Tajwid somo la 4: umuhimu wa kusoma Tajwid

Tajwid somo la 4: umuhimu wa kusoma Tajwid

Katika somo hili utakwend akujifunza kuhusu umuhimu wa kusoma elimu ya tajwid.

Fadhila na Umuhimu wa Tajwid

Elimu ya Tajwid ina umuhimu mkubwa katika umma wa Kiislamu. Msomaji wa Qur'an kama hatachunga kisomo anaweza kubadilisha maana ya Qur'an kabisa. Hivyo, elimu ya Tajwid ni msingi wa kuchunga maana ya matamshi ya Qur'an katika usomaji.

 

Tunahitajia imamu mwenye kiraa nzuri kwa sauti pia awe anajua Tajwid na anaitumia ipasavyo. Mtume (s.a.w) amesema: "Kutoka kwa Abu Mas’uud Al-Answaariyy (r.a) amesema: Mtume (s.a.w) amesema: 'Awaswalishe watu yule mwenye kujua Kitabu cha Allah na wakiwa katika kusoma wako sawa, basi mwenye ujuzi zaidi wa Sunnah, na wakiwa kwenye Sunnah wako sawa, basi aliyetangulia Hijra, na wakiwa katika Hijra wako sawa, basi mkubwa wao kwa umri, wala asiswalishe mtu (mwengine) katika nyumba yake wala katika mamlaka yake wala asikae mahali pake pa heshima isipokuwa kwa idhini yake.'"

 

Watu hupenda kusikiliza kiraa cha mtu anayesoma vizuri kwa sauti na kuchunga hukumu za Tajwid. Mtume (s.a.w) amesema: "Kutoka kwa Abu Musa Al-’Ash’ariyy (r.a) kwamba Mtume kamwambia: 'Ungeliniona jana nilivyokuwa nakusikiliza kisomo chako. Hakika umepewa mizumari miongoni mwa mizumari ya aila ya Daud.'"

 

Msomaji wa Qur'an atakuwa pamoja na malaika wema wenye kuandika. 'Aaishah (r.a) amesema: Mtume (s.a.w) amesema: "Yule aliyekuwa hodari wa kusoma Qur'an atakuwa pamoja na Malaika Waandishi (wa Allah) watukufu wema, na yule ambaye anaisoma Qur'an kwa mashaka na huku anajitahidi kwa kudodosa atapata ujira mara mbili."

 

Mwisho:

Katika somo linalofuata utakwenda kujifunza kuhusu makharija al khuruf katika herufi za kiarabu

 

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-07-14 17:04:45 Topic: Darsa za Tajwid Main: Masomo File: Download PDF Views: 1001

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Simulizi za Hadithi Audio     👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉5 kitabu cha Simulizi     👉6 web hosting    

Post zinazofanana:

Tajwid somo la 14: kuhumu za mim sakina

Katika somo hili utakwend akujifunza kuhusu hukumu za ki tajwid za mim sakina.

Soma Zaidi...
Tajwid somo la 11: hukumu ya idgham

Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu hukumu za idgham katika tajwid

Soma Zaidi...
Tajwid somo la 18: hukumu za waqf wal ibtidai

Katika somo hili utakwend akujifunz akuhusu hukumuza waqfu katika usomajiwa quran.

Soma Zaidi...
Tajwid somo la 6: sifat al khuruf

hapa utakwenda kujifunza kuhusu sifa za herufi za kiarabu

Soma Zaidi...
Tajwid somo la 9: hukumu za nun sakina na tanwin

Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu hukumu za kitajwid za nun sakina na tanwin

Soma Zaidi...
Tajwid somo la 20: hukumu za madd twab'iy yaani madd ya asili

Katika somo hili utakwend akujifunza kw akirefu kuhusu madd twab’iy yaani madd za asili.

Soma Zaidi...