Navigation Menu



image

Tajwid somo la 21: hukumu za madd far’iy

Katika somo hili utakwend akujifunz akuhusu madd far’iy katika usomaji wa Quran tajwid.

MADD (Al-Maddul-Far-’iy)

Al-Maddul-Far-’iy
الْمَدُّ الْفَرْعي - Al-Maddul-Far-’iy
Madd ambayo hutegemea sababu nyengine ima iwe hamzah au sukuwn ili iweze kurefushwa kuvutwa kwake kuishinda مَدُ الطَّبِيعي (maddutw-twabiy’iy) na hiyo sababu ya nje. Imeitwa ‘Al-Far-iy’ (tawi) kwa sababu madd hizi sio za asili bali zimechipuka kutoka katika مَدُ الطَّبِيعي (maddutw-twabiy’iy) . مَدُّ الْفَرْعِي Maddul-Far-‘iy Hugawanyika sehemu mbili kutokana na sababu inayopelekea kuwa madd:


Madd kutokana na hamzah
مَدُّ الْواجِبِ الْمُتَّصِل . 1 Maddul-Waajib Al-Muttaswil
مَدُّ الجْائزِ المنُْفصِل . 2 Maddul-Jaaiz Al-Munfaswil
مَ دُّ الصِّل ةِ الْكُبْرَى . 3 Maddusw-Swillatil-Kubraa

Madd kutokana na sukuwn
مَدّ الْعارِض لِلسُّكُون . 1 Maddul-‘aaridhwi lis-sukuwn
مَدّ ال لين . 2 Maddul-liyn
مَد الّلازِم . 3 Maddul-laazim

Madd kutokana na hamzah:
مَدُّ الْواجِبِ الْمُتَّصِل . 1 (Maddul-Waajib Al-Muttaswil) Na inaitwa ‘Waajib’ kwa kuwa Maqurraa wote wamekubaliana kuivuta zaidi kuliko مَدُ الطَّبِيعي (maddutw-twabiy’iy). Na inaitwa ‘Muttaswil’ kwa kuwepo hamzah na madd katika neno moja. Hukmu yake katika riwaayah ya Hafsw ‘an ‘Aaswim twariyq Ash-Shaatwibiyyah ni kuivuta ima kwa harakah nne au tano.



2 (Maddul-Jaaiz Al-Munfaswil) Ni kuwepo herufi ya madd mwisho wa neno, na kufuatiwa na hamzah katika mwanzo wa neno linaloifuatia. Huvutwa haraka nne mpaka tano.


Madd kutokana na sukuwn
مَدُّ الْعأرِض لِلسُّكُون .. 1 Maddul-‘aaridhw lis-sukuwn
Ni kuwepo baada ya herufi ya madd na baada yake sukuwn ’aaridhw kwa sababu ya kusimama. Hukmu yake kwa kila qiraa-ah inajuzu kuivuta katika hali tatu:
• Qaswr (kuifupisha) kama harakah mbili
• Tawasw-swutw (wastani) harakah nne
• Twuwl (kurefusha) harakah sita.



2 Maddul-Liyn
Hii ni madd ambayo ni tofauti na madd nyinginezo kwa sababu herufi zake ni tofauti kwani hizo zinajulikana ni ‘herufi za madd’ ( ا و ي ) zinazonasibiana na i’raab katika herufi ya kabla yake. Ama hii inajulikana kuwa ni ‘Harfulliyn’. Herufi za اللِّين (liyn) ni herufi za و au ي zinapokuwa saakin na kabla yake ni herufi iliyokuwa na fat-hah: ÏImeitwa اللِّين (liyn) kwa sababu ya kutamkwa kwake kwa usahali (ulaini) bila ya taklifu.


اللِّين (liyn)Ni kuwepo baada ya herufi ya اللِّين na baada yake sukuwn ’aaridhw kwa sababu ya kusimama. Hukmu yake ni kuvutwa harakah ima mbili au nne au sita kwa kila qiraaah


3 Maddul-Laazim
Ni kuwepo baada ya herufi ya madd herufi saakin yenye sukuwn ya asili ambayo inayothibiti wakati wa kusimama na kuunganisha. Maqurraa wamewafikiana katika kuivuta madd hii harakah sita. مَد الّلازِم (maddullaazim) na huvutwa haraka 6 inagawanyika sehemu mbili:
I. الْكَلِمِيّ Al-Kalimiyy (ya neno)
II. الحَْرْفِيّ Al-Harfiyy (ya herufi)

I. الْكَلِمِيّ Al-Kalimiyy (ya neno):
i. أل مَدّ الّلازِم الْكَلِمِيّ الْمُثَقَّل Al-Madd Al-Laazim Al-Kalimiyyi Al-Muthaqqal
Huitwa الْكَلِمِيّ (ya neno) kwa vile inatokana na neno. Huitwa الْمُثَقَّل (iliyo nzito) itakapokuja baada ya herufi ya madd herufi yenye shaddah. Itambulike kuwa herufi yenye shaddah asili yake ni herufi mbili zinazofanana; ya kwanza huwa ni saakin na ya pili ni yenye i’raab, hivyo ikatokea idghaam.



