Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu hukumu za kitajwid za nun sakina na tanwin
Nuwn saakinah ni herufi ya nuwn (نْ) isiyokuwa na i’raab ambayo huthibiti katika kutamkwa, kuandikwa, kusimama, na katika kuunganisha. Tanwin hapa tunazungumzia hasa fatahateni, kasrteni na dhuma ten endapo zitakutana ha herufi nini kifanyike.
Wataalamu wa Tajwid wameeleza hukumu nne pindi nuwn sakina au tanwin zinapokutana na herufi. Hukumu hizo ni:
Maana: Kudhirisha kitu wazi. Katika hukumu za Tajwid, ni kuitoa kila herufi katika makhraj yake bila ya kuwepo ghunnah. Hii hutokea pale nuwn saakinah au tanwin inapofuatiwa na mojawapo wa herufi sita za al-halq (koo) ambazo ni ء, ه, ح, خ, ع, غ.
Maana: Kuingiza kitu kwenye kitu. Katika hukumu za Tajwid, ni kuingiza herufi saakin kwenye herufi yenye i’raab na kuzipelekea herufi mbili hizi kuwa herufi moja ya pili nzito. Hii hutokea pale nuwn saakinah au tanwin inapofuatiwa na mojawapo ya herufi sita za idgham ambazo ni ي, ر, م, ل, ن, و.
Idghaam inafanyika kwenye maneno mawili tu. Herufi ya mwisho ya neno la kwanza iwe na tanwin au nuwn saakinah na herufi ya kwanza ya neno linalofuata iwe ni mojawapo ya herufi za idgham.
Idgham Bighunnah: Kuingiza nuwn saakinah au tanwin kwenye herufi za ي, ن, م, و pamoja na kuleta ghunnah inayotokea puani.
Idgham Bighayri Ghunnah: Kuingiza nuwn saakinah au tanwin kwenye herufi za ر, ل bila ya ghunnah.
Maana: Kugeuza kitu na kukifanya kuwa kitu kingine. Katika hukumu za Tajwid, ni kuigeuza nuwn saakinah au tanwin kwa kuitamka kama miym (م) pamoja na ghunnah. Hii hutokea pale tu nuwn saakinah au tanwin inapokutana na ب (baa).
"أنبئهم" (anbi'uhum)
Maana: Kuficha kitu. Katika hukumu za Tajwid, ni kuificha nuwn saakinah au tanwin katika herufi za ikhfaa. Hivyo nuwn saakinah au tanwin itatamkwa ikiwa baina ya idh'har na idgham kwa kuipa ghunnah isiyokuwa na shaddah. Herufi za ikhfaa ni: ث, ج, د, ذ, ز, س, ش, ص, ض, ط, ظ, ف, ق, ك.
"من تفعل" (min taf'al)
Katika somo linalofuata tutakwenda kujifunza zaidikuhusu idhhar na kuona mifano zaidi.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu hukumu za Al ikhfaa katika usomaji wa Tajwid
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu hukumu za Qalaqala katika usomaji wa tajwid.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunzakuhusu haraka na irabu katika lugha ya kiarabu
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza kanuni za usomaji wa isti’adha na basmallah.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwend akujifunz akuhusu hukumuza waqfu katika usomajiwa quran.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu hukumu za tafkhim na tarqiq
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu madd na aina zake. Utajifunza herufi za madd na umuhimu wa madd katika tajwid.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwend akujifunza kuhusu sijda zinazotokea wakati wa kusoma Quran.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwend akujifunza maana ya elimu ya tajwid kisheria. Pia utajifunza hukumu ya kusoma tajwid.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwend akujifunza kuhusu umuhimu wa kusoma elimu ya tajwid.
Soma Zaidi...