image

Kuandaliwa Mtume (s.a.w) Kulingania Uislamu katika mji wa Makkah

7.

Kuandaliwa Mtume (s.a.w) Kulingania Uislamu katika mji wa Makkah

Kuandaliwa Mtume (s.a.w) Kulingania Uislamu katika mji wa Makkah

7.2Kuandaliwa Mtume (s.a.w) Kulingania Uislamu katika mji wa Makkah.
Nasaba ya Mtume (s.a.w).
- Mtume (s.a.w) alizaliwa siku ya kuamkia Jumatatu, tarehe 20 mwezi April, 570 A.D. sawa na mwezi 12 Rabi’ul-Awwal, mwaka wa tembo.

- Muhammad (s.a.w) alizaliwa katika kabila la Quraish, baba yake ni Abdullah bin Abdul-Muttalib, aliyefariki kabla ya kuzaliwa kwake.

- Mama yake Muhammad (s.a.w) ni Amina bint Wahhab, ambaye ni miongoni mwa koo za Kiqureish pia.

- Uzaliwa wa Muhammad (s.a.w) una nasaba na kizazi cha Nabii Ismail (a.s), alipozaliwa alipewa jina la ‘Muhammad’ au ‘Ahmad’ lenye maana ya mwenye kusifiwa kwa vitendo vizuri.



Malezi ya Mtume (s.a.w).
- Muhammad (s.a.w) baada ya kuzaliwa, alinyonyeshwa na kulelewa na Bibi Halimah bint Dhayb kutoka mji wa Taif, kutokana na hali ya hewa safi ya huko mpaka alipofikia umri wa miaka miwili.

- Muhammad (s.a.w) alirejeshwa Makka na alikaa na mama yake muda wa miaka 6 naye alifariki 576 A.D. hapo akawa chini ya malezi ya babu yake Abdul-Muttalib aliyefariki mwaka 578 A.D. Muhammad (s.a.w) akiwa na miaka 8.

- Baada ya kufariki babu yake, Muhammad (s.a.w) akawa chini ya malezi ya ami (baba mdogo) yake Abu Talib mpaka alipopata Utume.




Kuandaliwa Muhammad (s.a.w) kabla ya kupewa Utume.
- Maandalizi (mafunzo) haya yalikuwa ya Kiil-hamu ambayo hata Muhammad mwenyewe na jamii haikujua kuwa anaandaliwa, na yalikuwa kama ifuatavyo;

i.Kuzaliwa katika kabila tukufu la Kiqureish ambalo ni kizazi cha Nabii Ibrahim (a.s) kupitia kwa Nabii Ismail (a.s).
Rejea Qur’an (2:129).

ii.Kupewa jina la Muhammad na babu yake lililo na maana sawa na ‘Ahmad’- Mshukuriwa, alilotabiriwa nalo katika Injili, na Qur’an pia.
Rejea Qur’an (61:6).

iii.Malezi bora aliyopata kupitia Mama yake mzazi, Bi Halimah, babu yake Abdul-Muttalibu na Ami ya Abu Talibu pamoja na kuwa alikuwa yatima.
Rejea Qur’an (93:6).

iv.Tabia yake njema isiyo na mfano kuanzia utotoni hadi utuuzima wake kutoathiriwa na kila aina ya ubaya.
Rejea Qur’an (68:4).

v.Ndoa yake Muhammad (s.a.w) na Bi Khadija bint Khuwailid, aliiandaa Allah (s.w) ili kumuwezesha Muhammad kuitumikia jamii hata kabla ya utume.
Rejea Qur’an (93:8).

vi.Kuchukia kwake maovu na kujitenga pangoni ili kutafuta msaada ulio nje ya uwezo wa kinaadamu baada ya kufanya jitihada mwisho wa uwezo wake.
Rejea Qur’an (93:7) na (94:1-3).



