Kupigwa vita Uislamu Tanganyika na Afrika Mashariki
Kupigwa vita Uislamu Tanganyika na Afrika Mashariki
i. Wamishionari wa kikristo waliona kuwa Uislamu ni kikwazo kwao, waliagiza machifu (viongozi wa kikabila) kuzuia Uislamu kuenea zaidi nje ya miji ya Pwani.
ii. Mkutano wa Berlin mwaka 1884, ulitoa kipaumbelea na fursa ya Ukristo kuwa na nguvu Afrika na kuweka mikakati ya kudhoofisha Uislamu na waislamu.
iii. Vyama vya Wamishionari, kikiwemo cha White Fathers chini ya Kardinali Lavingire, walianzisha mashule, vyuo na makanisa ilikueneza ukristo kupitia mbinu zifuatazo;
a. Kuficha uadui na uhasama wao dhidi ya waislamu na kujenga urafiki wa uongo na kinafiki.
b. Kujikita sana maeneo ya vijijini ndio ambapo waislamu wengi hawajui dini yao.
c. Kuanzisha makanisha na huduma za kijamii kama vile; mashule na hospitali.
iv. Wamishionari wa kikristo kupitia serikali za Kijerumani na Kiingereza, walianza mashule zilizotumia mfumo wa silabi zisizokuwa za kiarabu ili kudhoofisha utamaduni wa wenyeji wanaotumia silabi za kiarabu.
v. Wamishionari wa kikristo kutokana na ustawi wa waislamu walioukuta, walimshutumu Gavana Von Soden kuwapendelea waislamu, hivyo ikawekwa sera rasmi ya kuwabagua waislamu kielimu.
vi. Serikali ilinyima kabisa au kutoa misaada kidogo (grant in aid) shule zote za waislamu huku ikielekeza makanisani.
Mfano mwaka 1957 serikali ilitoa paundi 1,338,925 kwa mashirika yanayotoa elimu kati ya hizo, waislamu walipewa paundi 6,848 tu
vii. Masharti magumu au kupigwa marufuku waislamu kuanzisha shule zao katika misikiti (Qurโanic schools) na kutakiwa kuendesha kwa maelekezo ya serikali. viii. Serikali za kikoloni zikishirikiana na wamishionari, zilitaifisha mali zote za
waislamu ikiwemo; mashule, maduka, majumba, mashamba, n.k ili kuwadhoofisha kiuchumi kupitia sare ya ujamaa.
ix. Serikali iliwaua au kuwafunga au kuwahamisha viongozi waislamu makini ili kudhoofisha harakati zao juu ya Uislamu.kama akina Tewa Said Tewa, Suleiman Takadr, Bi Titi Mohamed, n.k.
x. Wamishionari kwa kushirikiana serikali, walianza sera ya dini mseto na taasisi za kimagharibi zinazoshughulikia miradi ya waislamu mfano; mradi wa kuritadisha waislamu wa โIslam in Africa Projectโ huko Nairobi.
xi. Serikali za kikoloni kwa kushirikiana na wamishionari na wenyeji wakristo, walitumia nguvu ya kuwateka na kuwaua machifu (viongozi waislamu wa kikabila) kama akina; Bushiri wa Pangani, Mkwawa wa Iringa, Isike wa Unyanyembe, Ali Songea Mbano, Suleiman Mamba, n.k ili kuvunja nguvu ya Uislamu.
xii. Chuki za serikali na mishionari dhidi ya machifu waislamu na waislamu, zilizidi na kuamua kupambana nao kivita kama vile vita vya maji maji, n.k.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
๐1 Simulizi za Hadithi Audio ๐2 Dua za Mitume na Manabii ๐3 Bongolite - Game zone - Play free game ๐4 Madrasa kiganjani ๐5 Kitau cha Fiqh ๐6 Kitabu cha Afya
Post zinazofanana:
HISTORIA YA MTUME ILYASA(A.S)
Mtume Ilyasa ni mmoja wa Mitume waliotumwa kupitia kizazi cha Bani Israil.
Soma Zaidi...Musa(a.s)Kupewa Utume Rasmi
Musa alipotimiza muda, alifunga safari na ahali zake kurejea Misri.
Soma Zaidi...Mafunzo yatokanayo na kuanzishwa kwa dola ya uislamu madinah
Dola ya uislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Nabii Salih(a.s)
Mafunzo tuyapatayo hayatofautiani na yale yatokanayo na Historia ya Nabii Hud(a.
Soma Zaidi...Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Nabii Musa(a.s) na Harun(a.s)
Kutokana na Historia ya Nabii Musa na Harun(a.
Soma Zaidi...