Tajwid somo la 1: Maana ya elimu ya Tajwid na kanuni zake

Tajwid somo la 1: Maana ya elimu ya Tajwid na kanuni zake

Katika somo hili utakwend akujifunza maana ya elimu ya tajwid kisheria. Pia utajifunza hukumu ya kusoma tajwid.

Maana ya Elimu ya Tajwid

Neno "Tajwid" linatokana na neno la Kiarabu جَوَّدَ (jawwada) ambalo kilugha lina maana ya "ufundi," yaani kufanya kitu kwa uhodari au ustadi. Kwa mujibu wa Kishariah, maana ya Tajwid ni kuitamka kila herufi kama inavyotakiwa kutamkwa, kwa kuipa haki yake na sifa zake huku ukifuata hukumu zote za Tajwid.

 

Katika Qur'an na Sunnah, imehimizwa sana kusoma Qur'an kwa tajwid au tartila. Elimu hii ya Tajwid ilianza zamani toka enzi za masahaba na wakati Mtume Muhammad (s.a.w) akiwa hai. Mtume alikuwa akiwaelekeza masahaba kwa watu maalumu ili wapate kujifunza Qur'an kwa ufasaha. Imepokewa kuwa Mtume (s.a.w) amesema: "Mwenye kupenda kuisoma Qur'an kama vile ilivyoteremshwa basi na asome kwa Qiraa-ah (kisomo) cha ibn Ummi ‘Abd" (imepokelewa na Ibn Majah na Ahmad).

 

Pia, Allah amesema: "وَرَتِّلِ ٱلْقُرْءَانَ تَرْتِيلًا" ("na soma Qur'an kwa tartila" - kisomo cha utaratibu upasao). Katika kuonesha maana ya neno tartila, 'Aliy Ibn Abi Talib ambaye ni khalifa wa nne baada ya kufariki Mtume amesema: "التَّرتيلُ هُوَ تَجويد الحُروفَ ومَعرِفةِ الوقوفِ" ("Ni kuisoma Qur'an kwa ujuzi wa kutamka herufi ipasavyo na kuwa na ujuzi wa hukumu za kusimama").

Kanuni Zinazofungamana na Elimu ya Tajwid

  1. Ujuzi wa kujua matamshi ya herufi na yanapopotamkiwa na yanavyotamkwa.

  2. Ujuzi wa kujua tabia na sifa za herufi.

  3. Ujuzi wa kujua namna ambavyo herufi zinabadilika kulingana na mpangilio wa maneno.

  4. Kufanya mazoezi ya ulimi pamoja na kurudia rudia.

 

Hukumu ya Kujifunza Tajwid

Kusoma Qur'an bila ya Tajwid, yaani kuchunga herufi ipasavyo, ni katika makosa mbele ya maulamaa wa Tajwid. Maulamaa wa elimu hii wanasema kuwa kujifunza Tajwid ni faradhi kifaya (faradhi ya kutoshelezana) kwa kauli za walio wengi. Pia, wapo wanaosema ni faradhi 'ayn (faradhi ya lazima) kwa kila Mwislamu.

Hawa waliosema ni faradhi kifaya wanamaanisha sio faradhi ya lazima kwa wote ila inatosha kwa wachache wakiwa na elimu hii. Kundi hili pia linasema kuwa inapasa kwa msomaji asisome kwa kukosea ijapokuwa hajui hukumu za Tajwid. Yaani, achunge matamshi kama yalivyoandikwa ili asije akatamka vinginevyo na kubadilisha maana.

 

Mwisho:

Tukutane somo linalofuata utakwenda kujifunza kuhusu herufi saba katika usomaji wa tajwid.

 

Zoezi la Maswali

Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-07-14 16:13:43 Topic: Darsa za Tajwid Main: Masomo File: Download PDF Views: 1688

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     👉3 Dua za Mitume na Manabii     👉4 Kitau cha Fiqh     👉5 kitabu cha Simulizi     👉6 Bongolite - Game zone - Play free game    

Post zinazofanana:

Tajwid somo la 14: kuhumu za mim sakina

Katika somo hili utakwend akujifunza kuhusu hukumu za ki tajwid za mim sakina.

Soma Zaidi...
Tajwid somo la 22: hukumu za sijdat tilawa

Katika somo hili utakwend akujifunza kuhusu sijda zinazotokea wakati wa kusoma Quran.

Soma Zaidi...
Tajwid somo la 5: makharija al khuruf

Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu makharijal khuruf

Soma Zaidi...
Tajwid somo la 8: hukumu za kusoma basmala na isti'adha

Katika somo hili utakwenda kujifunza kanuni za usomaji wa isti’adha na basmallah.

Soma Zaidi...
Tajwid somo la 10: hukumu ya idhhar

Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu hukumu za idhhar na mifano yake.

Soma Zaidi...
Tajwid somo la 17: hukumu za idgham na idhhar katika laam.

Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu hukumu idgham na idhhar katika laam.

Soma Zaidi...