Mafunzo yatokanayo na maandalizi haya ya Ki-Ilhamu
i.Hatuna budi kuwaandaa watoto wetu kuwa Makhalifah (viongozi) wa Allah (s.w) hata kabla hawajazaliwa.

ii.Hatuna budi kuwaandaa walimu (madai’yah) watakaoufundisha Uislamu na taaluma zingine kwa lengo la kuusimamisha Uislamu katika jamii.

iii.Hatuna budi kushirikisha familia zetu kwenye harakati za kuuhuisha na kuusimamisha Uislamu katika jamii.

iv.Wanawake wa Kiislamu hawanabudi kumuiga Bi Khadija, mkewe Mtume (s.a.w) katika kuwasaidia waume zao katika harakati za kuupigania Uislamu.

v.Pia hatuna budi kuchukia kila aina ya uovu na dhuluma unaofanywa katika jamii, na tujitahidi kuyaondoa kwa mikono na kauli zetu kabla ya kujitenga.

vi.Hatuna budi pia kujipamba na kila tabia na mwenendo mwema kwa kadri ya uwezo wetu.

vii.Pia hatuna budi kujiimarisha kiuchumi kwani ndio ni katika nyenzo kuu za kuweza kuusimamisha na kuuendeleza Uislamu katika jamii.



Kuandaliwa Muhammad (s.a.w) wakati na baada ya kupewa Utume.
- Maandalizi haya yalikuwa ya kimafunzo (maelekezo) yaliyotokana na wahay moja kwa moja ulipokuwa unamshukia, ulianza katika sura tatu zifuatazo;



Suratul-A’laq (96:1-5).
- Huu ulikuwa wahay wa kwanza kabisa kumshukia Muhammad (s.a.w)
kama ifuatavyo;


“Soma kwa jina la Mola wako aliyeumba, Amemuumba mwanaadamu kwa Alaq (pande la damu). Soma, na Mola wako ni Karimu sana. Ambaye amemfundisha (elimu zote) kwa msaada wa kalamu. Amemfundisha mwanaadamu (chungu ya) mambo aliyokuwa hayajui.”


Suratul-Muzzammil (73:1-10).
- Huu ulikuwa wahay wa pili kumshukia Mtume (s.a.w) kama ifuatavyo;
“Ewe uliyejifunika maguo! Simama usiku (kucha kufanya ibada), ila muda mdogo (tu hivi) nusu yake au ipunguze kidogo au izidishe na soma Qur’an vilivyo. Hakika sisi tutakuteremshia kauli nzito. Hakika kuamka usiku (na kufanya ibada) kunawafikiana zaidi na moyo, na maneno (yake) yanatua zaidi. Hakika mchana una shughuli nyingi. Na litaje jina la Mola wako na ujitupe kwake kwa kweli. (Yeye ndiye) Mola wa mashariki na magharibi, hakuna muabudiwa wa haki ila Yeye, basi mfanye kuwa mlinzi (wako). Na subiri juu ya hayo wasemayo (hao makafiri) na uwaepuke mwepuko mwema.”



Suratul-Muddaththir (74:1-7).
- Huu ulikuwa ni wahay wa tatu kumshukia Mtume (s.a.w) kama
ifuatavyo;


“Ewe uliojifunika maguo. Simama na uonye (watu) na Mola wako umtukuze. Na nguo zako uzisafishe (uzitwaharishe). Na mabaya yapuuze. Wala usiwafanyie watu ihsani (viumbe) ili upate kujikithirisha. Na kwa ajili ya Mola wako fanya subira.”



Mafunzo yatokanayo na Maandalizi ya Mtume (s.a.w) Kimafunzo
(Ki-wahay).
i.Elimu katika fani zote (isipokuwa uchawi) ndio nyenzo kuu katika maandalizi kuusimasha Uislamu katika jamii.



ii.Kisimamo cha usiku kufanya ibada, ni katika nyenzo kuu ya pili katika maandalizi ya kusimamisha Uislamu katika jamii.



iii.Kusoma Qur’an kwa mazingatio kwa lengo la kuifanya muongozo pekee wa maisha pia ni maandalizi ya kuutawalisha Uislamu katika jamii.