ii. الْمَدُّ اللاَّزِمِ الْكَلِمِيِّ الْمُخَفَّف Al-Madd Al-Laazim Al-Kalimiyyi Al-Mukhaffaf
Huitwa الْكَلِمِيِّ (ya neno) kwa vile inatokana na neno. Huitwa الْمُخَفَّف (khafifu) itakapokuja baada ya herufi ya madd herufi saakin isiyo na shaddah kwa maana, hapatoeki idghaam. Katika riwaayah ya Hafsw ‘an ‘Aaswim hakuna isipokuwa mara mbili pekee katika neno moja tu nalo ni tø9!#u katika Swurat
Yuwnus aya 51 na 91

II. الحَْرْفِيّ Al-Harfiyy: (ya neno)
الْمَد الّلازِمْ الحَْرْفِيّ Al-Madd Al-Laazim Al-Harfiyy ni madd inayopatikana katika herufi zilizokuja kwenye mwanzo wa Suwrah 29 za Qur-aan zinazoitwa:
الحُْرُوف الْمُقَطَّعة Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah (Herufi zilizokatika) kwa maana zinatamkwa kama herufi za hijaaiyyah. Jumla ya herufi hizo ni 14 ambazo zimeundwa katika ibara kadhaa mojawapo ni: طرق سمعك النصيحه
Baadhi ya hizi Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah zimekariri zaidi ya mara moja na kuzifanya jumla kuwa ni ishirini na tisa:


Herufi hizi zimegawika sehemu nne:
1. Isiyo na madd nayo ni الف) ا ) Alif -haivutwi kabisa.
2. Madd harakah mbili katika herufi za 1 حي طهر
3. Madd haraka mbili au nne au sita katika herufi ya عين) ع ) kwa kuwa inatekelezwa kwa مَدُّ اللِّين (maddul-liyn)
4. Madd harakah sita katika herufi za سنقص لكم (سين – نون – قاف – صاد – لام – كاف – ميم)


Imegawanyika katika sehemu mbili:
الْمَدُّ اللاَّزِمِ الحَْرْفِيّ المثَُقَّل -Al-Madd Al-Laazim Al-Harfiyy Al-Muthaqqal na الْمد الّلازِم الحَْرْفِيّ الْمُخَفَّف - Al-Madd Al-Laazim Al-Harfiyy Al-Mukhaffaf

 

Mwisho:

Katika somo linalofuata tutakwenda kujifunz akuhusu sijda kwenye kusoma quran.

 






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu image Tarehe 2024-07-14 18:11:17 Topic: Darsa za Tajwid Main: Masomo File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 324


Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉5 Simulizi za Hadithi Audio     👉6 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Tajwid somo la 20: hukumu za madd twab'iy yaani madd ya asili
Katika somo hili utakwend akujifunza kw akirefu kuhusu madd twab’iy yaani madd za asili. Soma Zaidi...

Tajwid somo la 2: herufi saba katikausomaji wa quran
Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu herufi saba katika usomaji wa tajwid. Soma Zaidi...

Tajwid somo la 6: sifat al khuruf
hapa utakwenda kujifunza kuhusu sifa za herufi za kiarabu Soma Zaidi...

Tajwid somo la 1: Maana ya elimu ya Tajwid na kanuni zake
Katika somo hili utakwend akujifunza maana ya elimu ya tajwid kisheria. Pia utajifunza hukumu ya kusoma tajwid. Soma Zaidi...

Tajwid somo la 21: hukumu za madd far’iy
Katika somo hili utakwend akujifunz akuhusu madd far’iy katika usomaji wa Quran tajwid. Soma Zaidi...

Tajwid somo la 16: hukumu za tafkhim na tarqiq
Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu hukumu za tafkhim na tarqiq Soma Zaidi...

Tajwid somo la 13: sheria za Al-ikhfaa
Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu hukumu za Al ikhfaa katika usomaji wa Tajwid Soma Zaidi...

Tajwid somo la 18: hukumu za waqf wal ibtidai
Katika somo hili utakwend akujifunz akuhusu hukumuza waqfu katika usomajiwa quran. Soma Zaidi...

Tajwid somo la 15: hukumu za qalqala
Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu hukumu za Qalaqala katika usomaji wa tajwid. Soma Zaidi...

Tajwid somo la 19: hukumu za madd na aina zake
Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu madd na aina zake. Utajifunza herufi za madd na umuhimu wa madd katika tajwid. Soma Zaidi...

Tajwid somo la 4: umuhimu wa kusoma Tajwid
Katika somo hili utakwend akujifunza kuhusu umuhimu wa kusoma elimu ya tajwid. Soma Zaidi...

Tajwid somo la 10: hukumu ya idhhar
Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu hukumu za idhhar na mifano yake. Soma Zaidi...