Kuchaguliwa kwa Makhalifa wanne baada ya kutawaf (kufariki) kwa Mtume muhammad (s.a.w)

8.

Kuchaguliwa kwa Makhalifa wanne baada ya kutawaf (kufariki) kwa Mtume muhammad (s.a.w)

HISTORIA YA UISLAMU BAADA YA KUTAWAFU MTUME (S.A.W) HADI LEO.

8.1. Ukuaji na Uendeshaji wa Dola ya Kiislamu Wakati wa Makhalifa Wanne Waongofu

Makhalifa wanne wa Mtume (s.a.w) waongofu walioendeleza Dola ya Kiislmu ni;

1. Abu Bakar Sswiddiq (r.a) kutoka mwaka 11 A.H ' 13 A.H.

2. Umar Ibn Khattab (r.a) kutoka mwaka 13 A.H ' 24 A.H.

3. Uthman bin Affan (r.a) kutoka mwaka 24 A.H ' 36 A.H

4. Ali bin Abu Twalib (r.a) kutoka mwaka 36 A.H ' 41 A.H



Uchaguzi wa Makhalifa wanne waongofu

1. Kuchaguliwa Abu Bakar Sswiddiq (r.a) kuwa Khalifa

- Mtume (s.a.w) mpaka anatawafu, hakuusia nani awe khalifa baada yake.

- Abu Bakar (r.a) alipendekezwa na Umar Ibn Khattab (r.a), na Answar wengi walikubali pendekezo hilo kutokana na sifa zifuatazo:
i. Sifa zilizopelekea Abu Bakar (r.a) kuchaguliwa kuwa kiongozi wa Dola ya Kiislamu ni pamoja na;

1. Ucha ' Mungu



2. Ujuzi wa kutosha wa Qur'an na Sunnah

3. Tabia njema

4. Siha (afya) nzuri



ii. Alisilimu akiwa mtu mzima na alikuwa karibu sana na Mtume (s.a.w)

kuliko sahaba yeyote yule.

Rejea Qur'an (9:40)



iii. Mtume (s.a.w) alimteua kuongoza swala kwa niaba yake alipokuwa mgonjwa.
iv. Alikuwa mwenye msimamo, maamuzi, ikhlas na uoni mpana kwa kufuata ipasavyo nyayo na mwenendo wa Mtume (s.a.w)



2. Kuchaguliwa Umar Ibn Khattab (r.a) kuwa Khalifa baada ya Abu Bakar (r.a)

- Abu Bakar (r.a) alipokaribia kutawafu aliitisha shura na kumpendekeza

Umar Ibn Khattab (r.a) kuwa Khalifa baada yake kutokana na sifa zake.

- Walikuwepo wajumbe wengi miongoni mwao ni pamoja na;

1. Umar Ibn Khattab (r.a) o Uthman bin Affan (r.a) o Ali bin Abi Twalib (r.a) o Zaid bin Thabit (r.a)
2. Abdul ' Rahman bin Auf (r.a)

3. Muadh bin Jabal

4. Ubay bin Ka'ab (r.a) na wengineo katika Muhajirina na Answaar.



- Baada ya shura, wajumbe wote walikubali pendekezo la Abu Bakar (r.a)

kuwa Umar bin Khattab (r.a) achukue nafasi ya kuongoza Dola ya Kiislamu.



3. Kuchaguliwa Uthman bin Affan (r.a) kuwa Khalifa

- Umar (r.a) alipendekekeza watu sita wenye sifa za kuongoza Dola ya

Kiislamu ambao ni;

1. Uthman bin Affan (r.a)

2. Ali bin Abu Twalib (r.a)

3. Saad bin Waqqas (r.a)

4. Talha (r.a)

5. Zubair bin Awwam (r.a) na

6. Abdul ' Rahman bin Auf (r.a)



- Siku ya tatu baada ya kutawafu Umar Ibn Khattab (r.a), Uthman bin Affan (r.a) alichaguliwa na jopo la masahaba baada ya Abdul ' Rahman bin Auf (r.a) na wengineo kujitoa.


- Siku ya nne, Uthman bin Affan (r.a) alitangazwa rasmi na kupewa bai'at

kuwa ndiye kiongozi wa Dola ya Kiislamu.



4. Kuchaguliwa Ali bin Abi Talib (r.a) kuwa Khalifa

- Baada ya miaka sita tu ya uongozi wa Ali bin Abi Talib (r.a), fitna ilizushwa na Myahudi aliyesilimu kwa uongo, Abdallah bin Sabaa.


- Waislamu waligawanyika makundi mawili, moja linakubaliana na uongozi wa Ali bin Abi Talib (r.a) na jingine kupingana nao.

- Sababu za kugawanyika ni kudai kuwa Khalifa Ali (r.a) halipizi kisasi kwa wauaji wa Uthman bin Affan (r.a), makundi hayo yalikuwa ni;

i. Wafuasi wa Uthman ' (Uthmanis);

- Wao walitaka Dola iwaadhibu wauaji wa Uthman bin Affan (r.a).



ii. Marafiki wa Ali ' (Shian ' Ali)

- Ndilo kundi la watu wa mji wa Kufa na Misr lililomuua Khalifa

Uthman (r.a)



iii. Mashibah

- Ni kundi la waislamu waliokwenda Jihad wakati Khalifa Uthman

(r.a) anauawa, hawakuwaunga mkono 'Uthmanis wala Shian ' Ali'



iv. Ahli ' Sunnah Wal- Jama'ah

- Lilikuwa ndilo kundi lenye masahaba wengi katika Dola yote ya

Kiislamu.

- Takriban uongozi wote wa Khalifa Ali (r.a) ulikumbwa na migogoro iliyopelekea kuuawa kwake.



                   

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 253

Post zifazofanana:-

Ukarimu na Sifa za kuwa Mkarimu na faida zake
30. Soma Zaidi...

HADITHI BYA KISIWA CHA MAWE YANAYOLIA
Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YAKISIWA CHA MAWE YANAYOLIA. Soma Zaidi...

FORM ONE BIOLOGY
Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet. Soma Zaidi...

DARSA ZA QURAN
Soma Zaidi...

Elimu
Uwanja wa elimu na maarifa Soma Zaidi...

Njia za kuzuia na kupunguza zinaa katika jamii
(ii) Hatua za Kuzuia Uzinzi JamiiUislamu pamoja na kutoa mafunzo ya maadii yanayomuwezesha mtu binafsi ajiepushe kwa hiari yake na kitendo kibaya cha zinaa, umechukua hatua mbali mbali ambazo huifanya zinaa isiwe kitendo chepesi katika jamii. Soma Zaidi...

HUKUMU YA NUN SAKINA NA TNWIN
Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa Soma Zaidi...

HISTORIA YA NABII YUSUFU(A.S.): Ndoto ya nabii Yusufu
Mtume Yusufu(a. Soma Zaidi...

Sababu Ya Uislamu Kuwa Ndiyo Dini Sahihi Pekee
1. Soma Zaidi...

HUDUMA YA KWANZA KWA MTU ANAYETOKWA NA DAMU YA PUA
Kama mtu anatokwa na damu za pua, basi juwa kuwa anahitaji huduma ya kwanza. Soma Zaidi...

More
Bila shaka umefurahishwa na huduma zetu, Je unataka huduma zaidi, Bofya kityfe cha Open hapo chini. Soma Zaidi...

dalili za mimba changa ndani ya wiki moja
Soma Zaidi...