iv.Kumtaja na kumtukuza Allah (s.w) vilivyo, pia ni katika nyenzo na maandalizi katika kuusimamisha Uislamu ndani ya jamii.



v.Kujitupa kwa Allah (s.w) kwa kweli – ni kumcha Allah (s.w) peke yake ukweli wa kumcha, nayo ni katika maandalizi ya kusimamisha Uislamu.
Rejea Qur’an (3:102).



vi.Kumfanya Allah (s.w) ndiye mlinzi pekee na kumtegemea, ni jambo la muhimu katika kusimamisha Uislamu katika jamii.



vii.Kusimama na kuonya (kulingania Uislamu), ni jambo muhimu sana linalowezesha Uislamu kufahamika kwa watu.



viii.Kutakasa (kutwaharisha) nguo ni amri ya Allah (s.w) inayomtaka kila mlinganiaji wa Uislamu kuwa safi wa kuigwa kimwili na kiroho pia.
Rejea Qur’an (41:33).



ix.Kupuuza na kujitenga na mabaya na wabaya ni jambo la muhimu ili kukataza kwake maovu kuwe na athari.



x.Kufanya ihsani (wema) kwa ajili tu kwa ajili ya kutafuta radhi za Allah (s.w) ndio uhai wa ibada ya muislamu.



xi.Kufanya subira kwa ajili ya Allah (s.w) ni katika nyenzo kuu katika kupelekea kuusimamisha Uislamu katika jamii.



xii.Utekelezaji wa ujumbe wa Qur’an ni kazi nzito na yenye kila aina ya misukosuko, hivyo kuwa na subira ndio nyenzo pekee.





                   





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Sira Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 658


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Simulizi za Hadithi Audio     👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉6 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

NI IPI FAMILIA YA MTUME MUHAMMAD (S.A.W) NA NI IPI NASABA YAKE, UKOO WAKE NA KABILA LAKE
FAMILIA YA MTUME (S. Soma Zaidi...

Imam Bukhari na Sahihul Bukhari
Soma Zaidi...

Kibri cha Ibilis na Uadui Wake Dhidi ya Binadamu
Ibilis ni katika jamii ya majini aliyekuwa pamoja na Malaika wakati amri ya kumsujudia Adam inatolewa. Soma Zaidi...

HISTORIA YA NABII AYYUUB(A.S)
Ayyuub(a. Soma Zaidi...

Nasaha za Lut(a.s) kwa Watu Wake
Nabii Lut(a. Soma Zaidi...

Historia ya bi Khadija na familia yake na chanzo cha utajiri wake.
Sira na historia ya Mtume Muhammad s.a.w, sehemu ya 17. Historia ya Bi Khadija na familia yake. Soma Zaidi...

Imam Tirmidh na Jami'u At-Tirmidh
Soma Zaidi...

HISTORIA YA BANI ISRAIL
Nabii Musa na Harun walikuwa na kazi kubwa mbili; kwanza, kuwakomboa Bani Israil kutokana na dhuluma waliyokuwa wakifanyiwa na Firaun na Serikali yake, na pili, kuwarudisha kwenye nchi yao takatifu ya Palestina. Soma Zaidi...

NAMNA MTUME(S.A.W) ALIVYOSIMAMISHA DOLA YA KIISLAMU MADINAH
Safari ya Mtume(s. Soma Zaidi...

Nabii Ibrahiim(a.s) Afanywa Kiongozi wa Harakati za Uislamu Ulimwenguni
“Na (kumbukeni habari hii) Mola wake alipomfanyia mtihani (Nabii) Ibrahiim kwa amri nyingi; naye akazitimiza. Soma Zaidi...

Harun(a.s), Achaguliwa Kuwa Msaidizi Musa(a.s) na kumkabili (kumlingania) firauni
Nabii Musa(a. Soma Zaidi...

Kuchimbwa upya kwa kisima cha Zamzam
Sura na historia ya mtume Muhammad S.A.W sehemu ya 3.Hapa utajifunza kuhusu kufukuliwa kwa kisima cha Zamzam baada ya kufukiwa muda mrefu. Soma Zaidi...