Katika somo hili utakwenda kujifunza kanuni za usomaji wa isti’adha na basmallah.
Tamko la "Bismillahir-Rahmanir-Rahim" hujulikana kama Basmala, na "A'udhu Billahi Minash-Shaytanir-Rajim" hujulikana kama Isti'adha. Matamko yote haya yana hukumu zake za usomaji mbele ya maulamaa wa Tajwid. Allah amesema: "...pindi unaposoma Qur'an, tafuta hifadhi kwa Allah kutokana na Shetani aliye mbali na rehema za Allah" (yaani, anza kusoma kwa Isti'adha).
Pindi utakapoanza kusoma Qur'an na ukataka kuanza na Isti'adha mwanzoni mwa sura, unatakiwa kuleta Basmala kabla ya kuanza sura. Hivyo basi, kutakuwa kumekutana Isti'adha, Basmala, na sura unayotaka kusoma. Hapa katika kusoma kwake kuna hukumu nne kama ifuatavyo:
Kukata zote: Kusoma kila moja kivyake kwa kusimama kati ya vitatu hivi. Yaani, utasoma Isti'adha kisha utasimama, halafu utasoma Basmala kisha utasimama na baadaye utaanza sura.
Kuunga zote: Kunganisha Isti'adha, Basmala, na sura bila kusimama.
Kuunga Basmala na sura: Kusoma Isti'adha kisha utasimama, halafu utasoma Basmala na sura kwa kuunganisha bila kusimama.
Kuunga Isti'adha na Basmala: Kusoma Isti'adha na Basmala kwa pamoja kisha unasimama, kisha unasoma sura.
Inapotokea umemaliza sura moja na unataka kuingia sura nyingine, hapa kuna hukumu zifuatazo:
Kukata zote: Kusoma mwisho wa sura, kisha unasoma Basmala, na kisha unasoma sura inayofuata.
Kuunga zote: Kuunganisha mwisho wa sura kisha unasoma Basmala, kisha unaanza kusoma sura mpya bila kupumzika.
Kuunga Basmala na mwanzo wa sura: Kumaliza sura kisha utasimama, kisha utasoma Basmala pamoja na kuanza sura mpya bila kusimama.
Mwisho:
Katika somo linalofuata tutakwend akujifunza hukumu za NUN sakina na tanwinkatika usomaji wa Quran.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu hukumu za kitajwid za nun sakina na tanwin
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu herufi saba katika usomaji wa tajwid.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu makharijal khuruf
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu hukumu idgham na idhhar katika laam.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu hukumu za Qalaqala katika usomaji wa tajwid.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu hukumu za tafkhim na tarqiq
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu madd na aina zake. Utajifunza herufi za madd na umuhimu wa madd katika tajwid.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwend akujifunza kuhusu umuhimu wa kusoma elimu ya tajwid.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwend akujifunza kuhusu sijda zinazotokea wakati wa kusoma Quran.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu hukumu za idhhar na mifano yake.
Soma Zaidi...