picha

Tajwid somo la 20: hukumu za madd twab'iy yaani madd ya asili

Katika somo hili utakwend akujifunza kw akirefu kuhusu madd twab’iy yaani madd za asili.

Maddu-twabiy’y


Hii ni madd ya asili ambayo madd zote zimepatikana kutoka hapa. Maddd hii ni ya haraka 2 na haijuzu kuzipunguza wala kuzizidisha na ni makosa kufanya vinginevyo. Madd hii itavutwa katika hali zote ima katika hali ya kuunganisha maneno au katika hali ya kusimama. Ili itokee madd hii haihitaji sababu zingine ila ni asili ya neno tu ni lazima liwe na madd hiyo.


Halikadhalika madd hii kuna maeneo saba ambayo haipatikani wakati wa kuunga maneno ila itapatikana tu pale msomaji anaposimama. Na sehemu hizi zipo saba tu na zinapatikana kwa kuwepo alif na hii huitwa jina la الْفات السبع (Alifaatus-Sab-‘iy - Alif Saba).


(maddutw-twabiy’iy) nyinginezo ni:
مَدُّ الصِّلَّةِ الصُّغْرى . 1 - Maddusw-Swillatis-Sughraa
2 مَدُّ الْعِوَضِ . - Maddul-‘Iwadhw
مَدُّ الْبَدَل . 3 – Maddul-Badl
مَدُّ التَّمْكِين . 4 – Maddut-Tamkiyn
ألِفَات حَيُّ طَهْر . 5 – Alifaatu Hayyun Twahr

1 Maddusw-Swillatis-Sughraa:
Swillah ni kuunganisha herufi ya ه (haa) ya kiwakilishi1 na herufi ya madd yenye kunasibiyana na i’raab yake (dhwammah au kasrah) kitakapokuwa hicho kiwakilishi cha ه ni chenye i’raab na kipo baina ya herufi mbili zenye i’raab. Swillah hii imegawanyika sehemu mbili mojawapo ni hii ya assughraa (ndogo) na ya pili yake ni ya al-kubraa (kubwa) itakayokuja maelezo yake katika Maddul-Far-’iy.

 

Shart zake:
i) Kuweko na i’raab (sio sukuwn au herufi ya madd) kabla ya ه (haa)
ii) Kuweko na i’raab ifuatie katika neno la pili.
iii) Haifuatwi na hamzah.





Hukumu hii haizingatiwi katika maeneo mawili kwenye qurani. Aya hizi moja wapo huvutwa (Al-Furqaan (25: 69) ) ijapokuwa haina sifa za kuvutwa na nyingine haivutwi (Az-Zumar (39 : 7)) ijapokuwa ina sifa za kuvutwa. Na hii ni kutokana kuwa hivyo ndivyo inavyosomwa. Maeneo hayo ni haya;-


(Az-Zumar (39 : 7) Al-Furqaan (25: 69)

2 Maddul-Badal
Kanuni ya badal: ni kuja kwa hamzah mbili zenye kufuatana moja baada ya nyengine, ya kwanza ikawa na i’raab na ya pili ikawa saakin katika neno moja, hivyo hubadilishwa hamzah ya pili saakinah na kuwa herufi ya madd yenye kuwiana na i’raab ya hamzah ya kwanza. Hukmu yake ni kuvutwa harakah mbili.



3. Maddul-‘Iwadhw
Ni madd inayotokea wakati wa kusimama msomaji katika neno lenye fathataan (tanwiyn fat-hah). Hukmu yake ni huvutwa kwa harakah mbili. Kusimama kwenye ة (taa marbuwtwah ya kike iliyofungwa) kunapelekea kutokuwepo hukmu hii ya مَدُّ الْعِوَض (maddul-‘iwadhw) kwani wakati huo huondoka tanwiyn na kusimamiwa kwa ه (haa) saakinah.

4.Maddut-Tamkiyn
Ni madd inayotokea wakati ي mbili zimekutana, ya kwanza ina shaddah na kasrah na ya pili ina sukuwn. Imeitwa tamkin مَدُّ التَّمْكِين kwa sababu inatamkwa ikiwa imethibitika kwa sababu ya shaddah. ي ya pili ambayo ina sukuwn inavutwa kwa harakah mbili.



5 - Alifaatu-Hayyin-Twahur
Ni مَدُ الطَّبِيعي (maddutw-twabiy’iy) inayotokana katika kutamkwa baadhi ya الحروف المتقاطعة (Al-Huruwf Al-Mutaqatw-twa’ah)1 zinazoanzia baadhi ya
Suwrah, kwa vile herufi hizo zinatamkwa kama herufi za hijaaiyah طا حا
ها را . Nazo zimeundwa katika ibara ya حيّ طهر (hayyun twahur) kwa jina
jingine huitwa ألِفَاتُ حَيٍّ طَهُ ر (Alifaatu hayyin twahur).



Mwisho:

Katika somo linalofuata tutakwenda kujifunza kuhsu madd Fr’iy katika usmaji wa tajwid.

 

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-07-14 Topic: Darsa za Tajwid Main: Dini File: Download PDF Views 854

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Dua za Mitume na Manabii    👉2 Madrasa kiganjani    👉3 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    👉4 ai web app    👉5 Kitabu cha Afya    👉6 kitabu cha Simulizi   

Post zinazofanana:

Tajwid somo la 7: haraka na irabu katika lugha ya kiarabu

Katika somo hili utakwenda kujifunzakuhusu haraka na irabu katika lugha ya kiarabu

Soma Zaidi...
Tajwid somo la 21: hukumu za madd far’iy

Katika somo hili utakwend akujifunz akuhusu madd far’iy katika usomaji wa Quran tajwid.

Soma Zaidi...
Tajwid somo la 6: sifat al khuruf

hapa utakwenda kujifunza kuhusu sifa za herufi za kiarabu

Soma Zaidi...
Tajwid somo la 2: herufi saba katikausomaji wa quran

Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu herufi saba katika usomaji wa tajwid.

Soma Zaidi...
Tajwid somo la 5: makharija al khuruf

Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu makharijal khuruf

Soma Zaidi...
Tajwid somo la 15: hukumu za qalqala

Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu hukumu za Qalaqala katika usomaji wa tajwid.

Soma Zaidi...
Tajwid somo la 11: hukumu ya idgham

Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu hukumu za idgham katika tajwid

Soma Zaidi...
Tajwid somo la 19: hukumu za madd na aina zake

Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu madd na aina zake. Utajifunza herufi za madd na umuhimu wa madd katika tajwid.

Soma Zaidi...
Tajwid somo la 1: Maana ya elimu ya Tajwid na kanuni zake

Katika somo hili utakwend akujifunza maana ya elimu ya tajwid kisheria. Pia utajifunza hukumu ya kusoma tajwid.

Soma Zaidi...
Tajwid somo la 13: sheria za Al-ikhfaa

Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu hukumu za Al ikhfaa katika usomaji wa Tajwid

Soma Zaidi...