes is a disease that occurs when the body fails to produce insulin or body fail to produce sufficient insulin hormone or body failure to use insulin hormone. Soma Zaidi...

darasa la lishe
Jifunze mengi kuhusu afya na lishe, ujuwe utaratibu wa lishe Soma Zaidi...