vita vya ahzab, sababu ya kutokea vita hivi na mafunzo tunayoyapata
Vita vya Ahzab- Maquraish waliungana na mayahudi, wanafiki na makabila mengine ya waarabu baada ya kuona kuwa wao peke yao hawawezi kuufuta Uislamu.
vita vya ahzab, sababu ya kutokea vita hivi na mafunzo tunayoyapata
Vita vya Ahzab
- Maquraish waliungana na mayahudi, wanafiki na makabila mengine ya waarabu baada ya kuona kuwa wao peke yao hawawezi kuufuta Uislamu.
- Makafiri wakiwa 10,000 waliojizatiti kivita mwaka wa 5 A.H. kwa ajili ya kuivamia Madinah na waislamu wakiwa askari 3,000 tu na dhaifu kwa njaa.
- Waislamu kupitia rain a ushauri wa Salman Al-Farsy walibuni kuchimba handaki lenye upana yadi 5 na kina yadi 5 kuzunguka mji wa Madinah.
- Maadui walipozingira, walishindwa kuruka handaki na wakawa wamezingira mji wa Madinah kwa muda wa mwezi 1.
- Waislamu walipata dhiki kubwa ya njaa siku 3 na zaidi na huku wakiendelea kuchimba mtaro.
- Waislamu walishinda kwa kupata nusura kutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w) baada ya kuletwa mvua na upepo mkali uliowakimbiza maadui.
Rejea Qur’an (33:9-15), (33:25).
Mafunzo yatokanayo na vita vya Ahzab (Handaki).
1.Kushauriana katika kupanga mambo ni jambo la busara sana, kama alivyoshauriana Mtume (s.a.w) juu ya sehemu ya kupiganwa vita vya Uhudi.
Rejea Qur’an (3:159) na (3:166-167).
2.Tunajifunza pia ni wajibu waislamu kutumia mbinu, ujuzi, uzoefu, na jitihada za kivita pamoja na kuwa wanapata msaada wa Mwenyezi Mungu (s.w).
Rejea Qur’an (8:60).
3.Msamaha na nusura ya Mwenyezi Mungu (s.w) upo karibu kwa waislamu pindi watakapotubia na kurejea kwake na kupambana na maadui ipasavyo.
Rejea Qur’an (3:152-154), (3:166-167) na (3:139-141).
4.Ushindi wa waislamu katika vita unatoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w) na sio kutokana na ubora wa silaha na wingi wa askari.
Rejea Qur’an (3:123-124), (8:42-45).
5.Choko choko na mbinu za maadui dhidi ya Uislamu na waislamu ni zenye kuendelea na hazitaisha kamwe hadi siku ya Qiyama.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Madrasa kiganjani 👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉3 ai web app 👉4 Simulizi za Hadithi Audio 👉5 Kitabu cha Afya 👉6 Dua za Mitume na Manabii
Post zinazofanana:
Ukasha bin Mihsan ni Sahaba aliyechangamkia Fursa
Katika somo hili utakwnda kujifunz anamna nambavyo Sahaba Ukasha alivyochangamkia fursa katika mambo ya heri
Soma Zaidi...Kwanini mwanadamu hawezi kuunda dini sahihi
Dini anayostahiki kufuata mwanadamu (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...MTUME MUHAMMAD (S.A.W)ANAKUTANA NA BAHIRA (MTAWA WA KIYAHUDI)
KUKUTANA NA BAHIRA (MTAWA) WA KIYAHUDIMzee Abu talib alikuwa ni mfanya biashara, hivyoslikuwa akimchukuwa kijana wake kwenda kwenye biashara.
Soma Zaidi...Vitimbi vya Makafiri Dhidi ya Nabii Salih(a.s) na Waumini na kuangamizwa kwao
Makafiri wa Kithamud hawakuishia tu kwenye kuukataa ujumbe wa Nabii Salih(a.
Soma Zaidi...